Loading...
title : JEZI ZA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA HOUSTON ZAWASILI
link : JEZI ZA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA HOUSTON ZAWASILI
JEZI ZA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA HOUSTON ZAWASILI
Jezi za Yanga
Jezi za Simba
Mtanange unaosubiliwa kwa hamu Houston na vitongoji vyake, pambano la watani wa jadi Yanga na Simba litakalochezewa katika viwanja vya Cullen Park anuani ni 19008 Saums Rd, Houston, TX 77084. Kila mwaka jezi za timu hizo hudhaminiwa na DELINA GROUP kampuni ya Davis Mosha yenye makao makuu Sinza.
Mpambano huo ambao huchezwa mara mpja kila mwaka na timu ya Yanga ikiwa ikizidiwa ujanja na timu ya Simba, mara zote timu hizi zinapokutana mpambano unakua mkali sana na huwezi kutabili mshindi mpaka dakika ya 90. Mechi ya kwanza Columbus, Ohio Simba iliibuka mshindi kwa kuifunga Yanga 2-1 na mechi iliyochezwa DMV na kuchezeshwa na refarii Kazi kutoka Tanzania, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na katika mikwaju ya penati Simba ilipata penati 4 na Yanga ilipata penati 3 na hivyo kukubali kipigo kingine kutoka kwa Simba.
Mechi hizi za Yanga na Simba ni sehemu ya kusherehekea Old School Reunion ambayo mwaka huu inafanyika Houston, Texas ambayo safari hii itakua ya aina yake na si ya kukosa.
Old School Reunion ilianzishwa kwa lengo la kuwakutanisha vijana wa enzi zilee katika kukumbuka enzi zao, kwa michezo na burudani inayowakumbusha miaka hiyo walipokua vijana.
Tamasha hili la Old School Reunion lilianzia Columbus, Ohio mwaka 2017, na mwaka uliofuata lilifanyika DMV na sasa mwaka huu mwezi March tarehe 22 na 23 litafanyika Houston, Texas.
Mwitikio ni mkubwa wadau mbalimbali ndani na nje ya Marekani hujitokeza kuhudhuria onyesho hili la vijana wa zamani linalo waunganisha madj wakongwe na madj wenyeji wa jimbo linakofanyikia.
Old School Reunion hii ya mwaka huu, 2019 ni ya aina yake kwa jinsi ya mwamko ulivyokua mkubwa kutoka kila pembe, wadau wengi wameipania sana na hasa inavyokuja mechi ya Yanga na Simba huvutia wachezaji wengi husafiri kutoka kila jimbo ikiwemo Canada na Sweden. Inakua mechi ya kukamiana sana, hakuna timu inayotaka kupoteza mchezo.
Michezo mingine inayokuwepo ni mpira wa kikapu ambayo hukutanisha wachezaji wa zamani waliochezea timu za Pazi, Vijana Don Bosco na timu nyingine za mchezo huo nchini Tanzania.
Old School Reunion itaanzia Ijumaa March 22, 2019 kwa usiku utakaotawaliwa na nyimbo zinazotamba sasana usiku huo utaitwa KARIBU NIGHT na siku ya Jumamosi saa kumi kamili jioni utachezwa mpambano wa Simba na Yanga na baadae usiku ndio siku inayosubiliwa kwa hamu OLD SCHOOL REUNION usiku utakaowakutanisha vijana wa zamani kukumbuka enzi zao.
Yote haya yatafanyika kwenye paa moja CRYSTAL PALACE PARTY HALL anuani ni 12450 Bissonet # 220, Houston, TX 77099. KARIBU HOUSTON UANDIKE HISTORIA
Hivyo makala JEZI ZA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA HOUSTON ZAWASILI
yaani makala yote JEZI ZA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA HOUSTON ZAWASILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JEZI ZA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA HOUSTON ZAWASILI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/jezi-za-mtanange-wa-simba-na-yanga.html
0 Response to "JEZI ZA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA HOUSTON ZAWASILI"
Post a Comment