Loading...
title : KATIBU MKUU AWABANA WAHARIBIFU MALI ZA CUF
link : KATIBU MKUU AWABANA WAHARIBIFU MALI ZA CUF
KATIBU MKUU AWABANA WAHARIBIFU MALI ZA CUF
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Chama cha Wananchi (CUF) kimewataka wanachama visiwani Zanzibar kutojiusisha na vitendo vya uharibifu pamoja uvunjifu wa amani mbavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya watu.
Kutokana na vitendo ambavyo vimefanya na baadhi ya watu Zanzibar CUF imefungua kesi namba 16 ya mwaka 2019 katika mahakama ya Vuga dhidi ya watu wote waliousika kushusha bendera na kubadilisha rangi za ofisi za Chama hicho kwa kuzipaka rangi ya chama cha ACT wazalendo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa CUF, Khalifa Suleiman khalifa alisema vitendo vinavyofanywa ni kinyume na sheria na vililenga kuvuruga amani.
"Ofisi zote ni mali ya CUF, na hiki Chama ni Taasisi na sio cha mtu mmoja, hivyo watu wote waliofanya uharibifu wa kuchoma moto bendera, kubadilisha rangi watachukuliwa hatua za kisheria" alisema Khalifa
Alifafanua kuwa mpaka sasa tayari wamekushany ushaidi wa matokeo yote yaliofanyika pamoja na majina ya watuhumiwa ambao watafikishwa mahakamani.
Alisema kuwa hakuna ofisi yoyote ya CUF ambayo ilinunuliwa na mtu binafsi au mwanachama kwani taarifa zote za mali za CUF zipo kwa msajili wa vyama vya siasa.
"Mpaka sasa tayari kuna ofisi zaidi 100 zimefanyiwa hujuma na nitahakikisha na simamia mali zote za chama" alisema Khalifa
Hata hivyo alieleza kuwa ziara ya aliyekuwa katibu Mkuu wa CUF Maalif Seif Sharif Hamad mjini Pemba ilikuwa ni kujitambulisha kwa wananchi kuwa amejiunga na ACT Wazalendo pamoja na kuwashawishi kumfata.
"Ile ziara ya pemba sio ya kujenga Chama Cha ACT Wazalendo ilikuwa ni kujitambulisha kwa wananchi pamoja na kuwaomba wanachama kumuunga mkono" alisema Khalifa
Katika hatua nyingine amewataka wabunge wote wa CUF kuendeleza ushirikiano na Chama chao kwa kufika ofisi na kupeana mikono na kukijenga Chama.
"Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba alishawasamehe wabunge wote kwa sasa kinachotakiwa kuwa na ushirikiano wa pamoja kutokana wabunge wamechaguliwa na wananchi" alisema Khalifa
Hivyo makala KATIBU MKUU AWABANA WAHARIBIFU MALI ZA CUF
yaani makala yote KATIBU MKUU AWABANA WAHARIBIFU MALI ZA CUF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU MKUU AWABANA WAHARIBIFU MALI ZA CUF mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/katibu-mkuu-awabana-waharibifu-mali-za.html
0 Response to "KATIBU MKUU AWABANA WAHARIBIFU MALI ZA CUF"
Post a Comment