Loading...
title : DAS ILALA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TANKI LA MAJI MAJOHE
link : DAS ILALA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TANKI LA MAJI MAJOHE
DAS ILALA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TANKI LA MAJI MAJOHE
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Tanki la Maji lenye uwezo wa kuhifadhi Lita 150,000 kwa siku katika Mtaa wa Kichangani Majohe Jijini Dar es Salaam.
Akiweka jiwe la Msingi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Katibu Tawala DAS Sheila Edward amesema kuwa mradi huu utawasaidia wananchi wa eneo hilo kwa kuwapunguzia kero ya maji waliyonayo kwa muda mrefu.
Amesema, serikai inaendelea kutekeleza ahadi za serikali ya mapinduzi ili kufikia malengo ya kumtua mama ndoo kichwani na wamekuwa wanashirikiana na madiwani kwani marndeleo hayana chama.
DAS amesema, Uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa maji Mtaa wa Kichangani Majohe utasaidia wananchi takribani laki saba (700,000) na amezitaka mamlaka husika kusimamia mradi huo pindi utakapomalizika ili uweze kujiendeleza.
Kaimu Mkurugenzi Wa Manispaa ya Ilala Mhandisi Upendo Lugongo amesema kuwa mradi huo wa maji umejengwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA na utawasaidia wananchi wote wanaoishi mtaa wa Kichangani Mahoje.
Amesema kuwa, gharama za mradi huo ni takribani milioni 230 na unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa nne na lengo kuu ni kupunguza kero ya maji kwa wananchi.
Upendo amesema, serikali kwa kushirikiana na mamlaka za maji wanaendelea kushirikiana kwa pamoja kupeleka maji kwenye maeneo ambayo hayakuwa na mtandao wa maji na kufikia lengo la asilimia 95 mwaka 2020.
“Kuna mradi mwingine wa maji unaosimamiwa na DAWASA wa Ujenzi wa tanki la Kisarawe ambapk kufikia mwishoni mwa mwaka huu wananchi wote wa Majohe na Gongo la Mboto kaa ujumla watapata majisafi na salama,”amesema Upendo.
Diwani wa Kata ya Kichangani Mwanevyale Waziri ameishukuru ofisi ya Mkurugenzi kwa kufanikisha kuja kwa mradi huo kwani wana muda mrefu wananchi wa eneo hilo hawajapta majisafi na salama.
Mradi huo wa maji wa Mtaa wa Kichangani utakapomalizika kutajengwa vizima saba vya kuchotea maji kwa ajili ya kuwarahishia wananchi wa maeneo hayo.
DAWASA wanaendelea kuadhimisha wiki ya maji iliyoanza Machi 16 na itamalizika Machi 22 ikiwa na kauli mbiu ya Hakuna atakayeachwa.
Katibu Tawala DAS Ilala Sheila Edward akiwa sambamba na Diwani wa Mtaa Kichangani Mwanevyale Waziri wakiweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Ilala Upendo Lugongo akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko akizungumza na wananchi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam
Hivyo makala DAS ILALA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TANKI LA MAJI MAJOHE
yaani makala yote DAS ILALA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TANKI LA MAJI MAJOHE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DAS ILALA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TANKI LA MAJI MAJOHE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/das-ilala-aweka-jiwe-la-msingi-ujenzi_18.html
0 Response to "DAS ILALA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TANKI LA MAJI MAJOHE"
Post a Comment