Loading...

RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”, asema Daraja la Momba Kufungua fursa za kiuchumi kwa Wanarukwa,

Loading...
RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”, asema Daraja la Momba Kufungua fursa za kiuchumi kwa Wanarukwa, - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”, asema Daraja la Momba Kufungua fursa za kiuchumi kwa Wanarukwa,, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”, asema Daraja la Momba Kufungua fursa za kiuchumi kwa Wanarukwa,
link : RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”, asema Daraja la Momba Kufungua fursa za kiuchumi kwa Wanarukwa,

soma pia


RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”, asema Daraja la Momba Kufungua fursa za kiuchumi kwa Wanarukwa,

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ameliagiza jeshi la polisi Mkoani Humo kuhakikisha wanamsaka na kumkamata mganga wa jadi anayesadikiwa kuwaibua na kuwaadhiri wachawi katika bonde la ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga.

Agizo hilo limekuja baada ya kufanya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali katika bonde hilo pamoja na kujionea maendeleo na changamoto za shule ya sekondari Kipeta iliyoezuliwa paa pamoja na shule ya msingi Msia iliyobomoka madarasa manne kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyosababisha madhara hayo mwezi Disemba mwaka 2018.

Ameonya kuwa hataki yaliyotokea mkoa wa Njombe yajirejee katika Mkoa wa Rukwa ikiwa bado watu hawajasahau machungu waliyoyapata kutokana na matukio hayo, na kuongeza kuwa mganga huyo wa kienyeji analindwa na kiongozi wa chama cha kisiasa na hivyo kumtaka mkuu wa kituo cha Kijiji cha Kilyamatundu kuhakikisha anamkamta kiongozi huyo hata kama ni wa Chama cha Mapinduzi.

“OCS na vyombo vyako vile fanya upepelezi wa kina na ukamate yeyote yule ambae ametoka nje ya mkoa huu, nje ya Kilyamatundu anayefanya shughuli hizi, kamata weka ndani fanya mahojiano ya kina, na wengine nimeambiwa hap ani viongozi wa vyama vya kisiasa, usijali huyu ni chama tawala, huyu ni nani, kama ukijua kwa uhakika kamata mhoji mpaka kieleweke, sisi hatutaki kuletewa Lambalamba hapa,” Alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Wangabo aliwapongeza waalimu, Uongozi wa vijiji husika pamoja na wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha katika kuhakikisha majengo yaliyobomoka na kuezuliwa katika shule hizo yanarudi katika hali yake ya kawaida na hatimae wanafunzi kuendela na masomo.

Pamoja na michango ya wadau mbalimbali iliyohamasishwa na Wangabo ambayo imesaidia kurudishisa mapaa ya majengo ya utawala, mabweni mawili, nyumba sita za waalimu na vyoo vya wasichana na wavulana kwa shule ya sekondari Kipeta na kujenga madarasa manane kwa shule shule ya Msingi Msia, Wizara ya Elimu pamoja kwa ushirikiano na Wizara ya TAMISEMI imetoa shilingi Milinoni 75.2 kwaajili ya kuongezea ujenzi wa madarasa na vyoo kwa shule hizo.

Naye Diwani wa kata ya Milepa Apolinari Macheta alipongeza juhudi za Mkuu wa Mkoa kwa kuhakikisha shule hizo zinakuwa bora zaidi ya zilivyokuwa na kumuahidi kuwa Shilingi Milioni 48.6 walizopatiwa kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili na vyoo matundu sita kwa shule ya msingi Msia atahakikisha kwa ushirikiano wa wananchi watapata darasa jingine kwa fedha hizo.
Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewasisitiza wakati wa Kijiji cha Kilyamatundu, Kata ya Kipeta, Wilayani Sumbawanga kuhakikisha wanaitumia vyema fursa inayoletwa kwa kukamilika kwa ujenzi wa daraja la momba ili kuinuka kiuchumi.

Amesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo ni kufunguka kwa neema ambayo muda mrefu wanacnhi wamekuwa wakiisubiri na kuongeza kuwa kazi ya serikali ni kuhakikisha inaweka miundombinu sahihi ili kuwarahisishia wananchi wake kupata huduma wanazostahili na sio kuwawekea fedha wananchi mifukoni.

