Loading...

MBUNGE KIGAMBON "NAJIVUNIA ASILIMIA 67 YA KIGAMBONI IMEPIMWA"

Loading...
MBUNGE KIGAMBON "NAJIVUNIA ASILIMIA 67 YA KIGAMBONI IMEPIMWA" - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MBUNGE KIGAMBON "NAJIVUNIA ASILIMIA 67 YA KIGAMBONI IMEPIMWA", tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MBUNGE KIGAMBON "NAJIVUNIA ASILIMIA 67 YA KIGAMBONI IMEPIMWA"
link : MBUNGE KIGAMBON "NAJIVUNIA ASILIMIA 67 YA KIGAMBONI IMEPIMWA"

soma pia


MBUNGE KIGAMBON "NAJIVUNIA ASILIMIA 67 YA KIGAMBONI IMEPIMWA"


Mwambawahabari 
Mbunge wa Kigamboni (CCM), Dk Faustine, Ndugulile, amesema anajivunia kuongoza eneo ambalo ardhi yake asilimia 67 imepimwa jambo ambalo limesaidia katika kutatua migogoro ya ardhi na kuwa na ardhi inayotambulika.
Naibu waziri huyo wa afya ametoa kauli hiyo  alipokuwa akigawa mikataba wa ununuzi wa viwanja kwa wananchi wa Mtaa wa Mwasonga, Kata ya Kisarawe2, vinavyouzwa kwa mkopo na kampuni ya KC inayojishughulisha na upimaji na kuendeleza ardhi nchini.
Ndugulile, amesema kitendo cha KC kupeleka mradi huo ni katika kuendeleza juhudi hizo za Serikali na kuahidi hadi kufika mwaka 2020 wana imani ardhi yote itakuwa imepimwa kwa eneo lilibaki ni asilimia chache.
“Eneo la kisarawe2 ni la kimkakati kwa ajili ya biashara na tayari eka 1,000 zimetengwa kwa ajili ya viwanda, hivyo mlioamua kununua viwanja hapa hamtajuta kwani huko mbele ya Kigamboni inatarajiwa kuwa kitovu cha biashara katika mkoa wa Dar es Salaam ,”amesema Ndugulile.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya KC, Khalid Mwinyi, amesema viwanja hivyo huuzwa kwa mkopo ambapo mteja akishalipa asilimia 20 ya bei ya kiwanja husika, inayobaki analipa kwa miezi 20.
Mwinyi amebainisha kuwa wamekuja na mkakati huo kama njia ya kuwawezesha wananchi wenye kipato cha chini kumiliki ardhi ambapo  ekari 200 zilizopimwa zimechukuliwa na wananchi zaidi ya 900.
“Moja ya changamoto tuliyoipata katika kupata wateja ni pamoja na suala la wananchi kuamini kama kweli watapata viwanja kwa kile walichodai wameshatapeliwa sana huko nyuma, hivyo tunajitahidi kuwaonyesha sisi hatupo hivyo kwa kuweka kila kitu wazi, hivyo tunaomba wananchi watuamini tumekuja kuleta suluhisho la migogoro ya ardhi,” amesema.
Naye Naibu Meya wa Ilala, Omar Kumbilamoto, ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuna alichojifunza kuhusu umuhimu wa kuwa na maeneo ya kupimwa kutoka Kigamboni, ustaarabu ambao amesema atapeleka elimu hiyo Ilala ili nao waige mfano huo mzuri.
Wananchi waliokabidhiwa mikataba akiwemo Eleotheria Namikowi ambaye ni mkazi wa Mwananyamala na Bashiru Mkabala wa Ubungo, wamesema moja ya jambo lililowashawishi kuchukua viwanja hivyo ni pamoja na kukopeshwa vifaa vya ujenzi.


Hivyo makala MBUNGE KIGAMBON "NAJIVUNIA ASILIMIA 67 YA KIGAMBONI IMEPIMWA"

yaani makala yote MBUNGE KIGAMBON "NAJIVUNIA ASILIMIA 67 YA KIGAMBONI IMEPIMWA" Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE KIGAMBON "NAJIVUNIA ASILIMIA 67 YA KIGAMBONI IMEPIMWA" mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/mbunge-kigambon-najivunia-asilimia-67.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MBUNGE KIGAMBON "NAJIVUNIA ASILIMIA 67 YA KIGAMBONI IMEPIMWA""

Post a Comment

Loading...