Loading...

CHECHE KURUDISHA SOKA LA PASI NA KASI KWENYE KIKOSI CHA AZAM

Loading...
CHECHE KURUDISHA SOKA LA PASI NA KASI KWENYE KIKOSI CHA AZAM - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CHECHE KURUDISHA SOKA LA PASI NA KASI KWENYE KIKOSI CHA AZAM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CHECHE KURUDISHA SOKA LA PASI NA KASI KWENYE KIKOSI CHA AZAM
link : CHECHE KURUDISHA SOKA LA PASI NA KASI KWENYE KIKOSI CHA AZAM

soma pia


CHECHE KURUDISHA SOKA LA PASI NA KASI KWENYE KIKOSI CHA AZAM

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BENCHI la ufundi la muda la Azam FC kwa sasa linafanya kazi kubwa ya kurudisha aina ya mpira uliozoeleka kwenye timu hiyo wa kucheza soka la pasi na kasi uwanjani.

Kwa muda wa wiki moja sasa, kikosi cha timu hiyo kipo chini ya makocha wa muda Meja Mstaafu, Abdul Mingange na Idd Nassor Cheche, wakishika nafasi hizo baada ya kustitishiwa mikataba kwa makocha Hans Van Der Pluijm na Msaidizi wake, Juma Mwambusi.

Wawili hao waneiongoza Azam katika michezo miwili na kuifanikisha timu hiyo kushinda na kuingia hatua ya nane bora Kombe la FA pamoja na ushindi wa goli kuu wa kwanza baada ya muda mrefu.

Katika mchezo wa pili dhidi ya African Lyon uliochezwa mwishoni mwa wiki hii Azam  walifanikiwa kupata ushindi wa goli 3-1 ukiwa ni muendelezo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), awali wakipata ushindi mwingine mnono walipoipiga Rhino Rangers 3-0 na kutinga robo fainali ya Kombe la FA.

Kocha wa muda wa timu hiyo Cheche amesema kwa sasa wanataka kurudisha aina ya soka la timu hiyo ili kuleta ushindani na usumbufu kwa timu pinzani kwenye mechi zinazokuja.

“Kwanza Azam ina aina yake ya mchezo ambayo ilikuwa inacheza tofauti, tunajaribu kurudisha mchezo wenye pasi nyingi na spidi ndio tunajaribu kupambana nao, kurudisha wachezaji warudi katika ile hali kuleta ushindani na usumbufu kwa timu pinzani, ndio kitu tunachokifanya sasa hivi, kunyanyua spidi ya wachezaji ambayo ilikuwa ipo chini,” alisema.

Akizungumzia kwa ufupi mchezo uliopita dhidi ya Lyon, Cheche alisema kiujumla ulikuwa ni mzuri huku akikiri kuwa kuna mambo madogo madogo wamekuwa wakizifanyia kazi ili kuondoa baadhi ya makossa yanayoonekana.

“Mchezo tulianza taratibu lakini kadiri tunavyokwenda tumeenda tikibadilika na kufuata yale maelekezo tuliyowapa na mabadiliko tuliyofanya katika kipindi cha pili yameweza kutusaidia kuleta mabadiliko ambayo yametupa ushindi,” alisema Cheche.

Baada ya kumaliza changamoto ya mchezo huo, Azam FC imerejea tena  t mazoezi leo Jumatatu tayari kuanza maandalizi ya mchezo ujao wa ligi, itakaocheza dhidi ya JKT Tanzania Machi 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex.



Hivyo makala CHECHE KURUDISHA SOKA LA PASI NA KASI KWENYE KIKOSI CHA AZAM

yaani makala yote CHECHE KURUDISHA SOKA LA PASI NA KASI KWENYE KIKOSI CHA AZAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CHECHE KURUDISHA SOKA LA PASI NA KASI KWENYE KIKOSI CHA AZAM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/cheche-kurudisha-soka-la-pasi-na-kasi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "CHECHE KURUDISHA SOKA LA PASI NA KASI KWENYE KIKOSI CHA AZAM"

Post a Comment

Loading...