Loading...

ZANTEL Yazindua Promosheni ya Watumiaji wa Huduma ya EZYPESA

Loading...
ZANTEL Yazindua Promosheni ya Watumiaji wa Huduma ya EZYPESA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ZANTEL Yazindua Promosheni ya Watumiaji wa Huduma ya EZYPESA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ZANTEL Yazindua Promosheni ya Watumiaji wa Huduma ya EZYPESA
link : ZANTEL Yazindua Promosheni ya Watumiaji wa Huduma ya EZYPESA

soma pia


ZANTEL Yazindua Promosheni ya Watumiaji wa Huduma ya EZYPESA

Mkuu wa Masoko na Huduma ya Fedha za simu za mkononi wa Zantel, Sakyi Opoku, akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wa Zantel
 Mkuu wa Huduma na Bidhaa wa Zantel, Aneth Muga, akifafanua jambo kwa waandishi wakati wa uzinduzi huo.
 Meneja Bidhaa Kitengo cha EZYPESA wa Zantel, Leonard Kameta, akiongea wakati wa uzinduzi huo
 Mkuu wa Masoko na Huduma ya Fedha za simu za mkononi wa Zantel, Sakyi Opoku (kushoto) akimkabidhi simu mwandishi wa gazeti la The Guardian, Beatrice Philemoni, baada ya kujishindia simu kupitia droo ndogo ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
 Wafanyakazi wa Zantel wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi huo
Wafanyakazi wa Zantel wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi huo
Kampuni ya mawasliano Zantel, imezindua promosheni kwa watumiaji wa huduma yake ya kifedha ijulikanayo kama EzyPesa ili kuwezesha wateja wake kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu.

Promosheni hii itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu, ni rasmi kwa ajili ya wateja wote wanaotumia Ezypesa pamoja na wateja wapya wanaoendelea kujiunga na huduma hio. 

Kila mara mteja atakapotuma ama kupokea fedha kupitia EzyPesa, atajiweka kwenye nafasi ya kujishindia zawadi nono kama simu za mkononi zinazotumia interneti (Smartphones) na fedha taslimu kuanzia shilingi 200,000/- hadi shilingi 1,000,000/- 

 Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko na Huduma za kifedha kupitia simu za mkononi wa Zantel, Sakyi Opoku, alisema promosheni hii itawezesha watumiaji wa huduma ya EzyPesa kujipatia motisha kama vile kurudishiwa fedha kwenye akaunti zao na kujishindia zawadi mbalimbali.

 Watumiaji wa huduma ya EzyPesa watakaongeza salio la muda wa maongezi kuanzia shilingi 500/- watarudishiwa fedha zao. Wateja watakaotuma au kupokea kiasi cha shilingi 10,000/-wataingia kwenye droo ya wiki inayowezesha kujishindia simu ya kisasa (Smartphone). 

Kila wiki droo itakuwa na washindi 10 wa fedha taslimu na washindi 15 wa simu. Droo ya mwezi italenga kuwapata wateja 10 waliotuma na 10 waliopokea fedha kwa wingi.

 EzyPesa ndio huduma pekee ya mtandao hapa Tanzania inayowezesha wateja wake kufanya miamala ya malipo ya kodi kwa ZBR na kununua umeme wa LUKU na TUKUZA. Huduma ya EzyPesa inaondoa adha ya wateja kupoteza muda mwingi wakipanga foleni ili kupata huduma za kibenki na kulipa ankra zao mbalimbali. 

Vile vile, EzyPesa sasa inapatikana katika program mpya ya simu za mkononi (Mobile Application) inayowezesha wateja kufanya malipo mbalimbali kwa njia rahisi zaidi. Kwa sasa wastani wa miamala inayofanyika kwa mwezi kupitia huduma hii inafika million 5.6 na Zantel ina malengo ya kufikisha huduma hio kwa wateja 100,000 wapya kila mwezi. 

Zantel pia inaendelea kufanya majadiliano na taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo benki za CRDB na NBC kuhusu ushirikiano katika kutoa huduma za kifedha kupitia mtandao wake.


Hivyo makala ZANTEL Yazindua Promosheni ya Watumiaji wa Huduma ya EZYPESA

yaani makala yote ZANTEL Yazindua Promosheni ya Watumiaji wa Huduma ya EZYPESA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ZANTEL Yazindua Promosheni ya Watumiaji wa Huduma ya EZYPESA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/zantel-yazindua-promosheni-ya-watumiaji.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ZANTEL Yazindua Promosheni ya Watumiaji wa Huduma ya EZYPESA"

Post a Comment

Loading...