Loading...
title : TAASISI ZA USANIFU NA UHANDISI WATAKIWA KUWA WABUNIFU
link : TAASISI ZA USANIFU NA UHANDISI WATAKIWA KUWA WABUNIFU
TAASISI ZA USANIFU NA UHANDISI WATAKIWA KUWA WABUNIFU
Na Woinde Shizza,Arusha
Naibu waziri wa viwanda,baishara na uwekezaji mhandisi Stela Manyanya ameitaka taasisi ya uhandisi na usanifu wa mitambo Tanzania(temdo )kuendelea kuwa wabunifu zaidi katika uzalishaji wao wa teknolojia ili wawweze kusanifu mitambo inayokidhi malengo ya serikali ya kuanzisha taasisi hiyo.
Injinia manyanya aliyasema hayo wakati kamati ya bunge ya viwanda,biashara na mazingira ilipotembelea taasisi ya TEMDO kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi.
Amesema kwa kuwa serikali inatambua mchango mkubwa wa Temdo katika kusanifu mitambo ni vema tasisi hiyo ikaongeza ubunifu zaidi katika uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya serikali ya kuzalisha bidhaa zinazoenda na wakati
Ameongeza kuwa serikali itaangalia namna ya kuendelea kuziwezesha taasisi hizo za utengenezaji wa zana za kilomo na mashine kwa kuzitolea fedha za bajeti ili ziendelee kuzalisha zana na mitambo yenye kukidhi mahitaji ya wananchi na viwanda.
Kwa upande wake Mwenyekiti Wa kamati yakudunu ya bunge viwanda ,biashara na Mazingira aliwataka pia taasisi hiyo kujiendesha kibiashara zaidi ,wazalishe fedha za ndani.
"Nendi kibiashara zaidi mtazalisha fedha zenu wenyewe ambazo zitawasaidia kuendelea kujiendesha hata kama fedha za bajeti za serikalini zikichelewa kuwafikia nyie mnaendelea kujiendesha wenyewe sio kukaa na kusubiri tu fedha za bajeti zije" alisema Mwenyekiti.
Kaimu meneja wa ushauri viwandani kutoka taasisi ya TEMDO Alexander Komba amesema ujio wa kamati ya bunge katika tassisi hiyo kunaiwezesha serikali kuweza kuongeza nguvu zaidi iliwaweze kuwa wabunifu katika teknolojia zenye kukidhi mahitaji ya soko kufuatia vitendea kazi wanavyonunua kupitia fedha wanazopewa za bajeti.
Kamati ya Kudumu Bunge ya viwanda ,biashara na mazingira ikikagua mashine zilizopo katika taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo Tanzania (TEMDO) iliopo jijini Arusha (Picha na Woinde Shizza).
Hivyo makala TAASISI ZA USANIFU NA UHANDISI WATAKIWA KUWA WABUNIFU
yaani makala yote TAASISI ZA USANIFU NA UHANDISI WATAKIWA KUWA WABUNIFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAASISI ZA USANIFU NA UHANDISI WATAKIWA KUWA WABUNIFU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/taasisi-za-usanifu-na-uhandisi-watakiwa.html
0 Response to "TAASISI ZA USANIFU NA UHANDISI WATAKIWA KUWA WABUNIFU"
Post a Comment