Loading...
title : Taswara za Edward Lowassa Alirejea Chama Cha Mapinduzi CCM.*Mwenyewe asema ametafakari na kuamua kurudi nyumbani *Rais Dk. Magufuli Atoa Neno, CCM Wachekelea Kila Kona.
link : Taswara za Edward Lowassa Alirejea Chama Cha Mapinduzi CCM.*Mwenyewe asema ametafakari na kuamua kurudi nyumbani *Rais Dk. Magufuli Atoa Neno, CCM Wachekelea Kila Kona.
Taswara za Edward Lowassa Alirejea Chama Cha Mapinduzi CCM.*Mwenyewe asema ametafakari na kuamua kurudi nyumbani *Rais Dk. Magufuli Atoa Neno, CCM Wachekelea Kila Kona.
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
WAZIRI Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Edward Lowassa ametangaza rasmi kurudi Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuanzia leo Machi 1,2019.
Lowassa aliondoka CCM na kwenda upinzani katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wakati wa mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.Aliondoka CCM na kwenda upinzani baada ya jina lake kukatwa katika kugombea urais kupitia Chama hicho.
Hivyo alipata ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais kupitia Chadema waliokuwa wameunganisha nguvu na vyama vingine vinne vya siasa vilivyokuwa vimeunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Akiwa upinzani Lowassa aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema lakini kuna kipindi aliamua kwenda Ikulu kufanya mazungumzo na Rais Dk.Magufuli ambapo baada ya kukutana na Rais alisema amevutiwa na utendaji kazi wake na anampongeza.
Akizungumza leo katika Ofisi za ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam,Lowassa hakuwa na maneno mengi ya kueleza zaidi ya kuwaambia Watanzania kuwa ameamua kurudi nyumbani (CCM).
"Nimetafakari na sasa nimeamua kurudi nyumbani CCM ambako sehemu kubwa ya maisha yangu nimekuwa huko,"amesema Lowassa huku mamia ya wananchi wakiwamo wanachama na wapenzi wa CCM walikuwa wanamshangilia.
Wakati Lowassa anatangaza kurejea CCM alikuwa amesikindikizwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga ambaye pia aliwahi kuwa Mtunza wa fedha wa CCM Rostam Aziz.
Akizungumza baada ya Lowassa kurudi CCM, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli amesema wamempokea Lowassa na katika kuthibitisha hilo waliona ni vema uamuzi wake akautangazia Ofisi za CCM Lumumba kama sehemu ya uthibitisho.
"Kama ambavyo amezungumza kwa kifupi mwenye Mzee Lowassa kwamba amerudi nyumbani ambako ni huku CCM, tumempokea.Amekuja kutangazia hapa Lumumba kama sehemu ya kutoa shuhuda.
"Kwa upande wetu tumekaa, tumefakari na kujiridhisha Lowassa amekaa kwenye Chama kwa muda mrefu na kwa bahati mbaya zilizojotokeza aliamua kwenda upinanzani.Tumemsikiliza mawazo yake kwamba amekaaa kwenye Chama Cha Mapinduzi sehemu kubwa ya maisha yake na kwamba kutokana na sababu ambazo amezieleza aliamua kwenda upinzani na leo hii amerudi nyumbani,"amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo kabla ya Rais Magufuli kuzungumza aliamua kuwatania watu waliokuwa wamejitokeza Lumumba na kuwaambia imekuaje wako hapo au wanamaono na hivyo walijua kitakachotokea.
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru Ally amesema Lowassa amefikia uamuzi wa busara kwa kurudi nyumbani kwa ajili ya kushirikiana katika kuleta maendeleo ya wananchi wote.
"Amerudi nyumbani, kwa hiyo tunaanza kazi ya kujenga Taifa letu na kujenga utu wetu, Lowassa ni kiongozi ambaye ametoa mchango mkubwa katika nchi yetu.Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama chetu tumepanga kumpokea na yupo tayari kushirikiana nasi kuwatumikia wananchi,"amesema Dk.Bashiru.
Hata hivyo uamuzi huo wa Lowassa umeonekana kuwakosha wana-CCM kwani baadhi yao wameonesha kufurahia uamuzi huo.
WAZIRI Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa akiwasili Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally akimpokea Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa aliyeongozana na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho walipowasili Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally wakimwangalia Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa akiweka sahihi kweny kitabu cha wageni akiwa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho walipowasili Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally wakiongea na Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho walipowasili Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally wakiongea na Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho walipowasili Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpeleka ofisini kwake Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa alipowasili Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia wakati Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz wakisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati wa maongezi na Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea jambo na Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa wakati wakitoka nje wakuwa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa wakati akitangazia umma rasmi kwamba anarudi nyumbani akiwa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa wakati akitangazia umma rasmi kwamba anarudi nyumbani akiwa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea baada ya Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa kuutangazia umma rasmi kwamba anarudi nyumbani akiwa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa baada ya kuutangazia umma rasmi kwamba anarudi nyumbani akiwa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa baada ya kuutangazia umma rasmi kwamba anarudi nyumbani akiwa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa baada ya kuutangazia umma rasmi kwamba anarudi nyumbani akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019.
PICHA NA IKULU
PICHA NA IKULU
Hivyo makala Taswara za Edward Lowassa Alirejea Chama Cha Mapinduzi CCM.*Mwenyewe asema ametafakari na kuamua kurudi nyumbani *Rais Dk. Magufuli Atoa Neno, CCM Wachekelea Kila Kona.
yaani makala yote Taswara za Edward Lowassa Alirejea Chama Cha Mapinduzi CCM.*Mwenyewe asema ametafakari na kuamua kurudi nyumbani *Rais Dk. Magufuli Atoa Neno, CCM Wachekelea Kila Kona. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Taswara za Edward Lowassa Alirejea Chama Cha Mapinduzi CCM.*Mwenyewe asema ametafakari na kuamua kurudi nyumbani *Rais Dk. Magufuli Atoa Neno, CCM Wachekelea Kila Kona. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/taswara-za-edward-lowassa-alirejea.html
0 Response to "Taswara za Edward Lowassa Alirejea Chama Cha Mapinduzi CCM.*Mwenyewe asema ametafakari na kuamua kurudi nyumbani *Rais Dk. Magufuli Atoa Neno, CCM Wachekelea Kila Kona."
Post a Comment