Loading...
title : CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) KUJENGA TAWI MKOA WA SIMIYU
link : CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) KUJENGA TAWI MKOA WA SIMIYU
CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) KUJENGA TAWI MKOA WA SIMIYU
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeahidi kujenga tawi jipya Wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu katika kata ya Sapiwi. Ili kusogeza huduma ya elimu karibu na wananchi. Chuo hicho kilifanya ziara mkoani Simiyu mnamo tarehe 26 Machi 2019 na kuonana na uongozi wa Mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa chuo cha Usimamizi wa Fedha,Profesa Tadeo Satta akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Antony Mtaka alimhakikishia kwamba chuo kitajenga tawi jipya ili kuwasogezea huduma wananchi wa mkoa huo.
Pia, Mkuu wa Chuo aliushukuru uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa kutoa ekari 20 bure na alihaidi kushirikiana na Serikali ya mkoa kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati.
Profesa satta aliuomba uongozi wa Mkoa kukisaidia Chuo kupata hati miliki mapema iwezekanavyo , na uongozi wa mkoa ushirikiane na chuo katika hatua zote ikiwamo upimaji wa eneo hadi ujenzi na ukamilishaji wa majengo ya chuo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Antony Mtaka akizungumza na uongozi wa chuo, alisema eneo waliopewa IFM ni eneo zuri ambalo lipo karibu kiwanja cha ndege kinachotarajiwa kujengwa, viwanja vya Nanenane na eneo ambalo viwanda vinavyotarajiwa kujengwa.
Pia alisisisitiza kwamba serikali ya mkoa iko tayari kushirikiana na chuo kwa kutoa wataalamu watakaosaidia katika usimamizi wa upimaji huku akiwashauri ujenzi wa majengo ya chuo hicho ufanyike kwa kutumia mfumo wa “force account” ili kupunguza gharama za ujenzi.
Mkuu wa mkoa alisisitiza kuwa mfumo huo utapunguza gharama kwa kuwa hautumii wakandarasi badala yake ujenzi utafanywa na mafundi wa kawaida wakisimamiwa na wahandisi wa ujenzi wa mkoa na halmashauri.
Pia mkuu wa Mkoa, aliwahakikishia uongozi wa Chuo kwamba Simiyu ina wanafunzi wengi ambao wanamaliza kwa wingi hawana pa kwenda, ili kupata elimu inawalazimu kusafiri mbali ikiwemo Mwanza, Shinyanga na Musoma . Alitoa mfano kwa mwaka huu wapatao wanafunzi elfu kumi wanatarajiwa kumaliza kidato cha nne. Hivyo basi chuo kikifungua tawi Simiyu watapata wanafunzi wengi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bw.Jumanne Sagini, alisema kwamba Mkoa unatoa nafasi kwa taasisi mbalimbali za elimu ya juu kuja kujenga taasisi zao simiyu , na alisisitiza kwamba mkoa unakaribisha fursa mbalimbali zingine. Lengo likiwa kuwasaidia wana Simiyu kujiendeleza ya kichumi na kifikra.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bw. Jumaane Sagini akipiana mkono na Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Profesa Tadeo Satta.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (katikati) Mhe. Antony Mtaka akiwa na uongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha uliofanya ziara Mkoani Simiyu, kushoto kwake (mwenye tai) ni Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Profesa Tadeo Satta.
Ujumbe wa chuo cha usimamizi wa fedha ukiongozwa na Mkuu wa Chuo Profesa Tadeo Satta ( mwenye tai) wakiwa wanaoneshwa eneo lililopo katika kata ya Sapiwi ambalo chuo limepewa na uongozi wa Mkoa wa Simiyu.
Hivyo makala CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) KUJENGA TAWI MKOA WA SIMIYU
yaani makala yote CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) KUJENGA TAWI MKOA WA SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) KUJENGA TAWI MKOA WA SIMIYU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/chuo-cha-usimamizi-wa-fedha-ifm-kujenga.html
0 Response to "CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) KUJENGA TAWI MKOA WA SIMIYU"
Post a Comment