Loading...

Wavuvi wanne Kizimbani kwa uvuvi haramu

Loading...
Wavuvi wanne Kizimbani kwa uvuvi haramu - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wavuvi wanne Kizimbani kwa uvuvi haramu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wavuvi wanne Kizimbani kwa uvuvi haramu
link : Wavuvi wanne Kizimbani kwa uvuvi haramu

soma pia


Wavuvi wanne Kizimbani kwa uvuvi haramu

Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii. 

WAVUVI wanne wakazi wa jijini Dar es Salaam,  leo Februari 4.2019 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za  kukutwa wakitumia vifaa vya kuvulia ambavyo vimekatazwa kinyume cha sheria namba 66(2)(q) na (4) ya sheria ya Uvuvi ya mwaka 2009.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi Maria Kasonde Wakili wa Serikali Sada Mohamed  amewataja washtakiwa hao kuwa ni Athumani Fakih (42), Mbwana Fakih (61), Mohamed Ushanga (38) na Khalifa Abdallah wote wakazi wa Kigamboni.
Wakili Saada amedai,katika shtaka la kwanza, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa,  Novemba 3, mwaka jana,  wakiwa katika bahari ya Hindi eneo la Fungu Baraka lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam walikutwa wakivua kwa kutumia nyavu ambazo zilikuwa chini ya kiwango au zimekatazwa. 

Katika shtaka la pili, imedaiwa,  siku hiyo hiyo washtakiwa wakiwa katika bahari ya Hindi eneo la Fungu Baraka Kigamboni jijini Dar es Salaam walikutwa wakitumia vifaa vya kuvulia vilivyokatazwa ambavyo ni mitungi ya gesi 28, leguleta sita, pea tatu za viatu vya kuvulia samaki pamoja vifaa 13 vya kuvulia samaki (mask to capture fish). 

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama.  Ambapo wametakiwa kila mmoja kuwa mdhamini mmoja wenye barua ya utambulisho ya serikali za mitaa,  vitambulisho na Pia wametakiwa kusaini bondi ya Sh. Milioni 10 kila mmoja.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi Februari 18, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. 


Hivyo makala Wavuvi wanne Kizimbani kwa uvuvi haramu

yaani makala yote Wavuvi wanne Kizimbani kwa uvuvi haramu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wavuvi wanne Kizimbani kwa uvuvi haramu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/wavuvi-wanne-kizimbani-kwa-uvuvi-haramu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wavuvi wanne Kizimbani kwa uvuvi haramu"

Post a Comment

Loading...