Loading...

Morogoro kutumia Tsh. 355 Bil 2019/2020

Loading...
Morogoro kutumia Tsh. 355 Bil 2019/2020 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Morogoro kutumia Tsh. 355 Bil 2019/2020, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Morogoro kutumia Tsh. 355 Bil 2019/2020
link : Morogoro kutumia Tsh. 355 Bil 2019/2020

soma pia


Morogoro kutumia Tsh. 355 Bil 2019/2020



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akifungua kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) kilichofanyika Machi Mosi, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro
Wajumbe wa Kikao cha RCC wakiwa katika Ukumbi tayari kwa majadiliano.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Clifford Tandari (aliyesimama)akimkaribisha Mwenyekiti wa Kikao cha RCC kufungua kikao hicho kilichofanyika Machi Mosi, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro
Mbunge wa Jimbo la Malinyi Mkoani Morogoro Mhe. Haji Mponda akichangia hoja wakati wa kikao cha RCC kilichofanyika Machi Mosi, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro
Wajumbewa Kamati ya RCC wakisikiliza kwa makini mawasilisho ya sekta mbalimbali zilizowasilishwa kwenye kikao hicho kilichofanyika Machi Mosi, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro



…………………..

Na. Andrew Chimesela – Morogoro

Mkoa wa Morogoro umepanga kutumia zaidi ya shilingi 355Bil. katika Bajeti yake ya makadirio ya mwaka wa fedha 2019/2020 ambazo fedha hizo zitatumika katika matumizi mbalimbali ikiwemo mishahara ya watumishi wake, Maendeleo na matumizi mengine.

Hayo yalibainishwa katika kikao cha Ushauri cha Mkoa kilichofanyika Machi Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Mjini Morogoro ambapo wajumbe wake waliridhia makadirio ya Bajeti hiyo Kutumika.

Akiwasilisha Bajeti hiyo, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uratibu na Utawala Bw. Diaz Ndomba kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Clifford Tandari alisema bajeti hiyo imezingatia mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya mwaka 2019/2020 na Ilani ya Uchaguzi ya chama cha Mapinduzi (2015).

Aidha, amesema Bajeti hiyo imezingatia pia Dira ya Maendeleo ya Taifa (2020/2025), malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (2030) pamoja na malengo ya Mpango wa kufanya mageuzi ya kiuchumi wa Viwanda hapa nchini.

“kipaumbele kimeendelea kuwekwa katika kuimarisha mazingira wezeshi ya Ujenzi wa Viwanda vidogo, vya kati na vikubwa” alisisitiza Bw. Ndomba.

Mchanganuo wa bajeti hiyo ambayo ni ongezeko la asilimia 16 ukilinganisha na Bajeti ya mwaka 2018/2019 ni za matumizi ya kawaida ambapo Sh. 267,398,052,000 zitatumika kwa ajili ya mishahara huku matumizi mengineyo zitatumika Sh. 36,075524,000 na kufanya jumla yake kuwa Sh. 303,473,576,000.

Kwa upande wa Matumizi ya miradi ya Maendeleo Mkoa huo umepanga kutumia Sh. 37,817,411,000 ikiwa ni fedha za ndani na Sh. 13,953,937,000 zitakuwa ni fedha za nje na kufanya jumla 51,771,348,000 hivyo jumla kuu kufikia Sh. 355,244,924,000.

Mwisho wa mawasilisho hayo Mkoa ulitoa Ombi kwa Serikali kuu hususan Wizara ya Fedha na Mipango kuendelea kutoa kwa wakati fedha zilizopangwa na kupitishwa kama ilivyoainishwa kwenye mpango kazi wa Mkoa.

Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe aliendelea kuwaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa huo kusimamia rasilimali fedha zinazopatikana ikiwa ni pamoja na kukusanya mapato ya ndani kwa kutumia mashine za kiilektroniki na kuzipeleka Bank kwa wakati.

Aidha, aliwaonya watumishi wa umma wenye tabia ya kutumia vibaya fedha za Serikali kuacha tabia hiyo mara moja la sheria itawafuata huku akiwataka Wenyeviti wa Halmashauri hizo kuwachukulia hatua kali za kisheria na za kinidhamu watumishi hao watakaokiuka katika kutumia vibaya rasilimali fedha za Serikali.

“Ila tu ukivunja utaratibu ndio mambo mengine yanajitokeza kwa bahati nzuri Wenye viti wa Halmashauri mpo, kama hayo yanatokea msisite kuchukua hatua, kwa sababu miongozo ipo na wataalamu wapo muwape taarifa sahihi kwa ajili ya kuchukua hatua.”alisisitiza Dkt. Kebwe

Katika kipindi cha kujadili yatokanayo suala la Kijiji cha Ngombo kilichopo Wilaya ya Malinyi Mkoani humo liliibuka huku baadhi ya wajumbe wakitaka ufafanuzi zaidi ambapo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omari Mgumba (MB) aliwaka wajumbe pamoja na wananchi wa Kijiji cha Ngombo kuendelea na kazi zao kama kawaida kama Serikali ilivyoagiza lakini bila kufanya uendelezaji mwingine katika maeneo hayo hadi hapo Serikali itakapotoa kauli nyingine.

Aidha, Naibu Waziri huyo wa Kilimo alishauri kuwa ili Mkoa uwe na mipango sahihi juu ya kilimo ni lazima Mkoa kuwa na mpango Mkakati kuhusu kilimo na kusimamia kwa karibu zoezi la kupata takwimu sahihi za wakulima hususan wa mazao ya kimkakati kwa kuwasajili ili kujua idadi yao, mahali walipo, kiasi cha eneo wanalolima, mazao wanayolima pamoja na mahitaji yao ya msingi.


Hivyo makala Morogoro kutumia Tsh. 355 Bil 2019/2020

yaani makala yote Morogoro kutumia Tsh. 355 Bil 2019/2020 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Morogoro kutumia Tsh. 355 Bil 2019/2020 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/morogoro-kutumia-tsh-355-bil-20192020.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Morogoro kutumia Tsh. 355 Bil 2019/2020"

Post a Comment

Loading...