Loading...
title : Fursa kwa Makampuni ya Tanzania kupata soko China
link : Fursa kwa Makampuni ya Tanzania kupata soko China
Fursa kwa Makampuni ya Tanzania kupata soko China
Makampuni ya Tanzania yanayohitaji kuuza bidhaa katika soko la China yamekaribishwa kutumia mtandao ( E-commerce platform)- mall.ca-b2b.com/index ulioanzishwa mahususi kwa ajili ya kuyakutanisha makampuni yanayonunua na kuuza bidhaa mbalimbali katika masoko ya China na Afrika
Fursa hiyo imeelelezwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya China-Africa E-Commerce ndugu Zhigang Hou alipokutana na Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki leo jijini Chengdu katika jimbo la Sichuan
Mtandao huo ulioanzishwa mwaka jana una makampuni 5000 yaliyosajiliwa kwa madhumuni ya kutafuta bidhaa mbalimbali zinazopatikana barani Afrika. Inatarajiwa kwamba ifikapo mwaka 2021 mtandao huo utaratibu biashara yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 200.
Balozi Kairuki ameyataka makampuni ya Tanzania yenye bidhaa zenye viwango na ubora unaotakiwa na soko la kimataifa wajisajili katika mtandao huo ili waweze kukutana na makampuni yanayohitaji kununua bidhaa zao. Aidha, wafanyabiashara wanaotaka kununua bidhaa kutoka China pamoja na nchi nyingine za Afrika nao wanaweza kujisajili katika mtandoa huo ili waweze kukutana na wauzaji mbalimbali.
Makampuni yenye nia ya kupata taarifa za kujiunga na mtandao huo yanaweza kuwasiliana na mratibu: zhounana@ca-b2b.com
Hivyo makala Fursa kwa Makampuni ya Tanzania kupata soko China
yaani makala yote Fursa kwa Makampuni ya Tanzania kupata soko China Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Fursa kwa Makampuni ya Tanzania kupata soko China mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/fursa-kwa-makampuni-ya-tanzania-kupata.html
0 Response to "Fursa kwa Makampuni ya Tanzania kupata soko China"
Post a Comment