Loading...

TFDA YAJIVUNIA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KATIKA KUDHIBITI UBORA WA DAWA, VIFAA TIBA, VIPODOZI NA VITENDANISHI

Loading...
TFDA YAJIVUNIA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KATIKA KUDHIBITI UBORA WA DAWA, VIFAA TIBA, VIPODOZI NA VITENDANISHI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TFDA YAJIVUNIA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KATIKA KUDHIBITI UBORA WA DAWA, VIFAA TIBA, VIPODOZI NA VITENDANISHI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TFDA YAJIVUNIA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KATIKA KUDHIBITI UBORA WA DAWA, VIFAA TIBA, VIPODOZI NA VITENDANISHI
link : TFDA YAJIVUNIA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KATIKA KUDHIBITI UBORA WA DAWA, VIFAA TIBA, VIPODOZI NA VITENDANISHI

soma pia


TFDA YAJIVUNIA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KATIKA KUDHIBITI UBORA WA DAWA, VIFAA TIBA, VIPODOZI NA VITENDANISHI


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JITIHADA za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli za kuhakikisha inadhibiti ubora wa dawa na vifaa tiba umeiwezesha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kushika nafasi ya kwanza Barani Afrika na kwa duniani kuwamo kwenye orodha ya nchi 50 tu ambazo zipo kwenye levo ya tatu katika udhibiti wa ubora wa dawa, vifaa tiba, vipodozi na vitendanishi .

Kwa mujibu wa TFDA, mchakato wa kufikia levo ya tatu ni mrefu na unahatua mbalimbali zikiwemo za wataalam wa Shirika la Afya Duniani kufuatilia mifumo, maabara, kuhoji na kufanya uchunguzi kwa lengo la kujiridhisha ambako kote huko mamlaka hiyo ilifanikiwa na hatimaye mwaka jana ikafikia hatua hiyo na kuifanya Tanzania kuwa nchi pekee kwa nchi za Bara la Afrika kufikia levo tatu.

Ifahamike leo Machi 27,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuna mkutano mkubwa wa wanasayansi ambao umeshirikisha nchi za Afrika Mashariki na kuhudhuriwa na watalaam na wadau mbalimbali . TFDAimeamua kuweka banda lake katika mkutano huo kwa lengo la kutoa elimu kwa umma na kubwa zaidi kuzifahamisha nchi za Afrika Mashariki kuwa Mamlaka hiyo imepiga hatua kubwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) inatambua uwezo wake wa kimifumo katika kudhibiti ubora.

Wakizungumza na Michuzi Blog, Ofisa Mkuu Uelimishaji Umma James Ndege na Ofisa Mwandamizi Uelimishaji Umma Roberta Feruzi wote kutoka TFDA wamesema Tanzania imefanikiwa kupiga hatua kubwa katika eneo la udhibiti wa ubora wa dawa na vifaa tiba na hiyo imetokaa na jitihada ambazo zinafanywa na Serikali katika kuweka mifumo ya kisasa katika maabara mbalimbali za TFDA pamoja na utoaji wa mafunzo ya mara kwa mara kwa watalaam.

"Mwaka jana ndio tulifanikiwa kufika levo ya tatu na kwa Afrika ni Tanzania pekee kupitia TFDA ndio tumefikia hatua hiyo.Kwa maana nyingine TFDA ilikofikia haina tofauti na mataifa makubwa yakiwamo ya nchi za Ulaya ambayo nayo yapo hatua hiyo hiyo ambayo nasi tunayo.

"Kwa duniani kote kuna nchi 50 tu ambazo zipo levo ya tatu na Tanzania ni miongoni mwao.Kwa maana rahisi ni kwamba katika mifumo bora ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba ni kumhakikisha mlaji anachotumia tunakifahamu, tunajua kinakozalishwa, kinatumika vipi, na tunafuatilia hatua kwa hatua kwa lengo la kumhakikisha usalama mlaji,"amesema Ndege.

Ndege amesema ilipofikia TFDA ni jambo la kujivunia kwa nchi zote za Bara la Afrika kwani inatoa tafsiri kuwa Bara la Afrika linaweza kufanya mambo makubwa na hivyo kikubwa ni kuweka mikakati na malengo ya kusonga mbele."Tuko hapa kuiambia jamii ya Afrika Mashariki TFDA tunaweza na tunasonga mbele."

