Loading...

KCB BANK TANZANIA YAFANYA KINGAMANO LA KIBIASHARA JIJINI ARUSHA

Loading...
KCB BANK TANZANIA YAFANYA KINGAMANO LA KIBIASHARA JIJINI ARUSHA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KCB BANK TANZANIA YAFANYA KINGAMANO LA KIBIASHARA JIJINI ARUSHA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KCB BANK TANZANIA YAFANYA KINGAMANO LA KIBIASHARA JIJINI ARUSHA
link : KCB BANK TANZANIA YAFANYA KINGAMANO LA KIBIASHARA JIJINI ARUSHA

soma pia


KCB BANK TANZANIA YAFANYA KINGAMANO LA KIBIASHARA JIJINI ARUSHA


Benki ya KCB Tanzania imefanya kongamano la kwanza ya Biashara Club kwa mwaka 2019 jijini Arusha baada ya kuandaa kongamano kama hilo jijini Mwanza mwishoni kwa mwaka 2018. 

Zaidi ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi, KCB Biashara Club pia inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao kwa kuwakutanisha na wafanyabiashara wa nje na ndani ya nchi.

Tangu kuzinduliwa kwake, KCB Biashara Club imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara  kwa kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati yaani (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara.

Kongamano hilo lilikuwa na lengo mahususi la kukutanisha wadau mbali mbali katika sekta ya utalii wakiwemo wafanyabiashara na lilifanyika katika sehemu mbili ambapo sehemu yakwanza ilikuwa mahususi kwa wateja wa Benki ya KCB wapatao 250, huku sehemu ya pili ikiwa ni jukwaa la wazi kwa wakazi wengine wa Arusha kupata elimu ya huduma za kibenki kutoka kwa wataalam wa Benki ya KCB.

Akiongea wakati wa kufungua kongamano hilo, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Christine Manyenye alisema Benki ya KCB imefanya juhudi za mahususi za kuwaleta wadau kama Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.

 Kwa upande wake Meneja wa Tawi, Benki ya KCB Arusha, Judith Lubuva aliwapongeza wafanya biashara, wadau na wakazi wa Arusha kwa kuhudhuria kongamano. Aliongeza kwamba kongamano hilo limefanyika kwa wakati muafaka ambapo sekta ya utalii inaendelea kuimarika katika kanda ya kaskazini na Tanzania kwa ujumla.

Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabishara Wadogo na wa Kati (SME)  Abdul Juma aligusia fursa tofauti zinazoletwa na Biashara Club zikiwemo kuwakutanisha wafanya biashara mbali mbali wa nje na ndani ya nchi, kupanua wigo wa masoko kupitia safari za pamoja kwenda nchi kama China, Malaysia na Afrika Kusini. 

Juma aliwahakikishia wadau kwamba KCB Bank ina dhamira ya kuinua sekta ya utalii kwa kuitambulisha Tour Operator Account inayowezesha malipo ya kieletroniki pamoja na kuwana faida zingine zikiwemo huduma kwa njia ya mtandao kuwa bure na kutoa pesa bure.

Akiongea katika warsha hiyo, mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA), Ombeni Urio aliyekuwa mshauri wa masuala ya kodi, alisisitiza umuhimu wa wafanya biashara hao kufuata kanuni za kodi. Aliipongeza Benki ya KCB kwa kumualika ili aweze kutoa elimu hiyo ambayo ilikuwa inahitajika kwa sana.

 Mkuu wa Idara ya Masoko na Mahusaino Christine Manyenye akijibu maswali kutoka kwa wafanya biashara wa jijini Arusha katika kongamano lililohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 ikiwajumuisha wadau mbali mbali kutoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
 Afisa Masoko wa TANAPA  Ernest Jackinda akiongea na wageni waalikwa katika warsha ya Biashara Club iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Masuala ya Kibenki Masika Mukule akiongea na wageni waalikwa wakati wa maongezi ya ana kwa ana katika warsha ya Biashara Club iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.


Hivyo makala KCB BANK TANZANIA YAFANYA KINGAMANO LA KIBIASHARA JIJINI ARUSHA

yaani makala yote KCB BANK TANZANIA YAFANYA KINGAMANO LA KIBIASHARA JIJINI ARUSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KCB BANK TANZANIA YAFANYA KINGAMANO LA KIBIASHARA JIJINI ARUSHA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/kcb-bank-tanzania-yafanya-kingamano-la.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KCB BANK TANZANIA YAFANYA KINGAMANO LA KIBIASHARA JIJINI ARUSHA"

Post a Comment

Loading...