Loading...

Total Tanzania Yamwaga Mamilioni Kwa Washindi wa Shindano la Ujasiliamali, Serikali Yawapongeza

Loading...
Total Tanzania Yamwaga Mamilioni Kwa Washindi wa Shindano la Ujasiliamali, Serikali Yawapongeza - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Total Tanzania Yamwaga Mamilioni Kwa Washindi wa Shindano la Ujasiliamali, Serikali Yawapongeza, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Total Tanzania Yamwaga Mamilioni Kwa Washindi wa Shindano la Ujasiliamali, Serikali Yawapongeza
link : Total Tanzania Yamwaga Mamilioni Kwa Washindi wa Shindano la Ujasiliamali, Serikali Yawapongeza

soma pia


Total Tanzania Yamwaga Mamilioni Kwa Washindi wa Shindano la Ujasiliamali, Serikali Yawapongeza

.Kampuni ya Mafuta ya Total, Imetoa zawadi za Milioni 65 za Tanzania, kwa Washindi Watatu wa Shindano la Total Staterupper of Year Total Challenge ambapo erikali Yaipongeza Kampuni ya Total Tanzania kwa misaada mbalimbali wanayoitoa kusaidia maendeleo ya jamii ya Tanzania, ikiwemo uwezeshaji wajasiliamali wadogo na wakati, kwa kuwapatia mitaji na mafunzo ya kitaalamu ya ujasiliamali.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Kazi na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, wakati wa hafla ya kuwatangaza washindi wa shindano la Total Starupper of Year, kwa mwaka huu, ambapo washindi watatu wa mwanzo, walipatiwa tuzo na fedha taslim, jumla ya Shilingi milioni 75 za Kitanzania.

Naibu Waziri  Mavunde amesema, anaipongeza sana kampuni ya Total kwa kusaidia vijana wenye mawazo mazuri ya kibiashara, na kuzitaka kampuni nyingine ziige mfano wa Total kwa kujenga uwezo kwa Watanzania, kwa sababu serikali pekee haiwezi kufanya kila kitu peke yake, hivyo kunahitajika juhudi za pamoja kwa kushirikiana na sekta binafsi, katika kuleta maendeleo ya Taifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania, tTarik Moufaddal, amesema, tuzo hizo, ni uthibitisho wa nia ya dhati ya Total, kuwa ni mshirika wa maendeleo wa Tanzania, na kusisitiza kuwa bado kuna mambo mengine mengi makubwa Total imepanga kuwafanyia Watanzania katika kuchangia maendeleo.

Washindi hao nao kwa upande wao, wameishukuru kampuni ya Total kwa kutambua vipaji vyao, na hivyo kuwapatia zawadi watakazozitumia kuboresha miradi yao.

Mshindi wa kwanza ni Doreen Peter Noni, amepata tuzo na zawadi ya fedha taslim Shilingi Milioni 30 za Tanzania kwa wazo la uanzishaji kipindi cha TV kinachoitwa Peter’s Daughter Show Project, kwa lengo la kusaidia vijana kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo, ikiwemo tatizo kubwa la msongo wa mawazo, kwa vijana walioshindwa kufanikiwa.

Mshindi wa pili ni Michael Sayi, aliyepata tuzo na fedha taslimu Shilingi milioni 20, kwa mradi wa Kasome International Project, unaowasaidia wanafunzi wa sekondari Tanzania, kujipatia vitabu na masomo ya ziada kupitia mtandao, hivyo kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi kutoka familia masikini, kupata mafunzo bora kwa gharama ndogo.

Mshindi wa Tatu ni  Prince Tillya aliyepata Tuzo na fedha taslim Shingi milioni 15 kwa mradi wake wa FixChap Project, unaounganisha mafundi bora wa huduma mbalimbali za majumbani kwa gharama nafuu. 

