Loading...
title : MGEJA AITOSA CHADEMA ARUDI CCM KWA KISHINDO
link : MGEJA AITOSA CHADEMA ARUDI CCM KWA KISHINDO
MGEJA AITOSA CHADEMA ARUDI CCM KWA KISHINDO
*Awapa CHADEMA ushauri mzito, ampongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kuleta maendeleo kwa watanzania
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
ALIYEKUWA mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga na baadaye kuhamia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Khamis Mgeja amerudi kwenye chama chake cha awali huku akiwaasa watanzania kutohadaika na propaganda za kuchafua taifa kwenye mataifa ya nje.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mgeja amesema kuwa alipumzika kwa muda katika masuala ya siasa na sio kustaafu kama inavyoelezwa na katika mapumziko hayo alipata wakati mzuri wa kutafakari mustakabali wa nchi kisiasa na kiuchumi na hasa kutafakari mwenendo wake wa kisiasa katika chama alichohamia akitokea CCM, na kugundua kuwa sababu zilizomfanya ahamie CHADEMA hazipo tena.
Amesema kuwa kwa muda aliokuwa CHADEMA walishauri kuhusu masuala ya kujenga nchi ikiwemo kuwa na sera mbadala, kuchangia bungeni, kuachana na mkakati wa kuichafua nchi nje ya nchi na kuacha siasa za kejeli na matusi lakini hawakusikilizwa.
Akieleza sababu zilizomfanya kuhamia CHADEMA Mgeja amesema kuwa walilenga mabadiliko ambayo yalilenga kuondoa kero kwa wananchi hasa kuboresha ustawi wao katika njanja zote muhimu lakini mambo yote hayo hayapo tena upinzani ila yanafanyika vizuri sana na kwa kasi ya ajabu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, na amesema kuwa walitumia muda wao mwingi kushauri chama hicho kuwa cha kisiasa na sio cha kiharakati lakini hawakusikilizwa na kueleza kuwa chama hicho kimegubikwa na ubinafsi na hakuna uwazi kabisa.
Aidha Mgeja ameomba radhi kwa mwenyekiti wa CCM taifa, wanachama, watanzania na familia yake huku akieleza sababu za kuamua kurudi nyumbani ikiwa ni pamoja na kazi nzuri za Rais Dkt. John Magufuli hasa mpango wa kuhamia Dodoma mpango uliokuwa tangu enzi za mwalimu Julius Nyerere pamoja na kuboresha sekta muhimu zikiwemo elimu, afya, barabara, reli,ununuzi wa ndege, miradi mikubwa ya umeme, kukemea vitendo vya rushwa pamoja na kutetea vitendo vya rushwa.
Vilevile Mgeja ametoa ujumbe wa CHADEMA kwa kuwahusia kuchukua maamuzi na kufanya harakati za kidemokrasia na kujenga hoja mbadala lasivyo wajiandae kisaikolojia kwa anguko kubwa litakalowakumba.
Hivyo makala MGEJA AITOSA CHADEMA ARUDI CCM KWA KISHINDO
yaani makala yote MGEJA AITOSA CHADEMA ARUDI CCM KWA KISHINDO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MGEJA AITOSA CHADEMA ARUDI CCM KWA KISHINDO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/mgeja-aitosa-chadema-arudi-ccm-kwa.html
0 Response to "MGEJA AITOSA CHADEMA ARUDI CCM KWA KISHINDO"
Post a Comment