Loading...

FARU 12 KUINGIZWA NCHINI

Loading...
FARU 12 KUINGIZWA NCHINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa FARU 12 KUINGIZWA NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : FARU 12 KUINGIZWA NCHINI
link : FARU 12 KUINGIZWA NCHINI

soma pia


FARU 12 KUINGIZWA NCHINI

Katibu Mkuu wizara ya maliasili na utalii Prof.Adolf Mkenda amesema kuwa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund inatarajia kuingiza faru 10 nchini kwa ajili kuongeza idadi ya wanyama hao hapa nchini.

Kuagizwa kwa Faru hao kutaongeza idadi yao kutoka 2 walioagizwa na taasisi hiyo hapo awali hadi kufikia 12.

Akizungumza katika kikao kilichowahusisha wadau hao wa uhifadhi kilichofanyika katika chuo cha Uhifadhi wa Wanyamapori cha Pasiansi jijiji mwanza, Prof. Mkenda amewashukuru wadau hao kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha shughuli za uhifadhi nchini.

Amesema Serikali itaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina yake na wadau wote wapenda maendeleo kwa lengo la kulinda na kukuza shughuli za uhifadhi wa wanyamapori nchini.

Prof. Mkenda amesema kuwa kuletwa kwa faru hao kutaongeza idadi ya wanyama hao hapa nchini na kuongeza kuwa taasisi ya Grumeti imesaidia kuwaleta watu maarufu kutoka katika mataifa mbalimbali kuja kutembelea hifadhi za Taifa na hivyo kuchangia kutangaza utalii na kuongeza pato la Taifa.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa idara ya wanyamapori Tanzania Canisius Karamaga akizungumzia kuhusu ujio wa Faru hao amesema kuwa jitihada zinazofanywa na taasisi hiyo zinalenga kuwaongeza Faru hao hapa nchini.

Ameongeza kuwa Faru hao wataingizwa nchini kwa lengo la kuboresha kizazi cha wanyama hao waliokuwa hatarini kutoweka ikiwa ni moja ya juhudi za kuwafanya waongezeke kwa kuzaliana na wale waliopo nchini.

Amesema kikao hicho kati ya wizara na wadau hao ni muhimu sana kwa kuwa kimejadili na kuangalia kwa utalaam Zaidi namna Faru hao watakavyoingizwa nchini, kutunzwa na kulindwa kwa kuwa wanyama hao ni adimu na muhimu kwa utalii.

Amewataka watanzania kuwa mstari wa mbele kulinda rasilimali za nchi ili ziwe na faida kwa vizazi vijavyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda akisalimiana na watumishi wa Wizara hiyo kutoka katika taasisi za Uhifadhi wa Wanyamapori na wadau kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund inayotarajia kuingiza faru 10 kwa ajili kuongeza idadi ya wanyama hao hapa nchini.
Wadau wa Uhifadhi kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund wakifuatilia kikao cha pamoja kilichowahusisha viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na watumishi wa Wizara hiyo kutoka katika taasisi za Uhifadhi wa Wanyamapori, kikao hicho kimefanyika katika Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori, Pasiansi jijini Mwanza.
Baaadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka katika taasisi za Uhifadhi wa Wanyamapori wakiwa katika kikao cha pamoja na Wadau wa Uhifadhi kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund kilichofanyika katika Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori, Pasiansi jijini Mwanza.PICHA/ Maliasili na Utalii-Mwanza.
 


Hivyo makala FARU 12 KUINGIZWA NCHINI

yaani makala yote FARU 12 KUINGIZWA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala FARU 12 KUINGIZWA NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/faru-12-kuingizwa-nchini.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "FARU 12 KUINGIZWA NCHINI"

Post a Comment

Loading...