Loading...
title : KESI YA KUTUMIA LUGHA CHAFU YA MATUSI INAYOMKABILI HALIMA MDEE KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 16
link : KESI YA KUTUMIA LUGHA CHAFU YA MATUSI INAYOMKABILI HALIMA MDEE KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 16
KESI YA KUTUMIA LUGHA CHAFU YA MATUSI INAYOMKABILI HALIMA MDEE KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 16
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka katika kesi ya kutumia lugha chafu ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuhakikisha tarehe ijayo kesi hiyo inasikilizwa.
Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ameyasema hayo leo Machi 21, mwaka huu kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa na wakili wa serikali Dasy Makakala ambayo ameiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa kuwa faili hilo lilikuwa kwa wakili mwingine na bado hajalipitia.
Wakili wa utetezi, Hekima Mwesipu alidai, shauri hilo ni la muda mrefu kwani limebakiza miezi minne tu kufikisha miaka miwili huku ikiwa haijamaliza kusikilizwa hivyo ameomba hili liwe ahirisho la mwisho.
Baada ya kusema hayo, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 16, 2019.
Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wamekwishatoa ushahidi akiwamo mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga.
Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni, Mdee anadaiwa kutamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa “anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki” na kwamba kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mdee alifikishwa mahakamani hapo Julai 10, 2017 na yupo nje kwa dhamana.
Hivyo makala KESI YA KUTUMIA LUGHA CHAFU YA MATUSI INAYOMKABILI HALIMA MDEE KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 16
yaani makala yote KESI YA KUTUMIA LUGHA CHAFU YA MATUSI INAYOMKABILI HALIMA MDEE KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 16 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KESI YA KUTUMIA LUGHA CHAFU YA MATUSI INAYOMKABILI HALIMA MDEE KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 16 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/kesi-ya-kutumia-lugha-chafu-ya-matusi.html
0 Response to "KESI YA KUTUMIA LUGHA CHAFU YA MATUSI INAYOMKABILI HALIMA MDEE KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 16"
Post a Comment