Loading...

Zahanati ya Kinyerezi kuwa kituo cha Afya

Loading...
Zahanati ya Kinyerezi kuwa kituo cha Afya - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Zahanati ya Kinyerezi kuwa kituo cha Afya, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Zahanati ya Kinyerezi kuwa kituo cha Afya
link : Zahanati ya Kinyerezi kuwa kituo cha Afya

soma pia


Zahanati ya Kinyerezi kuwa kituo cha Afya


Na Heri Shaban
Mwambawahabari
MANISPAA ya Ilala inatarajia kupandisha adhi zahanati ya Kata ya Kinyerezi kuwa kituo cha Afya kutokana na kuongezeka idadi wagonjwa wanaopewa huduma


Hayo yalisemwa Dar es salaam Jana Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri wakati wa kupokea msaada wa Vifaa vya Zahanati ya Kata hiyo vilivyotolewa na Benki ya NMB.

"Kutokana na kupokea idadi kubwa ya wagonjwa zahanati ya Kata hii na kuonyesha mafanikio mazuri Manispaa yangu ya Ilala tutaipanua majengo yaliopo eneo ili na kujenga majengo mengine ili iweze kuitwa Kituo cha Afya."alisema Shauri

Shauri alisema Manispaa ya Ilala ina Jumla ya zahanati 25 kwa sasa na vituo vya Afya vitatu na mwaka 2019/2020 imetenga bilioni 1.5 kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Ilala KIVULE katika upanuzi wa zahanati  ,zahanati ya Kata ya Kinyerezi itawekwa katika  orodha ya kupandishwa adhi kuwa kituo cha Afya.

Aliwapongeza Benki ya NMB kwa kuisaidia sekta ya Afya na kusema kuwa katika Maendeleo lazima afya iweze kuimalika.

 Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kinyerezi Dkt. Isack Makundi alisema  zahanati hiyo ina hudumia wakazi zaidi ya 60,000 katika mitaa sita, Kinyerezi, Kanga,Kwalimbanga,Kifuru,Kibaga na Kichangani.


Dkt Makundi alisema pia zahanati hiyo inatoa huduma kwa wagonjwa wanaoizunguka kata hiyo wakiwemo Mbenzi, Ukonga, Segerea, Bonyokwa na Tabata.

Alisema ina watumishi kwa sasa 23 idadi ya Wagonjwa kwa siku 450 hadi 500 kwa wiki wagonjwa 3000  changamoto watumishi waliopo wachache ,uchakavu wa jengo.

Naye Meneja wa Benki ya NMB Air Port Restus Asenga alisema  wanatambua juhudi za Rais wa awamu ya tano John Magufuli kwa kusimamia elimu na afya Kwa nguvu zote kwa kutoa elimu bure Shule za Msingi na sekondari pia kuboresha hutoaji wa huduma za Elimu na afya mjini na vijijini .

Alisema ingawa Serikali ina Fanya makubwa Kama benki ya NMB wajibu wetu kuunga mkono juhudi za Maendeleo kwa kusaidia Jamii .

"Benki ya NMB tumeamua kushirikiana na zahanati ya Kinyerezi pamoja na Jamiii inayozunguka kituo hichi kwa kuchangia vitanda vya Wagonjwa vitano, pamoja na magodoro yake, vitanda vya kujifungulia viwili mashuka 20  "alisema Assenga.




Hivyo makala Zahanati ya Kinyerezi kuwa kituo cha Afya

yaani makala yote Zahanati ya Kinyerezi kuwa kituo cha Afya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Zahanati ya Kinyerezi kuwa kituo cha Afya mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/zahanati-ya-kinyerezi-kuwa-kituo-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Zahanati ya Kinyerezi kuwa kituo cha Afya"

Post a Comment

Loading...