Loading...
title : RAIS WA JAMHURI YA RWANDA PAUL KAGAME KUWASILI KESHO NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI
link : RAIS WA JAMHURI YA RWANDA PAUL KAGAME KUWASILI KESHO NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI
RAIS WA JAMHURI YA RWANDA PAUL KAGAME KUWASILI KESHO NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI
Mhe. Paul Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, atawasili nchini tarehe 7 Machi 2019 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Ziara hiyo inafanyika kufuatia mwaliko wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ziara hii itatoa fursa kwa viongozi hao wawili kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Aidha, Viongozi hao wanatarajia kuzungumzia masuala mbalimbali ya mtangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe. Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda, atawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa Tisa Alasiri tarehe 7 Machi 2019 na kupokelewa na mwenyeji wake, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Rais Kagame anatarajia kuondoka nchini tarehe 8 Machi, 2019.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
6 Machi 2019
Hivyo makala RAIS WA JAMHURI YA RWANDA PAUL KAGAME KUWASILI KESHO NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI
yaani makala yote RAIS WA JAMHURI YA RWANDA PAUL KAGAME KUWASILI KESHO NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS WA JAMHURI YA RWANDA PAUL KAGAME KUWASILI KESHO NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/rais-wa-jamhuri-ya-rwanda-paul-kagame.html
0 Response to "RAIS WA JAMHURI YA RWANDA PAUL KAGAME KUWASILI KESHO NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI"
Post a Comment