Loading...
title : DKT. KALEMANI ATOA AGIZO KWA TANESCO NDANI YA SIKU 5 LIWE LIMETEKELEZWA
link : DKT. KALEMANI ATOA AGIZO KWA TANESCO NDANI YA SIKU 5 LIWE LIMETEKELEZWA
DKT. KALEMANI ATOA AGIZO KWA TANESCO NDANI YA SIKU 5 LIWE LIMETEKELEZWA
Waziri wa Nishati Dkt. MEDARD KALEMANI akitoa maelekezo kwa Tanesco mara baada ya kutembelea Substation ya Njiro jana. Picha na Vero Ignatus
Mkuu wa substation ya Njiro Heriel Mbuya akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani alipomtembelea jana, kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro. Picha na Vero Ignatus.
Meneja wa kituo cha gredi ya taifa kilichopo njiro Heriel Mbuya akiwa katika chumba maalumu cha kuongozea mitambo akitoa ufafanuzi kwa waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani pamoja. Na viongozi wengine waliotembelea katika kituo hicho. Picha na Vero Ignatus
Na. Vero Ignatus, Arusha
WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kaleman ametoa siku tano kwa Shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Arusha kufunga Transfoma tatu eneo la Meru ili kuwawezesha wananchi wa eneo hilo kupata umeme mkubwa unaokidhi haja zao
Dkt. Kaleman ametoa agizo hilo jana wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo kikuu cha kupokea umeme wa Gridi ya Taifa, kilichopo Njiro Jijini Arusha Dk.Kaleman alisema kumekuwa na malalamiko mengi ya wananchi wa eneo la Meru Wilayani Arumeru Mkoani hapa,kuwa wanapata umeme mdogo.
"Sasa nimeamua kuja kuangalia kituo hiki kinachopokea umeme kama upo wa kutosha, sasa nimejiridhisha upo umeme mwingi tatizo ni wafanyakazi wa Tanesco kupeleka Transfoma za nyongeza tu, sasa nawapa siku tano mpeleke Transfoma mbili au tatu eneo la Meru mkawafungie wapate umeme wa uhakika,"alisisitiza
Dkt.Kaleman alisema umeme unapokuwa mdogo wananchi wanalalamika haswa wafanyabiashara ambao ndiyo waathirika wakubwa na ndiyo wengi Mkoani Arusha
Alisema baada ya kuongeza Taransfoma hizo hatategemea wafanyabiashara kulalamika tena na kupata visingizo vya kutolipa kodi, bali wautumie kuzalisha bidhaa nyingi katika viwanda vyao na bora, pamoja na kulipa kodi stahiki kwa serikali.
Pia aliiagiza Tanesco ndani ya mwezi huu kuagiza kifaa maalum cha kukata umeme inapotokea hitilafu, mbili au tatu (Saketi breka)na kuzihifadhi katika stoo ya kituo hicho kama akiba, ili inapoharibika mashine moja inachukuliwa ya akiba na kufunga mara moja.
"Mkiwa nazo za akiba mtaondokana na kuwaletea kero wananchi, ambao wanalalamika na ukosefu umeme pale inapotokea mashine imeharibika mnachukua siku nne kusubiri kije kifaa hicho baada ya kuagiza, sasa hakikisheni ndani ya mwezi huu mnanunua viwili au vitatu vya akiba ili mashine ikiharibika mara moja mnakiweka na wananchi wanaendelea kupata umeme,"alisema
Kwa upande mwingine aliagiza shirika hilo kuweka utaratibu wa kuwapa posho, walinzi wanaolinda miundombinu ya Shirika katika kituo hicho usiku na mchana bila kupumzika,ili kuwapa moyo zaidi wa kufanya kazi hiyo bila kukata tamaa.
Hivyo makala DKT. KALEMANI ATOA AGIZO KWA TANESCO NDANI YA SIKU 5 LIWE LIMETEKELEZWA
yaani makala yote DKT. KALEMANI ATOA AGIZO KWA TANESCO NDANI YA SIKU 5 LIWE LIMETEKELEZWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT. KALEMANI ATOA AGIZO KWA TANESCO NDANI YA SIKU 5 LIWE LIMETEKELEZWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/dkt-kalemani-atoa-agizo-kwa-tanesco.html
0 Response to "DKT. KALEMANI ATOA AGIZO KWA TANESCO NDANI YA SIKU 5 LIWE LIMETEKELEZWA"
Post a Comment