Loading...
title : Mikataba Hoteli za Kitalii za Serikali kupitiwa
link : Mikataba Hoteli za Kitalii za Serikali kupitiwa
Mikataba Hoteli za Kitalii za Serikali kupitiwa
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu amesema Serikali inapitia mikataba na makubaliano ya wawekezaji waliopewa kuendesha Hoteli za Kitalii zinazomilikiwa na Serikali kwenye maeneo ya Hifadhi.
Kanyasu alitoa kauli baada ya kutembelea Hoteli ya Ngorongoro Wild Life Lodge iliyomo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni ziara yake iliyoanzia Hifadhi ya Serengeti, Manyara na kwingineko.
Naibu Waziri Kanyasu mara baada ya kuzungumza na Mejinementi ya NCAA, alisema kwamba hoteli hizo zilibinafsishwa kwa malengo ikiwamo kuona zinaendeshwa kwa faida, kuajiri Watanzania na kulipa kodi.
“Nitapita kwenye hoteli hizi moja baada ya nyingine kuangalia makubaliano ya kuziendesha ni yale yale au wamekiuka kama wamekiuka basi serikali itaangalia kwanza ushauri lakini kuvunja mkataba,” alisema Naibu Waziri Kanyasu.
Kaimu Mhifadhi wa NCAA Needpeace Wambuya kwa upande wake alisema moja ya jukumu lao n kuhakikisha ukaguzi wa utoaji huduma zenye viwango vya kimataifa unafanywa ndani ya hoteli zilizopo NCAA.
“Kwenye eneo hili la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro tuna hoteli kubwa tano ukijumlisha na nyingine za kawaida zinafikia hoteli 11,” alisema Wambuya.
Hivyo makala Mikataba Hoteli za Kitalii za Serikali kupitiwa
yaani makala yote Mikataba Hoteli za Kitalii za Serikali kupitiwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mikataba Hoteli za Kitalii za Serikali kupitiwa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/mikataba-hoteli-za-kitalii-za-serikali.html
0 Response to "Mikataba Hoteli za Kitalii za Serikali kupitiwa"
Post a Comment