Loading...

MKUU WA WILAYA NAMTUMBO ABAINI WIZI VYAMA VYA USHIRIKA

Loading...
MKUU WA WILAYA NAMTUMBO ABAINI WIZI VYAMA VYA USHIRIKA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKUU WA WILAYA NAMTUMBO ABAINI WIZI VYAMA VYA USHIRIKA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKUU WA WILAYA NAMTUMBO ABAINI WIZI VYAMA VYA USHIRIKA
link : MKUU WA WILAYA NAMTUMBO ABAINI WIZI VYAMA VYA USHIRIKA

soma pia


MKUU WA WILAYA NAMTUMBO ABAINI WIZI VYAMA VYA USHIRIKA

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh.Sophia Kizigo akifafanua jambo kwenye moja ya majukumu yake ya kazi.


*Ni baada ya baadhi ya viongozi kuiba Sh.milioni 33 ya tani 10 za korosho

*Aishauri Serikali kupitia upya Sheria ya Vyama vya ushirika kwani ...


Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo ametoa ombi kwa Serikali kuangalia upya Sheria ya Vyama vya Msingi,kwani amebaini zinatoa mwanya kwa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo ambao si waaminifu kuwaibia wakulima.

Kizigo ameeleza hayo baada ya kubaini wilayani Namtumbo kuna wizi ambao umefanyika kwenye moja ya vyama vya msingi na kusababisha wakulima kutoa malalamiko yao kwake na hivyo amechukua hatua kadhaa.

Baadhi ya hatua ambazo amechukua ni kufanya uchunguzi uliosaidia kuwapata viongozi wa vyama vya ushirika waliohusika na wizi huo kwa kuwaibia wakulima na kisha kuwaweka ndani.

Akizungumza na Michuzi Blog leo, Machi 28,2019,Mkuu wa Wilaya Kizigo amesema ofisi yake iliamua kufutilia na kubaini wizi huo baada ya kuwepo kwa malalamiko ya baadhi ya wakulima wa zao la korosho waliokuwa wakilalamika kutolipwa fedha zao wakati yeye anajua wengi wameshalipwa.

"Baada ya kufuatilia tukabaini wapo ambao waliingiziwa fedha kwenye  akaunti zao kumbe zilishakuwa mfu, pia wengine majina yao ya akaunti zao yalikuwa yanafanana na hivyo fedha kushindwa kuingia.Hata hivyo nimeshatoa maelekezo wale ambao wanasema hawajalipwa waandike majina yao ili nifuatile kwa kuyapeleka makao makuu ili tujue nani amelipwa na nani hajalipwa.

"Sababu ya tatu ni wizi ambao wameuasisi viongozi wa vyama vya ushirika wenyewe na kisha kuibia wakulima.Ukweli viongozi wa vyama vya ushiriki mmeiba sana na njia ambazo mnatumia kuiba ni nyingi sana.Kuna wizi wa kukata kilo , mkulima anakuja na kilo 10 na ninyi mnasema kilo tisa au nane,"amesema Kizigo.

Amefafanua wamechunguza na taarifa zote za wizi ulivyokuwa unafanyika na waliohusika wote wanawajua. "Tumebaini wapo wakulima ambao hajalipwa kabisa na fedha zao zimeliwa na viongozi ambao wamewateua wao na kuwaamini lakini ndio hao hao wanawaibia wakulima.Baadhi yao baada ya kuwabana wamekiri kuiba na tuliwaweka ndani."

Ameongeza korosho inayopatikana wilayani Namtumbo ndio bora na inashika nafasi ya kwanza kwa ubora duniani na kwamba kilo moja ya korosho ilitakiwa kulipwa Sh.3500.

"Tulipoongea na viongozi wao wa chama hicho cha msingi wamekiri kuibia wakulima ambapo Sh.milioni 33 zimeliwa na viongozi hao.Tulipombana mhasibu akasema bodi yote imeshiriki ingawa wengine walikataa.Tulipoona wanasumbua nikatoa agizo wakamatwe wote na kuwekwa ndani.

"Wakakaa kama siku tano au sita hivi , nikawaambia wakitaka kuachiwa walipe fedha ambayo wanadaiwa ambapo walilipa na kubaki kama Sh.milioni tisa.Cha kushangaza wakulima ambao walikuwa wanalalamika ndio hao hao wakawa wanaomba wawawekee dhamana, waliamua kuitisha na kikao na kisha wakachangishana fedha ili kuwatoa viongozi hao wakidai ni watoto wao,"amesema Kizigo.

Kutokana na hali hiyo amesema ili kukomesha tabia hiyo umefika wakati kwa Serikali kuangalia upya Sheria ya Vyama vya ushirika kwani inatoa mwanya kwa viongozi kuwaibia wakulima kwani sheria hiyo inaeleza wazi viongozi wa vyama vya ushirika wasiingiliwe na mtu yoyote yule wanapofanya maamuzi yao na inapotokea wizi wa fedha basi aliyehusika atatakiwa kulipa fedha tu.

"Sheria iliyopo haituruhusu kuingilia vyama vya ushirika.Hivi bila kuingilia wizi ambao umefanyika hapa Namtumbo hawa wakulima wangepata fedha zao kweli.Nitoe mwito kwa Serikali kuangalia upya sheria hii ili kukomesha tabia ya wizi inayofanywa na baadhi ya viongozi wasio waaminifu,"amesema Kizigo.


Hivyo makala MKUU WA WILAYA NAMTUMBO ABAINI WIZI VYAMA VYA USHIRIKA

yaani makala yote MKUU WA WILAYA NAMTUMBO ABAINI WIZI VYAMA VYA USHIRIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA WILAYA NAMTUMBO ABAINI WIZI VYAMA VYA USHIRIKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/mkuu-wa-wilaya-namtumbo-abaini-wizi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MKUU WA WILAYA NAMTUMBO ABAINI WIZI VYAMA VYA USHIRIKA"

Post a Comment

Loading...