Loading...
title : SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA MATIBABU KWA MTANDAO
link : SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA MATIBABU KWA MTANDAO
SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA MATIBABU KWA MTANDAO
Na WAMJW - DOM
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo imezindua Mfumo mpya wa utoaji huduma za afya kwa njia ya mtandao utaosaidia kurahisisha utoaji wa huduma za Afya ikiwemo huduma za matibabu ya kibingwa kwa wananchi.
Uzinduzi huo umefanyika leo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 7 wa masuala ya Sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki kujadili kwa pamoja juu ya njia ya kufanikisha malengo ya Afya ya umoja wa mataifa.
Mhe. Samia alisema kuwa nchi za Afrika Mashariki zikijikita katika utoaji huduma kwa mfumo huo kwa ushirikiano wa pamoja, itakuwa ni njia sahihi kwa nchi hizo kufikia malengo ya milenia na huduma za afya kwa wote.
“Tunapaswa kufikia malengo tuliyojiwekea kama bara la Afrika na nchi za Afrika mashariki, mkutano huu si tu wa watafiti kutoka Afrika Mashariki bali ni muhimu kwa wadau wote katika sekta ya afya tufanye kazi kwa pamoja kukamilisha malengo haya,” alisema Mhe. Samia.
Mhe. Samia aliendelea kusema kuwa tiba mtandao itawezesha na kuongeza ufanisi katika kufanya uchunguzi, utoaji wa tiba na dawa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali, hivyo kurahisisha utoaji huduma za Afya kwa Wananchi.
Aidha, Mhe. Samia Aliongeza kuwa tiba mtandao itapunguza gharama za wagonjwa na wanaowahudumia kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu katika Vituo vyakutolea huduma na Hospitali.
Nae,Waziri wa Afya na mapambano dhidi ya VVU kutoka Burundi Dkt. Thaddee Ndikumana alisema programu hiyo itakuwa ikitumika kwa nchi za Afrika Mashariki itakuwa chachu katika kuleta Mapinduzi ya utoaji huduma za Afya kwa Wananchi wa Afrika Mashariki.
“wananchi wa Burundi watakuwa wanaweza kupatiwa matibabu na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa nchini kwao bila kuja Dar es Salaam hiyo ni kitu muhimu tutakuwa tunabadilishana uzoefu raia wa Burundi walikuwa wanakuja kila siku sasa safari zitapungua, watabaki Bunjumbura na huduma watapata.” Amesema Dkt. Thaddee Ndikumana
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa daktari atakuwa na uwezo wa kuwasiliana na madaktari wenzake katika mtandao na madaktari bingwa wa nchi nzima wanaona lile tatizo jambo litalosaidia katika kutoa huduma bora kwa Wananchi wan chi za Afrika Mashariki.
Waziri Ummy Mwalimu, aliendelea kusema kuwa tayari Tanzania ilishaingia katika mfumo wa matumizi ya kidijitali katika utoaji wa huduma kwenye maeneo mengi, na umekuwa na msaada mkubwa sana katika Sekta ya Afya.
“Nchini Tanzania miezi mitatu iliyopita madaktari walianzisha mfumo mawasiliano kupitia dijitali ambao unawawezesha madaktari bingwa kuwasiliana moja kwa moja na madaktari waliopo pembezoni na umeweza kuokoa maisha ya kinamama sita ambao walikuwa wanajifungua,” amesema Ummy.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Nimr Profesa Yunus Mgaya alisema kuwa mfumo huo utapunguza gharama za utoaji wa huduma za afya na itaongeza ufanisi katika utendaji wa kazi wa wahudumu wa afya.
“Italeta utaalamu wa hali ya juu wa kibingwa katika maeneo ambayo hauwezi kufikika kwa mfano wataalamu wanaweza kuwepo Muhimbili na mgonjwa akawa mbali ambako hapafikiki kirahisi na hiyo ni msaada mkubwa sana kwa kuwa hizi huduma kama ingetakiwa wataalamu wawepo kule gharama yake ingekuwa kubwa sana,” alisema Prof. Mgaya.
Nae, Waziri wa Mambo ya Nje, Palamagamba Kabudi amesema kuwa nchi ya Tanzania itanufaika zaidi katika mfumo huo katika kulifikia lengo namba tatu la malengo ya milenia, pia itasaidia kufanikisha lengo la afya kwa wote ifikapo 2030.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akibofya batani, ikiwa ni ishara ya kuzindua Mfumo mpya wa utoaji huduma za afya kwa njia ya mtandao, katika Mkutano wa 27 wa masuala ya Sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki katika Kituo cha mikutano ya Kimataifa cha J.K Nyerere Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akinyanyua juu kitabu cha Mwongozo wa Mfumo mpya wa utoaji huduma za afya kwa njia ya mtandao utaosaidia kurahisisha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje, Palamagamba Kabudi na Watatu kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akitoa hotuba yake katika Mkutano wa 27 wa masuala ya Sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki katika Kituo cha mikutano ya Kimataifa cha J.K Nyerere leo jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Wakulia) akipata maelekezo, wakati alipita katika mabanda ya maonesho baada ya kumaliza Mkutano wa Kimataifa wa 7 wa masuala ya Sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki, mkutano huo umefanyika katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha J.K Nyerere Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (watatu kutoka kulia)akipata maelekezo katika banda la (TFDA) wakati alipita katika mabanda ya maonesho baada ya kumaliza Mkutano wa Kimataifa wa 7 wa masuala ya Sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki, mkutano huo umefanyika katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha J.K Nyerere Jijini Dar es salaam.
Wadau wa masuala ya Afya, kutoka nchi mbali mbali wakifuatilia ufunguzi wa wa mkutano wa 7 wa masuala ya sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa Afya kutoka nchi za Afrika Mashariki, mkutano huo ulifunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Hayupo kwenye picha)
Hivyo makala SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA MATIBABU KWA MTANDAO
yaani makala yote SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA MATIBABU KWA MTANDAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA MATIBABU KWA MTANDAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/serikali-yazindua-mfumo-wa-matibabu-kwa.html
0 Response to "SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA MATIBABU KWA MTANDAO"
Post a Comment