Loading...
title : SIKU YA WANAWAKE YAACHA ALAMA RUBALE, BUKOBA .
link : SIKU YA WANAWAKE YAACHA ALAMA RUBALE, BUKOBA .
SIKU YA WANAWAKE YAACHA ALAMA RUBALE, BUKOBA .
Anaandika Abdullatif Yunus - Bukoba Kagera.
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, ambayo huadhimishwa Machi 08 kila Mwaka, Wanawake wa Kata Rubale wamejitokeza kwa wingi na kujitolea Vifaa vya Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Rubale Wilaya ya Bukoba, Wodi inayotarajiwa kuanza kujengwa mara moja.
Kufuatia Sherehe hizo zilizohudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali, Taasisi, Mashirika na Wadau wa Maendeleo, Mgeni Rasmi katika Shughuli hizo Mwenyekiti wa Halmasahuri ya Bukoba Murshidi Ngeze amelishukuru Shirika La World Vision Rukoma AP kwa kukubali kusaidia kiasi cha Fedha Shilingi Milioni 67 kwa ajili ya Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto, itayojengwa katika Kituo cha Afya Rubale ambapo gharama za Shughuli nzima za Ujenzi huo, ni Shilingi Milioni 22, Mbali na pesa hiyo kutoka shirika la World Vision tayari Kuna vifaa vya Ujenzi ambavyo vimekwisha tolewa na wadau pamoja na wananchi huku wengine wakiahidi kuleta.
Aidha Mh. Ngeze ameeleza nia ya Serikali ya Kuendelea Kuboresha Afya kwa akina mama hao na jamii kwa ujumla na kuwakumbusha umuhimu wa Kuwa na Bima ya Afya kwa kila kaya na faida zake, lakini pia Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa Eneo la Bujunangoma Kata Kemondo Wilayani Humo.
Mh. Ngeze akitoa ujumbe wake kwa Akina Mama hao amewaomba kuendelea kuwa walezi bora kwa familia zao hususani mabinti zao, kuwajenga katika misingi bora na kuwalinda dhidi ya Vishwawishi wanavyokumbana navyo vinavyopelekea mimba za Utotoni na mimba zisizotarajiwa na hatimae kukosa Elimu..
Kikundi cha Akina mama toka Kijiji Migara wakiwa wamebeba tofali za Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto, tofali hizi na mawe ni Vifaa walivyobeba kutoka Majumbani kwao.
Pichani ni sehemu ya Akina mama waliohudhuria Sherehe za Siku ya Wanawake Duniani ambapo Kwa Wilaya ya Bukoba sherehe hizi Kiwilaya zimeadhimishwa Katika Kata ya Rubale
Pichani Ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Murshidi Ngeze akipokea Vifaa vya Ujenzi Kutoka kwa Akina Mama wa Kata ya Rubale kama ishara ya uzinduzi wa Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto, pembeni ni Diwani wa Kata Rubale Rutta Kitale.
Pichani ni Bi. Penina Petro Meneja toka TADEPA akitoa salaam za Shirika lao, TADEPA wamekuwa wadau wakubwa wa Maendeleo ya Akina Mama Kata Rubale kwa Kuviwezesha Vikundi vya Ujasiliamali Mikopo midogo midogo.
Pichani ni Bwn. Gratian Rwezaula Afsa mwezeshaji wa Shirika la World Vision Rukoma AP, akizungumza na Wananchi (hawapo pichani) waliohudhuria Sherehe za Siku ya Wanawake Duniani Iliyofanyika Kiwilaya Kata ya Rubale, Rukoma Kama wadau wa Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto wametoa Shilingi Milioni 67.
Pichani ni Bi. Celina Willbard Mwwnyekiti wa Kikundi cha Muungano, akiwakilisha Wanakikundi wenzake kwa kuleta Jiwe kutoka Nyumbani kwake, kama mchango wake wa Ujenzi wa Wodi ya Akina Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Rubale
Hivyo makala SIKU YA WANAWAKE YAACHA ALAMA RUBALE, BUKOBA .
yaani makala yote SIKU YA WANAWAKE YAACHA ALAMA RUBALE, BUKOBA . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIKU YA WANAWAKE YAACHA ALAMA RUBALE, BUKOBA . mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/siku-ya-wanawake-yaacha-alama-rubale.html
0 Response to "SIKU YA WANAWAKE YAACHA ALAMA RUBALE, BUKOBA ."
Post a Comment