Loading...
title : DK. MABODI : KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE NA WAWAKILISHI KUTOPITA MAJIMBONI MWAO HAKIKUBALIKI
link : DK. MABODI : KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE NA WAWAKILISHI KUTOPITA MAJIMBONI MWAO HAKIKUBALIKI
DK. MABODI : KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE NA WAWAKILISHI KUTOPITA MAJIMBONI MWAO HAKIKUBALIKI
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Juma Abdullah Saadala { Mabodi } ameonya kwamba kitendo cha baadhi ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wenye kushindwa kupita Majimboni ni kitendo cha kidhalimu kisichokubalika na wapiga kura wao pamoja na Chama cha Mapinduzi.
Dk. Mabodi Ametoa onyo hilo wakati akiufungua Mkutano Mkuu wa CCM wa Jimbo la Mahonda ulioelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo hilo katika kipindi cha Mwaka 2015 /2019 uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM Mkoa uliopo Mahonda.
Dk. Abdullah Mabodi amesema kwamba tabia hiyo ya utoro Majimboni kwa baadhi ya Wabunge na Wawakilishi ambayo kwa kiasi kikubwa hubebwa na mizozano inayosababishwa na Makundi ya Wabunge na Wawakilishi hao haitavumiliwa tena na Chama chenyewe.
Akiwasilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo la Mahonda kuanzia Mwaka 2016/2019 Mwakilishi wa Jimbo hilo Balozi Seif Ali Iddi amesema amekuwa Mtu mwenye furaha kutokana na ushirikiano anaoendelea kuupata katika kuwatumikia Wananchi kwa kasi kubwa.
Balozi Seif amesema Jumla ya Shilingi Milioni Mia 433,237,700/- zimetumika katika kuendeleza Miradi mbali mbali katika kipindi cha Miaka Mitatu ambayo imeleta faraja kwa Wananchi walio wengi ndani ya Jimbo hilo hasa ile Miradi ya Huduma za Maji, Elimu, Afya pamoja na Bara bara.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mahonda Mheshimiwa Bahati Abeid Nassir akiwasilisha Utekelezaji wa Ilani kwa Mwaka 2016 /2019 amesema tatizo la huduma za Maji safi na salama lilikuwa sugu, lakini kutokana na jitihada kubwa zilizochukuliwa na Uongozi kwa kushirikiana na Wananchi changamoto hiyo imepunguwa kwa asilimia kubwa.
Mhe. Bahati amesema ahadi alizozitoa wakati wa Kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 anatarajia kuzitekeleza kwa nguvu zake zote ndani ya kipindi cha Miaka Mitano huku akiamini kwamba wasaidizi wake wataendelea kumpa ushirikiano.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Machi 03, 2019
Hivyo makala DK. MABODI : KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE NA WAWAKILISHI KUTOPITA MAJIMBONI MWAO HAKIKUBALIKI
yaani makala yote DK. MABODI : KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE NA WAWAKILISHI KUTOPITA MAJIMBONI MWAO HAKIKUBALIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DK. MABODI : KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE NA WAWAKILISHI KUTOPITA MAJIMBONI MWAO HAKIKUBALIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/dk-mabodi-kitendo-cha-baadhi-ya-wabunge.html
0 Response to "DK. MABODI : KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE NA WAWAKILISHI KUTOPITA MAJIMBONI MWAO HAKIKUBALIKI"
Post a Comment