Loading...

ARUSHA UNITED YAJITOA RASMI LIGI DARAJA LA KWANZA

Loading...
ARUSHA UNITED YAJITOA RASMI LIGI DARAJA LA KWANZA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ARUSHA UNITED YAJITOA RASMI LIGI DARAJA LA KWANZA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ARUSHA UNITED YAJITOA RASMI LIGI DARAJA LA KWANZA
link : ARUSHA UNITED YAJITOA RASMI LIGI DARAJA LA KWANZA

soma pia


ARUSHA UNITED YAJITOA RASMI LIGI DARAJA LA KWANZA

Na Woinde Shizza, Globu ya Jamii - Arusha

Timu ya mpira wa miguu ya mkoani Arusha ijulikanayo kwa jina la Arusha United (wana utalii) leo imetangaza rasmi kujitoa katika mashindano ya ligi daraja la kwanza Tanzania bara kwa kile kichodaiwa vurugu za mara kwa mara zinazotokea katika ligi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo, Mkurugenzi Mtendaji  wa timu hiyo, Otte Ndauka amesema kuwa timu hiyo imeamua kujitoa rasmi katika mashindano hayo kutokana na vurugu wanazofanyiwa mara kwa mara viwanjani wakati wakicheza michezo mbalimbali.

Amesema kuwa timu yao ya Arusha United imefanyiwa vurugu katika mechi mbalimbali ikiwemo mchezo nambari 69 wa ligi daraja la kwanza uliochezwa mjini Tabora mnamo February 2 mchezo uliochezwa katika kiwanja cha  Ali Hassan Mwinyi.

"Mchezo huu tulienda tulifika sikumoja kabla kwa mujibu wa sheria tulitakiwa kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo husika lakini jambo la kusikitisha sana na lisilo lakiugwana viongozi wa Rhino Rangers kwa kushirikiana na Meneja wa uwanja walifanya kila jitiada kuhakikisha hatufanyi mazoezi, Aidha pia katika mechi nyingine  tuliyocheza na klabu ya Polisi pia tulifanyiwa vurugu na sio timu tu au wachezaji wanafanyiwa vurugu hapana lakini pia waandishi wetu wanapigwa na hata kuna mmoja aliaribiwa vifaa vyake vya kazi" alisema Ndauka.

Alisema kuwa matukio yote ambayo yametokea wameandika barua TFF kulalamika pamoja na Bodi ya ligi lakini hakuna uamuzi wowote wa kinithamu ambao wameuchukua hivyo ndio maana wameamua kujitoa katika ligi hiyo.

Kuhusiana na swala la mikataba ya wacheza pamoja na mali za klabu hiyo walisema kuwa bodi ya timu hiyo inakaa chini na wachezaji kujadili kuhusiana na mikataba hiyo pia wanampango wa kuketi na bodi kujadili  kuhusiana na Mali hizo.

Akiongelea swala hilo Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha, Zakayo Mjema alisema kuwa wao kama chama hawajapata taarifa yoyote kuhusiana na timu hiyo kujitoa.


Hivyo makala ARUSHA UNITED YAJITOA RASMI LIGI DARAJA LA KWANZA

yaani makala yote ARUSHA UNITED YAJITOA RASMI LIGI DARAJA LA KWANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ARUSHA UNITED YAJITOA RASMI LIGI DARAJA LA KWANZA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/arusha-united-yajitoa-rasmi-ligi-daraja_21.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ARUSHA UNITED YAJITOA RASMI LIGI DARAJA LA KWANZA"

Post a Comment

Loading...