“Kwahiyo daraja hili la mto momba, nina hakika litakuza uchumi wa mikoa yetu, ndani ya mkoa wetu wa Rukwa na mikoa ya jirani, kuna Katavi watakuja kutumia lakini kuna jirani zetu wa Songwe na hata Mbeya, iliyopo ni kuongeza juhudi katika kuzalisha na hasa kilimo cha mpunga ambacho ndicho kinakubali huku, tulime zaidi halafu tuchakate, tuweke viwanda, awali nilishasema na nitarudia tena kutoa wito kwa wadau mbalimbali waje kuweka viwanda huku,” Alisisitiza.

Aidha, alisikitishwa na baadhi ya wafanyabiashra wanaotoka nje ya Mkoa wa Rukwa kuchukua mazao ya mkoa huo na kuyapeleka kwao na kisha kuweka kwenye vifungashio na kudai kuwa mazao hayo yanatoka katika mikoa yao.

Wakati akisoma taarifa ya mradi huo, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoani Rukwa Mhandisi Ndelalutse Karoza alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo ni muhimu sana kwa mikoa ya Rukwa na Songwe pamoja na Tanzania kwa ujumla na kubainisha kuwa ukamilifu wa daraja hilo utawainua wananchi kiuchumi na kijamii ikiwemo kupunguza gharama za usafirishaji wa mazao.

“Maendeleo ya kazi hadi kufikia Februari 2019 ni asilimia 95 kwenye daraja na asilimia 97 kwenye barabara za maunganisho, kazi muhimu zimekwisha kamilika na daraja linaweza kutumika, kazi ambazo hazijakamilika ni pamoja na alama za barabarani na kazi ya kuweka taa,” Alimalizia.
Ujenzi wa daraja la mto Momba  linalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe kwa upande wa bonde la ziwa Rukwa umefadhiliwa kwa asilimia 100 na serikali ya Tanzania na litagharimu shilingi bilioni 17.7 hadi kukamilika kwake tarehe 24.5.2019 ambapo mpaka sasa limekamilika kwa asilimia 95 na mkandarasi wa ujenzi huo ni Genjio Engineering Group Cooperation kutoka China.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (aliyevaa Kapelo) akiongoza ukaguzi wa ujenzi wa madarasa manane yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi na michango ya wadau katika shule ya Msingi Msia, kata ya Milepa Wilayani Sumbawanga. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (kushoto)  akipewa maelezo juu ya marekebisho yanayoendelea katika ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Msia na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga  Kalolo Ntila (kaunda suti nyeusi) wakati wa kuyakagua madarasa hayo.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea. 
 Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akikabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa niaba ya umoja wa waalimu wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Kipeta kwaajili ya wanafunzi ambao vitabu vyao vilirowa na mvua kutokana na mabweni kuezuliwa.



 Daraja la Momba linalounganisha Mkoa wa Rukwa na Katavi lenye urefu wa mita 84 na kugharimu shilingi bilioni 17.7
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyevaa kapelo) pamoja na wataalamu alioambatana nao wakitembea juu ya daraja hilo ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa daraja hilo lipo tayari kwa matumizi ya kuvuka kutoka mkoa wa Rukwa na kuelekea mkoa wa Songwe.
 Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wakitembea juu ya daraja hilo kuonyesha mwanzno wa matumizi ya daraja hilo muda mfupi baada ya kusikiliza nasaha za Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo. 
 Picha ya pamoja ya wataalamu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoani Rukwa pamojana Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (wa nne toka kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyevaa kapelo)


Hivyo makala RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”, asema Daraja la Momba Kufungua fursa za kiuchumi kwa Wanarukwa,

yaani makala yote RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”, asema Daraja la Momba Kufungua fursa za kiuchumi kwa Wanarukwa, Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”, asema Daraja la Momba Kufungua fursa za kiuchumi kwa Wanarukwa, mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/rc-wangabo-aagiza-kusakwa-na-kukamatwa_9.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”, asema Daraja la Momba Kufungua fursa za kiuchumi kwa Wanarukwa,"

Post a Comment

Loading...