Loading...
title : Dereva apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuendesha gari kizembe
link : Dereva apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuendesha gari kizembe
Dereva apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuendesha gari kizembe
DEREVA, Geofrey Elifuraha mkazi wa jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kuendesha gari kizembe.
Katika kesi hiyo namba 257/2019 mshtakiwa huyo amesomewa Shtaka lake hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Hanifa Mwingira.
Imedaiwa Kuwa, February 5 mwaka huko Kinondoni Hananasifu Mtaa wa Mkulima, uliopo Katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa Elifuraha alitenda kosa hilo.
Imedaiwa, siku ya tukio, mshtakiwa akiwa dereva anayeendesha gari namba T. 859CYT aina ya Toyota Noah, aliendesha gari hilo kwa uzembe na kushindwa kulimudu, hatimae akatoka nje ya barabara kisha kugonga mti na kusababisha uharibifu wa gari hilo.
Hata hivyo mshtakiwa huyo amekiri kutenda kosa hilo na amehukumiwa kulipa faini ya Sh. 30,000 ama kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani.
Aidha Mahakama imechukua leseni ya dereva huyo kwa kipindi cha mwezi mmoja. Hata hivyo dereva Elifuraha alifanikiwa kulipa faini hiyo na kufanikiwa kukwepa kifungo hicho.
Hivyo makala Dereva apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuendesha gari kizembe
yaani makala yote Dereva apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuendesha gari kizembe Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dereva apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuendesha gari kizembe mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/dereva-apandishwa-kizimbani-kwa-tuhuma.html
0 Response to "Dereva apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuendesha gari kizembe"
Post a Comment