Loading...
title : WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA TERMINAL THREE YA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM
link : WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA TERMINAL THREE YA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM
WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA TERMINAL THREE YA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM
Na Bahati Mollel
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema leo kuwa ameridhishwa na ujenzi wa mradi wa Jengo ka Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB III), wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
Mhe. Majaliwa amesema amefarijika kusikia ujenzi wa jengo hilo umekamilika kwa asilimia 95.05, ambapo imebaki asilimia 4.5 pekee kukamilika.
“Nawapongeza wakandarasi, Tanroads na wote mliopata ajira ya ujenzi wa jengo hili naamini sasa mmekuwa wataalam hodari, kwani jengo ni zuri, linavutia na lenye ubora nimeona maeneo muhimu pale pa kuondokea abiria, sehemu ya kupokelea mizigo na kwenye madaraja ambapo kote nimefarijika kwa kiasi kikubwa ujenzi unakwenda vyema,” amesema Mhe. Majaliwa.
Amesema mbali na ujenzi huo pia amefurahishwa na ukuta unaotambulika kama “Wall of Tanzania” ambao unaonyesha picha za vivutio mbalimbali ukiwemo mlima mrefu Barani Afrika, Mlima Kilimanjaro, wanyama Twiga, Tembo, Pundamilia, Nyumbu, Simba na Chui, ambao hutambulisha wageni kuwa tayari wamewasili Tanzania na wataweza kuona vivutio hivyo.
“Hizi picha ni nembo ya Kitanzania, na hapa zimekaa sehemu nzuri sana kila mgeni anapowasili na kufika eneo hili la kuchukulia mizigo anaona kweli amefika Tanzania kwani zinawakaribisha wageni, na hii ni faraja kwa kuwa jitihada za serikali za kuleta maendeleo zinafanyika vyema,” amesema Mhe. Waziri Mkuu.
Mhe. Majaliwa pia amekuwa na faraja kubwa kusikia jengo hilo litaweza kuhudumia abiria milioni sita (6) kwa mwaka, na kwa majengo yote likiwemo Jengo la Kwanza na la Pili jumla yataweza kuhudumia abiria milioni nane (8) kwa mwaka, ambapo pia kumekuwa na miundombinu kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum.
Hatahivyo, amesema anaamini Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imeanza taratibu za kuhakikisha mara baada ya kukabidhiwa jengo hilo kutoka kwa Wakandarasi mwezi Mei, 2019 wataweza kujiendesha, kwa kuanza na abiria moja kwa moja.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), ambao ndio wasimamizi wa ujenzi Mhandisi Patrick Mfugale awali alimweleza Mhe. Majaliwa kuwa ujenzi wa jengo hilo umekamilika kwa asilimia 95.05, ambapo eneo la maegesho ya ndege linaweza kuegesha ndege 19 za darala C, na 11 daraja E na jengo linaweza kuhudumia abiria 2,800 kwa saa muda ambao abiria ni wengi.
Hatahivyo, Mhandisi Mfugale amemhakikishia Mhe,. Majaliwa kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati na viwango vilivyowekwa, amesema jengo hilo litakabidhiwa kwa serikali tarehe 31 Mei, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu.

Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale akisoma taarifa ya Ujenzi wa mradi wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), leo alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
Kiongozi Mkuu wa Timu ya Wataalam wa Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi Julius Ndyamukama (aliyenyoosha mkono) akimuonesha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ukumbi wa abiria wanaoondoka katika jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia aina ya viti vya abiria vitakavyotumika kwenye Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) alipotembelea leo. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Bi. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Ilala na wa pili kushoto ni Mhandisi Julius Ndyamukama, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 
Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiaga wakati alipoondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Terminal Three, jijini Dar es salaam baada ya kukagua ujenzi wa uwanja huo ambao umekamilika kwa asilimin 95 na unarajiwa kukamilika Mei mwaka huu.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu na TAAA
Hivyo makala WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA TERMINAL THREE YA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM
yaani makala yote WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA TERMINAL THREE YA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA TERMINAL THREE YA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/waziri-mkuu-akagua-ujenzi-wa-terminal.html
0 Response to "WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA TERMINAL THREE YA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM"
Post a Comment