Loading...
title : MAHAKAMA YAAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUWASILISHA TAARIFA ZA KESI YA MKURUGENZI WA NIDA NA WENZAKE
link : MAHAKAMA YAAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUWASILISHA TAARIFA ZA KESI YA MKURUGENZI WA NIDA NA WENZAKE
MAHAKAMA YAAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUWASILISHA TAARIFA ZA KESI YA MKURUGENZI WA NIDA NA WENZAKE
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeutaka upande wa mashitaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa zamani (NIDA), Dickson Maimu na wenzake, kuharakisha mchakato wa kuwasilisha taarifa Mahakama Kuu kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi.
Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Salim Ally ameyasema hayo leo Machi 5, 2019 baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kudai kuwa wapo katika kukamilisha taratibu za mwisho kuwasilisha nyaraka Mahakama ya Kuu, na kwamba wataitaarifu mahakama hiyo hatua walizofikia.
Hata hivyo, wakili wa utetezi, Joseph Ndunguru amedai upande wa mashitaka unatakiwa kusema ni taratibu zipi zinazokwamisha mpaka sasa ili mahakama itoe msaada maana tangu Januari 29, mwaka huu upande huo wa mashitaka wamekuwa wakidai upelelezi umekamilika na kuomba mahakama ipange kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa maelezo ya mashahidi.
Akijibu hoja hiyo, Wakili Simon amedai maandalizi wanayofanya ni ya nyaraka mbalimbali hivyo wanaomba wavumilie na kwamba hawataomba msaada kwao kwa sababu hatua hiyo ikikamilika watawapatia nyaraka.
Hatahivyo, Hakimu Ally alisema bado kuna mchakato wa kuwasilisha taarifa mahakama Kuu licha ya kwamba upelelezi umekamilika, ameongeza upande wa mashitaka wafanye mchakato na wasichukue muda mrefu bali muongeze spidi ili shauri liendelee.
Maimu na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 7/2019 na kuisabishia serikali hasara ya Sh bilioni 1.16.
kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 19, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Mbali na Maimu washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kayombo Xavery, Meneja Biashara wa (NIDA), Aveln Momburi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond.
Awali washitakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 26 likiwemo la uhujumu uchumi, ila Januari 28,2019 waliachiwa huru na mahakama hiyo baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) kusema hana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi yao.
Hata hivyo baada ya washitakiwa kuondolewa mashtaka hayo na kuachiwa huru walikamatwa tena na walifikishwa katika mahakama hiyo kisha kusomewa mashtaka mapya 100 yakiwemo 25 ya utakatishaji fedha.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 22 ya kughushi, mashtaka 43 ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri, mashtaka mawili ya kula njama, mashtaka 25 ya kutakatisha fedha na mashtaka matano ya kuisababishia hasara NIDA.
Pia washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la matumizi mabaya ya madara lipo moja ambalo linamkabili Maimu na Sabina.
Hivyo makala MAHAKAMA YAAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUWASILISHA TAARIFA ZA KESI YA MKURUGENZI WA NIDA NA WENZAKE
yaani makala yote MAHAKAMA YAAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUWASILISHA TAARIFA ZA KESI YA MKURUGENZI WA NIDA NA WENZAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUWASILISHA TAARIFA ZA KESI YA MKURUGENZI WA NIDA NA WENZAKE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/mahakama-yaagiza-upande-wa-mashtaka.html
0 Response to "MAHAKAMA YAAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUWASILISHA TAARIFA ZA KESI YA MKURUGENZI WA NIDA NA WENZAKE"
Post a Comment