Kwa upande wake Feruzi amesema mafanikio ya TFDA yametokana na jitihada ambazo Serikali inazifanya kwa kuijenga uwezo, kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya maabara pamoja na kuwajengea uwezo watalaam wa TFDA na hatimaye kwa pamoja kufikia lengo ambalo ni kuhakikisha mamlaka hiyo inatimiza majukumu yake kikamilifu.

Feruzi amesema uamuzi wa Serikali kuijengea uwezo TFDA, imekuwa na uwezo mkubwa katika ufanya uchunguzi na kufuatilia hatua kwa hatua mambo ambayo wanayasimamia huku akitolea mfano katika eneo la dawa kabla ya kuingia nchini TFDA kupitia watalaam wake inakwenda eneo ambako dawa inazalishwa na kujiridhisha na ubora wake.

Pia amesema si tu kuzifuatilia maeneo ambayo dawa zinazalishwa bali wamekuwa na mfumo kwa kutumia maabara zake zinafanya uchunguzi wa kujiridhisha kwa kina na ubora wa dawa kabla ya kufika kwa mtumiaji na hawaishi hapo kwani wanafuatilia hata baada ya kuingia nchini.

"TFDA kupitia watalaam wetu na maabara zetu pia tunafanya majaribio ya dawa kabla haijaingia sokoni.Lazima tujiridhishe kwanza na ndipo sasa turuhusu, pale ambapo tunabaini kuna kitu hakiko sawa tunatoa taarifa kwa wahusika ambao ndio wazalishaji ili watoe ufafanuzi na tukiridhika tunaendelea na hatua zinazofuata.Kutokana na ufuatiliaji makini ambao TFDA tunao, ndio umetuwezesha kuaminika na kufikia levo ya tatu,"amesema .

Amefafanua kabla ya kufika levo ya tatu, kuna levo ya kwanza ambayo hiyo ni kwa ajili ya nchi ambazo zinaanza , kisha kuna levo ya pili na baada ya hapo ndio levo ya tatu ambayo hiyo ni safi zaidi na ni nchi chache tu ambazo imefikia mahali hapo.

Feruzi amesema TFDA kufikia levo hiyo imewezesha nchi nyingi Afrika na nje ya Afrika kutumia maabara za  TFDA na watalaam wake katika kufanya uchunguzi na tafiti mbalimbali kwani majibu yanayopatikana hapo yanaweza kutumika kokote duniani.

Pia amesema kwa nchi za Afrika Mashariki, Mamlaka kama TFDA ipo Tanzania tu kwani nchi nyingine nao ndio sasa wameanza mchakato na kwa maana hiyo TFDA imekuwa ikitumika katika kushauri na kutoa maoni yake kwa nchi hizo.

"Nchi za Afrika Mashariki ukiondoa Tanzania hakuna mamlaka ya udhibiti wa ubora na usalama.Kupitia mkutano huu unaondelea jijini Dar es Salaam watalaam wetu na wadau mbalimbali katika eneo hilo watabadilishana uzoefu na kujengana uwezo kati ya nchi moja na nyingine kuhusu udhibiti wa ubora na usalama,"amesema Feruzi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kissa Mwamwitwa akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mkuu Uelimishaji Umm James Ndege baada ya kutembelea banda la TFDA lililopo ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambako kuna mkutano wa wanasayansi unafanyika leo 
Ofisa Mkuu Uelimishaji Umma James Ndege (kushoto) na Ofisa Mwandamizi Uelimishaji Umma Roberta Feruzi (kulia) wote kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) wakifafanua jambo wakiwa kwenye bandao lao la kuelimisha umma lililopo Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.



Hivyo makala TFDA YAJIVUNIA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KATIKA KUDHIBITI UBORA WA DAWA, VIFAA TIBA, VIPODOZI NA VITENDANISHI

yaani makala yote TFDA YAJIVUNIA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KATIKA KUDHIBITI UBORA WA DAWA, VIFAA TIBA, VIPODOZI NA VITENDANISHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TFDA YAJIVUNIA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KATIKA KUDHIBITI UBORA WA DAWA, VIFAA TIBA, VIPODOZI NA VITENDANISHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/tfda-yajivunia-kushika-nafasi-ya-kwanza.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TFDA YAJIVUNIA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KATIKA KUDHIBITI UBORA WA DAWA, VIFAA TIBA, VIPODOZI NA VITENDANISHI"

Post a Comment

Loading...