Loading...

JAFO AELEKEZA HOSPITALI ZA WILAYA MPYA ZINAZOJENGWA ZIKAMILIKE IFIKAPO JUNE 30

Loading...
JAFO AELEKEZA HOSPITALI ZA WILAYA MPYA ZINAZOJENGWA ZIKAMILIKE IFIKAPO JUNE 30 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JAFO AELEKEZA HOSPITALI ZA WILAYA MPYA ZINAZOJENGWA ZIKAMILIKE IFIKAPO JUNE 30, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JAFO AELEKEZA HOSPITALI ZA WILAYA MPYA ZINAZOJENGWA ZIKAMILIKE IFIKAPO JUNE 30
link : JAFO AELEKEZA HOSPITALI ZA WILAYA MPYA ZINAZOJENGWA ZIKAMILIKE IFIKAPO JUNE 30

soma pia


JAFO AELEKEZA HOSPITALI ZA WILAYA MPYA ZINAZOJENGWA ZIKAMILIKE IFIKAPO JUNE 30

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
WAZIRI wa TAMISEMI, Selemani Jafo ameziagiza halmashauri zote zilizopatiwa fedha za kujenga hospitali ya wilaya mpya, kuhakikisha wanasimamia majengo hayo yanakamilika ifikapo June 30 mwaka huu. 

Aidha ameelekeza watalaamu wa halmashauri hizo wasimamie ubora wa majengo yanayoboreshwa na kupanua vituo vya afya ili yaweze kudumu kwa kipindi kirefu kijacho .
 Pamoja na hayo Jafo ameridhishwa na utekelezaji wa agizo alilolitoa kwa halmashauri ya Kibaha Vijijini, mkoani Pwani miezi michache iliyopita kuhusu kukarabati chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha afya cha Mlandizi. 

Akitembelea ujenzi wa upanuzi wa kituo cha afya Mlandizi na hospitali ya wilaya inayojengwa Kibaha Vijijini, Jafo alitaka hospital hizo zikamilike kwa muda huo na kwa kiwango chenye ubora kulingana na thamani iliyotolewa. 

Alisema serikali imetoa kiasi cha sh. milioni 400-500 kwa vituo vya afya 97 nchini ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi. 

Jafo pia aliyaasa mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo TACAIDS kukabidhi fedha za miradi wanayotaka kuyajenga ikiwemo maabara katika kituo cha afya Mlandizi kwa halmashauri ya Kibaha Vijijini badala ya kusimamia wenyewe ili kuondoa mkanganyiko. 

"Kwanini mkandarasi wamlete wao, nyie wenyewe mmeweza kujenga kwa umakini na kutumia fedha vizuri kuboresha kituo hiki cha afya, kwanini wao wasitoe hizo milioni 600 kwenu mkasimamia miradi hiyo "

"Msije kuingizwa mkenge simamie na wanapaswa kupitisha fedha hizo kwenu "alifafanua Jafo. 
 Kuhusu chumba cha kuhifadhia maiti amepongeza halmashauri hiyo kwa kutekeleza agizo lake kwa asilimia 100. Nae mbunge wa jimbo hilo, Hamoud Jumaa alimuomba waziri huyo kuwaongezea fedha kwa ajili ya kuboresha zahanati ya Dutumi na Kwala. 

Jafo alisema serikali itaangalia uwezekano wa jambo hilo ukizingatia Kwala kunajengwa bandari kavu hivyo ni bora huduma za kijamii zikaangaliwa. 


Hivyo makala JAFO AELEKEZA HOSPITALI ZA WILAYA MPYA ZINAZOJENGWA ZIKAMILIKE IFIKAPO JUNE 30

yaani makala yote JAFO AELEKEZA HOSPITALI ZA WILAYA MPYA ZINAZOJENGWA ZIKAMILIKE IFIKAPO JUNE 30 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JAFO AELEKEZA HOSPITALI ZA WILAYA MPYA ZINAZOJENGWA ZIKAMILIKE IFIKAPO JUNE 30 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/jafo-aelekeza-hospitali-za-wilaya-mpya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JAFO AELEKEZA HOSPITALI ZA WILAYA MPYA ZINAZOJENGWA ZIKAMILIKE IFIKAPO JUNE 30"

Post a Comment

Loading...