Loading...
title : Halmashauri ya Kilolo yakopesha wanawake navijana Tsh milioni 110
link : Halmashauri ya Kilolo yakopesha wanawake navijana Tsh milioni 110
Halmashauri ya Kilolo yakopesha wanawake navijana Tsh milioni 110
NA FRANCIS GODWIN,IRINGA
KATIKA utekelezaji wa agizo la serikali la kila Halmashauri nchini kutenga kiasi cha fedha asilimia 10 ya makusanyo yake ya ndani kwa ajili ya kuyawezesha makundi ya vijana ,walemavu na wanawake ,Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imetumia sherehe za siku ya wanawake duniani kwa kutoa mikopo kiasi cha shilingi milioni 110 kwa vikundi mbali mbali vikiwemo vikundi vya wanawake katika wilaya hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo Aloyce Kwezi mwakilishi wake katika sherehe hizo juzi Dr John Mwingira alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wavikundi vya wanawake wajasiliamali ndani ya wilaya ya Kilolo Halmashauri iliona ni vizuri kuweza kutumia siku hiyo ya wanawake duniani inayoadhimishwa Machi 8 kote duniani kwa ajili ya kuwawezesha wanawake hao kiuchumi.
Kuwa mikopo hiyo ambayo imetolewa kwa wanawake ni mikopo isiyo na riba na wakopaji watatakiwa kurejesha mikopo hiyo kwa muda uliopangwa bila ya kutozwa riba yoyote na kuwa pindi mikopo hiyo inaporejeshwa kwawakati vikundi vingine vya wanawake huendelea kukopeshwa zaidi .
" Halmashauri kupitia makusanyo ya mapato ya ndani imeendelea kutekeleza agizpo la serikali lililotolewa na Rais Dkt John Magufuli kwa Halmashauri zote nchini kupitia makusanyo yake ya ndani kutenga asilimia 10 kwa ajili ya kuwakopesha vikundi vya wanawake ,walemavu na vijana na halmashauri yetu imekuwa ikitekeleza kwavitendo na kwa wakati agizo hilo " alisema
Kuwakiasi hicho cha shilingi milioni 110 kimetumika kukopesha wanawake ,vijana na walemavu ambao kwa umoja wao walikabidhiwa fedha hizo kupitia sherehe hizo za siku ya wanawake duniani na kuwa azma ya Halmashauri kuendelea kuwasaidia mikopo vijana ,wanawake na walemavu ambao wamejiunga katika vikundi .
Alisema kuwa kupitia sherehe hizo vikundi vya wanawake 59 kutoka kata mbali mbali za wilaya ya Kilolo walikopeshwa kiasi cha shilingi milioni 66 wakati vikundi vya vijana vilivyopewa mkopo ni vikundi 24 ambavyo vilikopeshwa shilingi milioni 43 na kikundi kimoja cha walemavu kilichokopeshwa kiasi cha shilingi milioni 1.
Akikabidhi mfano wa hundi ya mikopo kwa vikundi hivyo mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Vallence Kihwaga alisema kuwa fedha hizo za mikopo walizokopeshwa na sehemu tu ya bajeti ya Halmashauri iliyotengwa kwa mwaka 2019 na kuwa kwa sasa wameanza kutekeleza matumizi ya bajreti hiyo kwa kuanza kutoa mikopo kwamakundi mbali mbali na wataendelea kutoa mikopo na kuwataka walengwa kuendelea kujiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiliamali .
" Tutaendelea kutoa mikopo hii mara kwa mara kama ambavyo bajeti yetu ilivyopangwa kwa mwaka huu na tunauhakika kuwa baada ya leo kutoa mikopo hii muda si mrefu tutatoa mikopo tena kwa makundi ya wanawake ,vijana na walemavu hivyo endeleeni kuunda vikundi vyenye tija vya ujasiliamali nacha kujivunia ni tayari Rais wetu mpendwa Dkt John Magufuli kwa kuwajali wajasilimali amekwisha toa vitambulisho kwa kila halmashauri kwa ajili yenu wajasiliamali kazikwenu kuchangamkia vitambulisho hivyo ili msinyanyasike mnapofanya shughuli zenu" alisema Kihwaga.
Aidha alisema wakopaji ambao watachelewesha kurejesha mikopo ama kushindwa kurejesha kabisa watakuwa wamejiondoa katika orodha ya watakaoendelea kukopeshwa mikopo hiyo na wale watakaoonyesha uaminifu wataendelea kunufaika na mikopo hiyo inayotengwa na Halmashauri ikiwa ni asilimia 4 vijana na asilimia 2 walemavu huku wanawake wakipata nao asilimia 4 katika asilimia 10 ya mikopo itokanayo ya makusanyo ya ndani ya Halmashauri .
Kihwaga alisema kuwa sifa kuu ya vikundi hivyo kukopeshwa ni kuwa kuwa na akaunti bank ambayo ni hai na sio akaunti iliyosinzia ambayo haionyeshi kama inatumika kuweka na kuchukua fedha .
Kwa upande wake wake wanawake wanufaika na mikopo hiyo Amina Sanga akizungumzia mikopo hiyo alisema kuwa imekuwa ni mkombozi mkubwa kwao kwani itawawezesha kuongeza uzalishaji katika kikundi na kuwa pale wanawake wanapokuwa na kipato kizuri ndani ya familia hata ndoa zao zimekuwa zisimama pasipo kuyumba kwani mama anakuwa na sauti kama baba ndani ya nyumba.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani IringaVallence Kihwaga (mwenye koti jeusi kushoto) na mwakilishi wamkurugenzi wa Halmashauriya Kilolo Dr John Mwingira ( wapili kulia) wakiwakabidhi mfano wahundi ya shilingi milioni 110 wanawake wa vikundi 59 vya wajasiliamali wilaya ya Kilolo kwa niaba ya vikundi vya walamavu na vijana juzi wakati wa sherehe za wanawake wilaya ya Kilolo (picha na Francis Godwin).
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Vallence Kihwaga (kushoto) akimkabidhi mmoja kati ya wazee wanaotoka katika familia masikini ndani ya mji wa Ilula kwa niaba ya wazee wengine ,msaada wa sabuni na vitu mbali mbalivilivyotolewa na wanawake wa wilaya ya Kilolo kwa wazee hao kwa ajili ya kusherekea siku ya wanmawake duniani juzi Machi 8 mwaka huu (Picha na Francis Godwin).
Hivyo makala Halmashauri ya Kilolo yakopesha wanawake navijana Tsh milioni 110
yaani makala yote Halmashauri ya Kilolo yakopesha wanawake navijana Tsh milioni 110 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Halmashauri ya Kilolo yakopesha wanawake navijana Tsh milioni 110 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/halmashauri-ya-kilolo-yakopesha.html
0 Response to "Halmashauri ya Kilolo yakopesha wanawake navijana Tsh milioni 110"
Post a Comment