Shindano la « Startupper of the year by Total » ni juhudi za Kampuni ya Total ya kimataifa kuhamasisha  maendeleo yakiuchumi na kijamii ili  kusaidia nchi zote  duniani ambako kampuni ya Total ipo. Shindano hili ni hatua madhubuti sanayenye lengo la kusisimua ubunifu wa  miradi ya maendelea yenye lengo la kuchangia uanzishwaji wa viwanda vidogo vitakavyotoa ajira na kuchangia maendeleo ya jamii na ya nchi za bara la Afrika kwa ujumla. Shindano hii linalenga kuibuka kwa miradi mipya, iliyotokana na wananchi wenyewe ambayo inaendena na malengo ya jumla ya uwepo wa kampuni yaTotal 

 Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za  kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total Katika kujitanua kibiashara kuelekea kwenye matumizi ya nishati mbadala, kampuni ya Total Tanzania Limited kupitia mradi wake wa Total Access to Solar (TATS) project, inasambaza taa za nishati jua zinazoitwa  AWANGO kwa jamii ya Watanzania. end.
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde (Mb), (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania, Tarik Moufaddal (Kushoto) wakikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge”Doreen Peter Noni aliyejinyakuwa Milioni 30,  katika hafla fupi iliyofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde (Mb), (Kulia) akikabidhi cheti kwamshindi wa kwanza wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge” Doreen Peter Noni aliyejinyakuwa Milioni 30,  katika hafla fupi iliyofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde (Mb), (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania, Tarik Moufaddal (Kushoto) wakikabidhi zawadi ya hundi ya Shilingi Milioni 15, kwa Mshindi wa Tatu wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge”  Prince Tillya wakati wa hafla fupi iliyofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde (Mb), (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania, Tarik Moufaddal (Kushoto) wakikabidhi zawadi ya hundi ya Shilingi Milioni 20, kwa Mshindi wa Pili wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge”  Michael Sayi wakati wa hafla fupi iliyofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam.
Washindi watatu wa shindano la wajasiriamali kwa vijana la Total, “Startupper of The Year by Total Challenge”  katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa zawadi zao katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam juzi. Mshindi wa Kwanza, Doreen Peter Noni (katikati) aliyenyakuwa Milioni 30, Kulia kwake ni Mshindi wa Tatu Prince Tillya alipata Milioni 15 na Kushoto ni Mshindi wa Pili, Michael Sayi aliyepata Milioni 20.
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde (Mb), Kushoto,  akimpongezazawadi ya hundi ya Shilingi Milioni 20, kwa Mshindi wa Kwanza wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge”  Doreen Peter Noni (katikati) aliyeshinda Milioni 30. wakati wa hafla fupi iliyofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam. Kulia ni  Mshindi wa Tatu Prince Tillya aliyepata Milioni 15.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania,  Tarik Moufaddal (Kushoto) akihutubia katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge”  katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam jana. Kutoka Kushoto ni mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Mh. Anthony Mavunde (Mb), Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mshindi wa Kwanza, Doreen Peter Noni aliyenyakuwa Milioni 30, Mshindi wa Tatu Prince Tillya alipata Milioni 15 na Mshindi wa Pili, Michael Sayi aliyepata Milioni 20.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania, Tarik Moufaddal (Kushoto), Mh. Anthony Mavunde (Mb), Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mshindi wa Kwanza, Doreen Peter Noni aliyenyakuwa Milioni 30, Mshindi wa Tatu Prince Tillya alipata Milioni 15 na Mshindi wa Pili, Michael Sayi aliyepata Milioni 20, wakinyanyua glasi kutakiana heri, katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge”  katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam jana


Hivyo makala Total Tanzania Yamwaga Mamilioni Kwa Washindi wa Shindano la Ujasiliamali, Serikali Yawapongeza

yaani makala yote Total Tanzania Yamwaga Mamilioni Kwa Washindi wa Shindano la Ujasiliamali, Serikali Yawapongeza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Total Tanzania Yamwaga Mamilioni Kwa Washindi wa Shindano la Ujasiliamali, Serikali Yawapongeza mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/total-tanzania-yamwaga-mamilioni-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Total Tanzania Yamwaga Mamilioni Kwa Washindi wa Shindano la Ujasiliamali, Serikali Yawapongeza"

Post a Comment

Loading...