Loading...

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MTAMBO WA KUTEKETEZA TAKA

Loading...
HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MTAMBO WA KUTEKETEZA TAKA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MTAMBO WA KUTEKETEZA TAKA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MTAMBO WA KUTEKETEZA TAKA
link : HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MTAMBO WA KUTEKETEZA TAKA

soma pia


HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MTAMBO WA KUTEKETEZA TAKA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya Dkt. Paul Lawala mara baada ya Mhe. Sima kutembelea Hospitali hiyo kukagua namna taka ngumu na hata hatarishi zinavyo teketezwa. 
Shimo ambalo linatumika kwa sasa kuteketeza taka za Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, mara baada ya mtambo maalumu wa kutetekeza taka hizo kuwa katika hatua za ukarabati. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Paul Lawala kuja na Mkakati wa haraka wa kupata mtambo mpya (Incinerator) ya kuteketeza taka hatarishi. 
Mtambo wa kuteketeza taka wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kama unavyoonekana ukiwa katika hali chakavu na ukifanyiwa ukarabati. Katika ziara ya kikazi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima ameagiza kukarabatiwa kwa mtambo huo mapema iwezekanavyo kama hatua za haraka na kutafuta kiteketezi taka ambacho kitakidhi mahitaji ya Hospitali ya Rufaa.



Frank Mvungi – MAELEZO, Dodoma

Urasimishaji ardhi Wilayani Chamwino mkoani Dodoma umetajwa kuwa kichocheo cha kukuza uzalishaji katika sekta ya kilimo na ufugaji baada ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wilayani humo.


Akizungumza katika mahojiano maalum Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Bw. Antony Temu amesema kuwa wakulima wamejengewa uwezo kupitia mafunzo yaliyoratibiwa na mpango huo baada ya urasimishaji wa mashamba ya wakulima hao.


“ Wakulima hawa wataweza kuzalisha kwa tija na kuongeza uzalishaji kutoka magunia 4 kwa sasa hadi kufikia magunia 10 kwa ekari moja na pia wataweza kutekeleza dhana ya ufugaji bora wa kuku na mifugo mingine ili kuendana na fursa zilizopo kutokana na Serikali kuhamia Dodoma,”alisisitiza Temu.

Akifafanua, Bw. Temu amesema kuwa wakulima zaidi ya 100 wamenufaika na mafunzo ya kuwajengea uwezo ambapo wakulima kutoka kijiji cha Membe wameonesha mwitikio mkubwa katika mafunzo hayo hali inayoonesha kuwa mafunzo yataleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa wakulima wilayani humo.

Aliongeza kuwa wakulima hao sasa wametambua mbegu bora za mazao wanayozalisha ikiwemo alizeti hali itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa kijiji cha Membe akiwemo Bi. Pelestatili Msilili amesema kuwa urasimishaji ardhi utawasidia kutatua changamoto zilizopo katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo na hivyo kujikwamua kiuchumi.

“Tutaweza kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha hivyo tunawashukuru MKURABITA kwa kuja na mpango huu wa kutujengea uwezo ambao ni ukombozi wa kweli,”alisisitiza Bi Msilili.Naye Bi Suzana Kuanikwa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Membe amebainisha kuwa anaishukuru Serikali kwa namna inavyowajali wananchi wake kupia uwezesjhaji huu unaotuwezesha kuwa na matumizi bora ya ardhi katika kijiji chetu.

Aidha, Bi Kuanikwa amebainisha kuwa kwa sasa wakulima wa kijiji hicho watapata mwamko mpya katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo na mifugo.

MKURABITA imekuwa ikiendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima baada ya kurasimisha mashamba yao katika halmashauri mbalimbali hapa nchini, kwa ujumla halmashauri 24 zimeshafikiwa na Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania.


Hivyo makala HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MTAMBO WA KUTEKETEZA TAKA

yaani makala yote HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MTAMBO WA KUTEKETEZA TAKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MTAMBO WA KUTEKETEZA TAKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/hospitali-ya-rufaa-ya-kanda-ya-mbeya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MTAMBO WA KUTEKETEZA TAKA"

Post a Comment

Loading...