Loading...
title : SAMATTA KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KIMATAIFA
link : SAMATTA KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KIMATAIFA
SAMATTA KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KIMATAIFA
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Bodi ya Utalii Tanzania(TTB), Ipo katika hatua za mwisho za Mazungumzo na Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Klabu ya Genk iliyopo nchini Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta kuwa Balozi wa kutangaza Utalii wetu Kimataifa.
akziungumza na Waandishi wa habari Mapema leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Muendeshaji wa Bodi hiyo, Devotha Mdachi amesema kuwa katika hatua ya kutangaza utalii kimataifa wameona wamtumie Mbwana Samatta.
"wote tunajua umaharufu wa Mchezaji wetu katika ligi ya ubegiji na soka la barani ulaya kwa sasa hivyo katika Malengo yetu ya kutumia watu maharufu ambao ni Vijana wa kitanzania tumezungumza na Mbwana Samatta na ametuambia kuwa ifikapo mwezi May atakapokuja katika mapumziko yake kila kitu kitakamilika"anasema Mdachi.
ametaja kuwa mbali ya Mbwana Samatta wapo wasanii wengi na Vijana Maharufu ambao wanataraji kuwafikia hili wawe mabalozi wa utalii wetu nchini lakini kwa kuanzia wameanza na Samatta pamoja na Miss Tanzania .
Samatta atakuwa Kijana wa Pili wa Kitanzania Mwenye Mafanikio ambaye atapata nafasi ya kuwa balozi wa TTB ambapo ametanguliwa na Miss Tanzania 2018/2019 Queen Elizabeth Mukune ambaye amesaini Mkataba leo.
--
Hivyo makala SAMATTA KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KIMATAIFA
yaani makala yote SAMATTA KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KIMATAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SAMATTA KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KIMATAIFA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/samatta-kuutangaza-utalii-wa-tanzania.html
0 Response to "SAMATTA KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KIMATAIFA"
Post a Comment