Loading...
title : Biteko asema ufahari wa kiongozi uwe kwenye kuwatumikia Wananchi
link : Biteko asema ufahari wa kiongozi uwe kwenye kuwatumikia Wananchi
Biteko asema ufahari wa kiongozi uwe kwenye kuwatumikia Wananchi
Na Issa Mtuwa – Bukombe
Waziri wa Madini ambae pia ni Mbunge wa Bukombe Mhe. Doto Biteko amesema viongozi wa serikali wajibu wao mkubwa ni kuwatumikia wananchi, dhamana yao ya madaraka kama haina msaada kwa wananchi haina maana, yeye kama waziri na mbunge kama shida na matatizo ya wanchi wa Bukombe na sekta nzima ya madini atashindwa kuzitatua haina maana ya uwepo wake na ndio maana anaumiza kichwa kila siku kuhakiksha sekta ya Madini inaleta tija kwa taifa huku pia wananchi wa Bukombe wanaozungukwa na Madini ya dhahabu pia wananufaika.
Biteko ameyasema hayo leo tarehe 02/03/2019 akihutubia wananchi kwa nyakati tofauti tofauti wilaya ya Bukombe katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu katika mkoa wa geita ambapo pamoja na mambo mengine anasikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi na zinazo husu sekta ya madini.
“ Rais Pombe Joseph Magufuli amekuwa akituambia mara kwa mara nendeni mkawahudumie Watanzania muwaondolee kero, ule mfumo wa watu wakiwa ofisini anakuwa Boss Magufuli hataki mfumo huoo, anataka mabosi wawe wananchii, wananchi wasikilizwe kama wana jambo litatuliwe na kama haliwezekani waambiwe ukweli sio kudanganya” amesema Biteko.
Amesema Bukombe inautajiri wa madini ya dhahabu na endapo kila mmoja atajishugulisha katika kutafuta kwa kutumia fursa zilizopo maisha ya wana Bukombe yataboreka, ametoa wito kwa vijana, akina mama na kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi ajishugulishe.
Aidha, ameongeza kwa kusema wajibu alionao kama Waziri wa Madini ni kuhakikisha kodi na malipo mbalimbali yanayohusiana na madini yanalipwa tena kwa wakati, na jamii zinazo zunguka migodi zinachangia maendeleo ya wananchi hao kama sheria inavyo wataka.
‘Msiwakamue sana hawa wawekezaji kwa sababu wanatumia fedha nyingi katika kuwekeza, sio kila shida ya kijiji, kata au wilaya mnakimbilia kwa mwekezaji wa mgodi hapaaaaaa! lakini sizui kuwaomba msaada lakini kuwe na kipimo yale ya kisheria waacheni watekeleze ili wasipo timiza mimi nitawabana” aliongeza Biteko.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akiongea kwenye kikao cha ndani na viongozi waandamizi wa Wilaya ya Bukombe katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Mkumba akisoma taarifa ya wilaya hiyo kwa Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Bukombe ambae ameanza ziara ya siku tatu wilayani humo.
.Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akihutubia wananchi mbalimbali wa kata ya wakiwa kwenye mkutano wa pamoja katika Vijiji wilayani Bukombe.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko mwenye Tshirt ya Njano akimsikiliza msimamizi wa ujenzi wa Zahanati katika kata ya Wakati wa ziara yake Wilayani Bukombe ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo.
Hivyo makala Biteko asema ufahari wa kiongozi uwe kwenye kuwatumikia Wananchi
yaani makala yote Biteko asema ufahari wa kiongozi uwe kwenye kuwatumikia Wananchi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Biteko asema ufahari wa kiongozi uwe kwenye kuwatumikia Wananchi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/biteko-asema-ufahari-wa-kiongozi-uwe.html
0 Response to "Biteko asema ufahari wa kiongozi uwe kwenye kuwatumikia Wananchi"
Post a Comment