Loading...
title : WATANZANIA WAMEANZA KUIELEWA CHEKO BILAKIKOMO: CHUCHU DOTE.
link : WATANZANIA WAMEANZA KUIELEWA CHEKO BILAKIKOMO: CHUCHU DOTE.
WATANZANIA WAMEANZA KUIELEWA CHEKO BILAKIKOMO: CHUCHU DOTE.
Na.John Luhende
Mwamba wa habari
Msanii wa sanaa za kuchekesha majukwaani , ambaye pia ni Mratibu wa Stand Up Comedy cheko bila kikomo, Angel Massaburi (Chuchu dote) amewashukuru watanzania na mashabiki wa mchezo huu kwa kujitokeza kwa wingi kuwaungamkono katika onyesha lao lililofanyika kwa kufana mwishoni mwa juma katika ukumbi wa Title Theater Oyeserbay Jijini Dar es salaam.
Akizungumza baada ya onyesho hilo Angel, ambaye anatumia jina la Chuchu dote , katika mitandao ya kijamii, amesema kilasiku wanapo andaa onyesho kumekuwa na mabadiliko ya mwitikio wa watu katika mahudhurio jambo ambalo yeye na wasanii wenzake linawatia moyo katika kazi yao.
“Mwakajana mwezi wa kumi na moja tulifanya onyesho lilikuwa zuri lakini nimeona laleo limefana zaidi kama unavyo ona watu wamejitokeza kwa wingi hii inaonyesha jinsi watanzania wameanza kuielewa sanaa hii , kwa wenzetu nchi za nje ni sanaa maarufu inayo pendwa sana ,nawaomba watanzania waendelee kutu unga mkono”Alisema.
"Sanaa inakua taratibu hivyo kazi yetu itafika mbali hasa kutokana na ushindani uliopo kwenye tasnia, kuna mambo mengi ya kufanya katika kazi yetu hasa ukizingatia kwamba kuchekesha mtu sio jambo jepesi kama wengi wanavyofikiria, tutaendelea kujituma na kufanya kazi nyingi na maonyesho zaidi," Alisema Chuhu.
Kwa upande wake Ramadhani Kilasi (Makuzi Comedian ) amesema watanzania sanaa hii walikuwa bado hawajaifahamu sana walizoea kuangalia mtandaoni kutoka nchi zanje hivyo Cheko bila kikomo imekuja kuwaonyesha kwa ukaribu zaidi uzuri wa sanaa hii.
“Hatuna majina makubwa sana lakini nawaomba watanzani tunapo kuwa na maonyesho kama haya wajitokeze kwa wingi tuna vitu vikubwa vya kuwaonyesha sanaa hii ninzuri sana”
Mwamba wa habari imezungumza na baadi ya mashabiki wailio hudhuria onyesho hilo ambapo Rachael Michael, amewapongeza wasanii hao kwa kwa umahili wao kwani wamekonga nyoyo za mashabiki wamecheka na kufurahi.
“Kazi ya kumchesha mtu nikazi ngumu sana , lakini hawa wameweza watu wote nimewaona wakati wa onyesho wanakicheka sana wasanii wetu wameonyesha ukomavu mkubwa Mungu awasaidie wasonge mbele”Alisema
Hivyo makala WATANZANIA WAMEANZA KUIELEWA CHEKO BILAKIKOMO: CHUCHU DOTE.
yaani makala yote WATANZANIA WAMEANZA KUIELEWA CHEKO BILAKIKOMO: CHUCHU DOTE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WAMEANZA KUIELEWA CHEKO BILAKIKOMO: CHUCHU DOTE. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/watanzania-wameanza-kuielewa-cheko.html
0 Response to "WATANZANIA WAMEANZA KUIELEWA CHEKO BILAKIKOMO: CHUCHU DOTE."
Post a Comment