Loading...
title : ASASI ZA KIRAIA ZASHINDA KESI YA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI YA MWAKA 2016 DHIDI YA JAMUHURI
link : ASASI ZA KIRAIA ZASHINDA KESI YA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI YA MWAKA 2016 DHIDI YA JAMUHURI
ASASI ZA KIRAIA ZASHINDA KESI YA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI YA MWAKA 2016 DHIDI YA JAMUHURI
Na. Vero Ignatus,Arusha
Shauri Namba 2 la mwaka 2017 kati ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kituo cha Sheria na Haki na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania jana limeamuliwa na mahakama ya Afrika Mashariki ambapo waleta maombi wameishinda Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imesema baadhi ya vipengele katika Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 inakiuka uhuru wa kujieleza pia vinapingana na Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao Tanzania imeuridhia.
Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imetoa hukumu jana dhidi ya sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge Novemba 2, 2016 na kusainiwa na Rais.
Kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2017 ilifunguliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wakilalamikia ukandamizaji wa uhuru wa habari.
Hivyo upande wa waleta maombi waliomba mahakama itamke kuwa; 1. Vifungu vya 7 (3) (a) (b) (c) (f) (g) (h) (i) na (j), 13, 14, 18, 19, 20, 21, 35, 36, 37, 38, 39, 40, 50, 54, 52, 53, 58, na 59 vya Sheria ya Huduma za Habari, 2016 vifutwe kwa kuwa vinaminya uhuru wa habari
Vipengele vilivyolalamikiwa vipo 18, walalamikaji wakiiomba mahakama hiyo itamke kwamba vipengele hivyo vinakiuka mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuilazimisha serikali kuvifuta kabisa.
Hukumu hiyo imesomwa jana Alhamisi Machi 28, mbele ya Jopo la majaji watatu Jaji Charles Nyachae, Monica Mugenyi na Jaji Justice Ngie.
Akisoma hukumu hiyo Jaji Nyachae amesema vifungu vilivyo kwenye sheria hiyo ni vibovu na vinavyokiuka mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo ameitaka Serikali ya Tanzania kurekebisha vifungu vya Sheria ya Uhuru wa Habari kutokana na kukiuka Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
"Sheria hii inapaswa kufanyiwa marekebisho ili iendane na mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya," amesema Jaji Nyachae.
Wadai halo walikua wakitetewa na mawakili, Fulgence Massawe, Jebra Kambole, Mpale Mpoki , Donald Deya na Jenerali Ulimwengu.
Mahakama ya EACJ imekubaliana na walalamikaji kuwa vifungu katika sheria ya Huduma ya Habari vya (3)(a), 13, 1920, 21,34 pamoja na vifungu vingine vinakiuka utawala bora, demokrasia na utawala unaozingatia sheria na inapingana na mkataba ulioanzisha EAC.
Mara baada ya hukumu hiyo, Wakili kiongozi wa walalamikaji, Fulgence Massawe amesema ushindi huo ni wa kihistoria na unathibitisha hoja za wadau mbalimbali walizokua wakisema sheria hiyo siyo nzuri kwa maslahi mapana ya nchi.
Hivyo makala ASASI ZA KIRAIA ZASHINDA KESI YA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI YA MWAKA 2016 DHIDI YA JAMUHURI
yaani makala yote ASASI ZA KIRAIA ZASHINDA KESI YA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI YA MWAKA 2016 DHIDI YA JAMUHURI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASASI ZA KIRAIA ZASHINDA KESI YA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI YA MWAKA 2016 DHIDI YA JAMUHURI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/asasi-za-kiraia-zashinda-kesi-ya-sheria.html
0 Response to "ASASI ZA KIRAIA ZASHINDA KESI YA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI YA MWAKA 2016 DHIDI YA JAMUHURI"
Post a Comment