Loading...
title : KAMATI YA BAJETI YA BUNGE YATEMBELEA KIWANDA CHA TANELEC ARUSHA, WAPOKELEWA NA WAZIRI WA NISHATI DKT. KALEMANI
link : KAMATI YA BAJETI YA BUNGE YATEMBELEA KIWANDA CHA TANELEC ARUSHA, WAPOKELEWA NA WAZIRI WA NISHATI DKT. KALEMANI
KAMATI YA BAJETI YA BUNGE YATEMBELEA KIWANDA CHA TANELEC ARUSHA, WAPOKELEWA NA WAZIRI WA NISHATI DKT. KALEMANI
Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene wakimsikiliza Mkurugenzi mkuu wa TANELEC Zahir Saleh akiwaeleza kuhusiana na utendaji, uzalishaji katika kiwanda hicho
Mkurugenzi wa TANELEC akiendelea kuelezea utendaji wa kazi katika kiwanda hicho
Kutoka kulia ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Mwenyekiti wa kamati ya bajeti ya Bunge George Simbachawene, Mkurugenzi mkuu wa TANELEC Zahir Saleh wakibadilishana mawazo na baaadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Bunge
Mmoja wa wafanyakazi wa TANELEC akionyesha vikombe vya kupitishia nyaya na kupunguzia umeme mara unapopita
Mmoja wa wafanyakazi katika Kiwanda cha TANELEC akisuka Transfoma kama inavyoonekana katika picha.
Mkurugenzi mkuu wa TANELEC Zahir Saleh ufafanuzi mbele ya waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani pamoja na Kamati ya bajeti ya bunge kama wanavyoonekana pichani
Mwanamama huyu akiwa anapanga sumaku zinazokaa ndani ya transfoma kama anavyoonekana ambapo kwa siku huwa anapanga mbili ila inategemea size
Wafafanyakazi wakiwa katika hatia za awali wa kusuka transfoma kama wanavyoonekana katika picha
Taransfoma ikiwa katika hatua ya kukamilishwa kama inavyoonekana katika picha
Transfoma ikiwa imeshakamilika na ipo kwa ukaguzi wa mwisho kupitishwa ili iingie sokoni
Transfoma zikiwa zimekamilika zikiwa tayari kuingia sokoni kwa matumizi. Picha zote na Vero Ignatus.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kiwanda cha kutengeneza Transfoma cha TANELEC kilichopo Njiro Jijini Arusha
Na. Vero Ignatus, ARUSHA
Kamati ya kudumu ya bajeti Bunge imetembelea kiwanda cha kutengeneza Transfoma cha Tanelec ikiwa na lengo la kuona utendaji, uzalishaji, pamoja maendeleo ya kiwanda hicho
Ugeni huo umepokelewa na Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani,ambapo amesema lengo la serikali ni kuhakikisha inawezesha viwanda vya ndani ili viweze kupiga hatua na katika kufanikisha kufikia uchumi wa kati.
Dkt. Kaleman amesema kiwanda hicho kwa kushirikiana na serikali kimefanya jitihada za kukifufua na kufanikisha uongezaji wa uzalishaji unapanda toka mwaka 2016 walipokuwa wakizalisha Transfoma 7,000, mwaka 2017 Taransfoma 10,000 na sasa 14,000.
Ongezeko hilo la Transfoma ni kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza uchumi wa nchi kufikia wakati kupitia sekta viwanda ambavyo vingi vinatumia umeme.
Hata hivyo serikali imekipongeza kiwanda cha kuzalisha Transfoma cha Tanelec kilichopo Jijini hapa kwa kuongeza uzalishaji wa Transfoma kutoka 7,000 hadi 14,000 kwa kipindi cha mwaka jana.
Akitoa pongezi hizo leo mbele ya kamati ya Bunge ya Bajeti,Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani, alisema uzalishaji huo unawezesha uanzishwaji wa viwanda na kuchangia kukuza ajira.
Aidha alisema kuimarika kwa kiwanda hicho na msimamo wa Rais John Magufuli wa kutaka watanzania kujenga utamaduni wa kupenda vitu vinavyozalishwa nchini kumesaidia kuepuka gharama iliyokuwa ikitokana na uagizaji Taransfoma nje ya nchi.
"Kupitia kiwanda chetu gharama za usafirishaji,muda wa kutumia kusubiri kuletwa na bado zikija sio bora kama zetu tumeachana nazo,"alisema
Aidha alisema kufikia kwa hatua hiyo kumeleta maumivu makubwa kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao walikuwa wakinufaika na uagizaji Tarnsfoma hizo nje ya nchi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene aliahidi kumpa ushirikiano Waziri katika kulisimamia hilo ili kukipa nguvu zaidi kiwanda hicho na vingine nchini.
"Nikupongeze Waziri kwa kusimamia wazabuni katika sekta ya nishati kutumia bidhaa za ndani,natambua siasa za wafanyabiashara kuna wakati zilikupa wakati mgumu ukabaki peke yako endelea kusimamia uamuzi huu sisi tupo nyuma yako kukulinda,"alisema
Akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa mjumbe wa kamati ya Bunge kuhusiana na umeme kupanda na kushuka Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito Mwinuka amesema inaweza kuwa ni matatizo ya kiufundi katika mifumo ya umeme wala haihusiani na Transifoma
Amesema yapo maeneo mengi ambayo TANESCO wanahitaji AVR ili umeme uweze kwenda kwa wateja ukiwa mzuri
Kuhusu ombi la Mkurugenzi wa kiwanda cha Tanelec Zahir Saleh la kutaka Transfoma zinazoingia nchini kutozwa asilimia 40 atalisemea bungeni.
Mkurugenzi wa kiwanda cha Tanelec,Zahir Salehe ameomba bunge na serikali kutoza bidhaa za nje zinazoingizwa nchini hususanibTaransfoma ili kulinda bidhaa za ndani.
Amesema kwa upande wao wameweza kutoa gawio kwa serikali Sh. Milioni 500 kwa mwaka jana.
Hivyo makala KAMATI YA BAJETI YA BUNGE YATEMBELEA KIWANDA CHA TANELEC ARUSHA, WAPOKELEWA NA WAZIRI WA NISHATI DKT. KALEMANI
yaani makala yote KAMATI YA BAJETI YA BUNGE YATEMBELEA KIWANDA CHA TANELEC ARUSHA, WAPOKELEWA NA WAZIRI WA NISHATI DKT. KALEMANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMATI YA BAJETI YA BUNGE YATEMBELEA KIWANDA CHA TANELEC ARUSHA, WAPOKELEWA NA WAZIRI WA NISHATI DKT. KALEMANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/kamati-ya-bajeti-ya-bunge-yatembelea.html
0 Response to "KAMATI YA BAJETI YA BUNGE YATEMBELEA KIWANDA CHA TANELEC ARUSHA, WAPOKELEWA NA WAZIRI WA NISHATI DKT. KALEMANI"
Post a Comment