Loading...

KAMPUNI YA COCA-COLA YAPONGEZWA KWA UBUNIFU KUPITIA MICHEZO YA COPA COCA-COLA

Loading...
KAMPUNI YA COCA-COLA YAPONGEZWA KWA UBUNIFU KUPITIA MICHEZO YA COPA COCA-COLA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAMPUNI YA COCA-COLA YAPONGEZWA KWA UBUNIFU KUPITIA MICHEZO YA COPA COCA-COLA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAMPUNI YA COCA-COLA YAPONGEZWA KWA UBUNIFU KUPITIA MICHEZO YA COPA COCA-COLA
link : KAMPUNI YA COCA-COLA YAPONGEZWA KWA UBUNIFU KUPITIA MICHEZO YA COPA COCA-COLA

soma pia


KAMPUNI YA COCA-COLA YAPONGEZWA KWA UBUNIFU KUPITIA MICHEZO YA COPA COCA-COLA

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Mwita Waitara leo ameshiriki uzinduzi wa semina shirikishi ya maofisa michezo kutoka mikoa 26 nchini katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla Mhe. Mwita Waitara alipongeza uamuzi wa Coca Cola kutambulisha Kampeni ya ‘COPA Coca Cola Kusanya na Ushinde’, ambayo imenuia kutoa hamasa kwa vijana kuyatunza mazingira kwa kuwajibika kukusanya chupa za plastiki mashuleni katika kipindi ambacho michezo ya Copa Coca-Cola UMISSETA itakapokuwa inaendelea kuwa ni muelekeo sahihi.

“Ninafahamu kuwa kwa mwaka huu, lengo la COPA Coca-Cola (UMISSETA) ni kujenga uelewa juu ya umuhimu wa utunzaji mazingira kupitia ukusanyaji wa chupa za plastiki. Ninapenda kuwahakikishia kuwa, nipo tayari kuwaunga mkono ili kufanikisha hamasa hii ya kuhifadhi mazingira ya shule zetu hapa nchini,"alisema.

“Mwaka jana, niliwaombeni muendelee kufadhili mashindano ya UMISSETA na mchukue umiliki wa michezo hii. Ninafarijika kuona ili mmelifanyia kazi kwa wakati. Wakati akizindua michezo ya mwaka 2019 COPA Coca-Cola, Waziri amebainisha kimkoa yataanza Manyara Aprili 5, mwaka huu.

Mhe. Waitara pia alibainisha kuwa, Serikali inatambua mchango mkubwa wa Coca Cola katika kuendeleza vipaji vya vijana. Amesema, Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha katika kampuni hiyo ya vinywaji. Waitara alitoa wito kwa makampuni mengine na wadau wa michezo kuipa michezo shuleni kipaumbele kama Coca Cola inavyofanya kwa miaka mingi na dhamira ya Serikali ni kuinua michezo shuleni.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma na Mawasiliano wa Coca-Cola Kwanza, Haji Mzee amesema, michezo ni chaguo la vijana wengi na mizizi ya maendeleo ya soka nchini huanzia kwao. Mfumo huu wa Coca-Cola umejikita katika kutoa hamasa ya michezo kwa kuibua vipaji mbalimbali katika michezo.

Ameongeza kuwa, mashindano ya COPA huwa yanawawezesha vijana kuonyesha vipaji vyao katika umri mdogo, pia huwapa fursa ya kuviendeleza vipaji vyao. “Mwaka huu COPA Coca-Cola dhumuni lake ni Kukusanya na Ushinde, mradi uliobuniwa kuhakikisha plastiki zote zinakusanywa katika shule shiriki wakati wa michezo.Kupitia kampeni hii tumelenga wanafunzi wawe wawajibikaji katika jamii kwa kuyahifadhi vema mazingira,"alisema.

Aidha, ameishukuru Serikali na wadau mbalimbali wa michezo kwa kuunga mkono juhudi hizo za Coca Cola. Semina hiyo imehudhuriwa na maofisa michezo wa mikoa yote, walimu wa michezo wa shule za sekondari, Maafisa elimu wa mikoa, Shule za Sekondari na Msingi, Wizara ya habari, Tamaduni, Sanaa na michezo, Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI.
1056724
Meneja bidhaa wa Kampuni ya vinywaji Kampuni ya Coca-Cola Pamela Lugenge akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Mwita Waitara wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca-Cola kwa shule za Msingi na Sekondari kwa mwaka huu jijini Dodoma.
1056726
Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma na Mawasiliano-Coca Cola Kwanza akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara katika hafla ya uzinduzi rasmi wa semina elekezi ya mashinadano ya Copa Coca-Cola kwa shule za Msingi na Sekondari Tanzania 2019 jana Jijini Dodoma. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni.
1056733
Pamela Lugenge akitoa hotuba yake.
1056734
Mheshimiwa Waziri akihutubia wageni waalikwa.


Hivyo makala KAMPUNI YA COCA-COLA YAPONGEZWA KWA UBUNIFU KUPITIA MICHEZO YA COPA COCA-COLA

yaani makala yote KAMPUNI YA COCA-COLA YAPONGEZWA KWA UBUNIFU KUPITIA MICHEZO YA COPA COCA-COLA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA COCA-COLA YAPONGEZWA KWA UBUNIFU KUPITIA MICHEZO YA COPA COCA-COLA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/kampuni-ya-coca-cola-yapongezwa-kwa_29.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KAMPUNI YA COCA-COLA YAPONGEZWA KWA UBUNIFU KUPITIA MICHEZO YA COPA COCA-COLA"

Post a Comment

Loading...