Loading...
title : HATMA YA DHAMANA YA MBOWE NA MATIKO KUJULIKANA KESHO
link : HATMA YA DHAMANA YA MBOWE NA MATIKO KUJULIKANA KESHO
HATMA YA DHAMANA YA MBOWE NA MATIKO KUJULIKANA KESHO
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam kesho, Machi 7, 2019 inatarajia kutoa hatma ya ama kuendelea kusota rumande au kurudi uraiani kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni takribani miezi minne tangu viongozi hao wafutiwe dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 23, mwaka jana baada ya kukiuka masharti yaliyowekwa na mahakama hiyo
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Jaji Sam Rumanyika, baada ya kusiliza hoja za pande zote, ambapo wakata rufaa, waliwakilishwa na Wakili Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya, huku upande wa ukiwa na jopo la mawakili watano wa Serikali, wakiongozwa na wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi, Paul Kadushi Salim Msemo, Wankyo Simon( mawakili wa Serikali) na Wakili Serikali Mwandamizi, Jakline Nyantori.
Jaji Rumanyika amesema amesikiliza hoja zao na uamuzi atautoa kesho saa saba mchana.
Wakiwasilisha hoja zao, wakili Kibatala amedai, walikuwa na sababu nne za kukata rufaa, lakini baada ya Mahakama hiyo kuziondoa mbili zimebaki mbili, kwa hiyo watajikita katika hoja hizo na kudai kuwa Mahakama ya Kisutu ilifanya makosa kuwafutia dhamana Mbowe na Matiko wakati siku hiyo ambayo ilikuwa ni Novemba 23, 2018 washtakiwa wote walikuwepo mahakamani.
Amedai washtakiwa hao walifika mahakamani hapo bila hata ya kukamatwa licha ya kwamba kulikuwa na hati ya kukamatwa, waliingia mahakamani na kujieleza kuwa siku ambazo hawakuwepo walikuwa nje ya nchi na kwamba kama wateja wake hawafiki mahakamani basi siku hiyo wadhamini wao wanafika mahakamani hapo na kutoa sababu, lakini cha kushangaza licha ya wadhamini hao kufika na kujileza bado dhamana ilifutwa.
Ameongeza kudai kuwa, mahakama ilikosea kuwafutia dhamana washtakiwa kwani hakukuwa na mantiki yoyote ya kufanya hivyo na hivyo wameomba Mahakama ilidhie ione hoja zao zina mashiko kisheria.
Pia Kibatala aliendelea kueleza kuwa, wakati Hakimu anatoa uamuzi huo wa kuwafutia dhamana hakukuwa na 'material' yoyote ambayo yaliiegemiza Mahakama kutoa uamuzi huo.
Katika suala la kiapo kilichowaailishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Dkt. Zainabu Mango katika Mahakama ya Kisutu, Kibatala anaeleza kuwa haikuwa sahihi kwa wakili huyo kuapa kiapo hicho kwa niaba ya Jamhuri wakati na yeye ni mmoja wanaoendesha kesi hiyo, ambapo sheria hairuhusu kufanya hivyo.
Kwa upande wake, Mtobesya alidai ni maoni yao kwa Mahakama Kuu, ikatengua uamuzi wa Mahakama ya Kisutu ili wateja wao warudi kufarahia haki yao ya msingi ya kuwa nje kwa dhamana, kwa sababu uamuzi wa kuwafutia dhamana haukuwa sahihi.
Wakijibu hoja hizo, Wakili Nyantori amedai kuwa hakuna hoja za msingi katika misingi ya kisheria ambazo zimewasilishwa na wakati rufaa ( Mbowe na Matiko), zitasababisha rufaa yao kukubaliwa, sababu ya kwamba washtakiwa walikuwepo siku hiyo ya Novemba 23,2018 ndiyo wasifutiwe dhamana, kutokana na kwamba walipewa haki yao ya msingi ya kujieleza na mahakama ikatoa uamuzi huo.
Nyantori alidai kuwa, Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo, baada ya kuwasikiliza wadhamini na washtakiwa wenyewe, ambapo Mbowe aliwasilisha na hati yake ya kusafiria ambayo iliyoonesha jinsi alivyosafiri sehemu mbalimbali, kwa hiyo haikukosea katika uamuzi wake.
Aliendelea kudai kuwa mara kadhaa Mbowe na Matiko wamekuwa wakionywa na mahakama kwa kutofika mahakamani bila kutoa sababu za msingi.
Novemba 23, 2018 (Mbowe na Matiko) walifutiwa dhamana Mahakama ya Kisutu na siku iliyofuata wakiongozwa na Kibatala walikata rufaa kupinga maamuzi hayo.
Novemba 27, 2018, Jaji Rumanyika aliona kuwa rufaa hiyo imepelekwa chini ya hati ya dharura hivyo aliagiza mwenendo wa shauri upelekwe mahakamani hapo pamoja na wahusika wapande zote wafike.
Hata hivyo, Novemba 28, upande wa mashitaka na wa utetezi walifika mahakamani hapo na mapingamizi ya pande zote yalisikilizwa ikiwemo sababu nne za Mbowe na Matiko za kupinga uamuzi huo kwamba mahakama haijawapa nafasi wadhamini ya kujieleza kwa mujibu wa sheria.
Pia walidai mahakama imekosea kuwafutia dhamana kwa sababu Novemba 12, 2018 Mbowe na Matiko walifika mahakamani bila kukamatwa na kuwa chini ya ulinzi.
Alidai masharti ya dhamana waliyopewa washtakiwa ni kinyume na sheria.
Hata hivyo, upande wa mashitaka uliomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa hiyo kwa sababu tatu ikiwemo warufani kushindwa kukata rufaa kupinga dhamana iliyotolewa na mahakama ya Kisutu na kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza rufaa kwani taarifa ya kusudio la kukata rufaa imekosekana.
Baada ya Jaji Rumanyika kusikiliza mapingamizi hayo alikubaliana na hoja za upande wa serikali za kupewa mwenendo wa shauri hilo wa kesi ya msingi iliyopo Mahakama ya Kisutu uliochapishwa ambao unasomeka vizuri na sio kama ule waliopewa awali.
Pia alikubaliana na hoja ya pingamizi ya upande wa serikali kuwa sababu mbili za rufaa za kupinga masharti ya dhamana, zinakiuka matakwa ya sheria kwa kuwa zimekatiwa rufaa bila kutoa kwanza taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga masharti hayo ya dhamana yaliyotolewa kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka jana.
Hata hivyo, baada ya mahakama kupanga kuanza kusikiliza rufaa hiyo, upande wa mashitaka alidai kuwa wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga maamuzi ya yaliyotolewa na kuiomba mahakama hiyo kuacha kuendelea kusikiliza rufaa hiyo kwa sababu haina mamlaka.
Hivyo makala HATMA YA DHAMANA YA MBOWE NA MATIKO KUJULIKANA KESHO
yaani makala yote HATMA YA DHAMANA YA MBOWE NA MATIKO KUJULIKANA KESHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HATMA YA DHAMANA YA MBOWE NA MATIKO KUJULIKANA KESHO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/hatma-ya-dhamana-ya-mbowe-na-matiko.html
0 Response to "HATMA YA DHAMANA YA MBOWE NA MATIKO KUJULIKANA KESHO"
Post a Comment