Loading...

UJUMBE WA JOSEPH KUSAGA KWENYE MAZIKO YA KIBONDE WAIBUA HISIA NZITO ,WAACHA TAFAKARI KWA WAOMBOLEZAJI

Loading...
UJUMBE WA JOSEPH KUSAGA KWENYE MAZIKO YA KIBONDE WAIBUA HISIA NZITO ,WAACHA TAFAKARI KWA WAOMBOLEZAJI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UJUMBE WA JOSEPH KUSAGA KWENYE MAZIKO YA KIBONDE WAIBUA HISIA NZITO ,WAACHA TAFAKARI KWA WAOMBOLEZAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UJUMBE WA JOSEPH KUSAGA KWENYE MAZIKO YA KIBONDE WAIBUA HISIA NZITO ,WAACHA TAFAKARI KWA WAOMBOLEZAJI
link : UJUMBE WA JOSEPH KUSAGA KWENYE MAZIKO YA KIBONDE WAIBUA HISIA NZITO ,WAACHA TAFAKARI KWA WAOMBOLEZAJI

soma pia


UJUMBE WA JOSEPH KUSAGA KWENYE MAZIKO YA KIBONDE WAIBUA HISIA NZITO ,WAACHA TAFAKARI KWA WAOMBOLEZAJI

*Azungumza maneno mazito, asema kifo cha Kibonde kimemuachia funzo kuwa umaarufu,fedha havina nafasi

*Asema kama umaarufu basi Kibonde alikuwa maarufu kuliko msanii yoyote lakini bado alikuwa mnyenyekevu


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWILI wa aliyekuwa Mtangazaji maarufu nchini marehemu Ephraim Kibonde umepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam huku ujumbe mzito uliotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group ukigusa mioyo ya waombolezaji.

Wakati wa kuupumzisha mwili wa Kibonde mamia ya waombolezaji wakiwamo viongozi wa ngazi mbalimbali, familia,ndugu,jamaa na marafiki wameshiriki kwenye maziko hayo.Huzuni ilikuwa imetawala wakati wote wa maziko.

Mwili wa Kibonde ulianza kushushwa kaburini saa saa 10:02 Alasiri ya leo Machi 9,2019 baada ya kutolewa neno la faraja ambapo pamoja na kuelezea majonzi ya msiba huo waombolezaji waambiwa kifo ni adui na sio mpango wa Mungu.

SALAM ZA FAMILIA

Baada ya mwili wake kuwekwa kaburini,Msemaji wa familia ya Kibonde kupitia Frank Chagula imetoa shukrani kwa waombolezaj wote ,viongozi wa Serikali huku ikielezewa miongoni kwa walioguswa na msiba huo ni Rais Dk.John Magufuli ambaye kutokana na majukumu aliyonayo amemwagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumuwakilisha.

Chagula amesema wanatoa shukrani kwa kila mtu ambaye ameshiriki kwenye mazishi na maziko ya marehemu Kibonde."Kwa umati huu ambao umejitokeza nyumbani na hapa makaburini familia tunatoa shukrani kwa wote,ukweli kutaja jina la kila mtu mmoja hatutaweza ,hivyo tunatoa shukrani kwa wote."

Baada ya familia kutoa shukrani ikafuata hatua ya kufukia kaburini. Wakati kaburini lenye mwili wa Kibonde linafukiwa kimya kilikuwa kimetawala makaburini hapo kulikuwa na umati mkubwa watu.


ALICHOSEMA RAFIKI WA KIBONDE 

Wakati huo huo salamu za Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi Garda G Habashi amemueleze Kibonde enzi za uhai wake alivyoingia kwenye utangazaji na safari yake ilianza ya utangazaji mwaka 1990 baada ya kupata kazi kituo cha CTN na baadae mwaka 1999 alijiunga Clouds Media Group.

Aliingia Clouds Media Group baada ya kuanzisha kipindi cha michezo na burudani. Uwepo wa Clouds Media Group alionesha umahiri mkubwa Garza alimuomba wawe wote kwenye kipindi cha Jahazi.

"Kibonde alikuwa pacha wangu kabla ya kazi na baada ya kazi.Hata kwenye mambo ya familia walishirikiana.Na hata katika mambo ya starehe kwa kweli tulifanya starehe zetu vizuri,niamini mimi.

"Kibonde leo huyo ametangulia ,sipo naye tena. Sitalia kwasababu nikilia nitamsikitisha,nikilia naye atalia na wote tutalia wakati wote," amesema Garda G Habashi na kuongeza ucheshi wa Kibonde alionesha kwa kila mtu kwani hata wakiwa wanaongoza alikuwa anamuacha nyuma kutokana na kupenda kusalimia kila tena kwa kumshika mkono.

Hata hivyo amesema kuwa ni wiki iliyopita wamempoteza Mkurugenzi wao wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba na sasa Kibonde lakini ametoa ahadi ya kwamba wafanyakazi pamoja na kuondokewa na wapendwa wao watafanya kazi ili hata huko waliko wafarijike.

UJUMBE MZITO WA KUSAGA 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amesema ni pigo kubwa kwa Clouds Media Group kwani ndani ya wiki mmoja wameondokewa na watu muhimu.

"Machozi niliyonayo moyoni yatachelewa kukauka , ni pigo kubwa sana kwetu.Hata hivyo nitoe shukrani kwa Rais Dk.John Magufuli kwani baada ya taarifa kifo cha Kibonde alinipigia simu ya kunipa pole," amesema Kusaga.

Hata hivyo amesema kwamba kifo cha Kibonde ambaye baada ya kupata matatizo lakini baada ya kupata huduma za matibabu alipata nafuu lakini baadae akafariki.

"Fundisho ambalo nimelipata baada ya kifo cha Kibonde ni kwamba tuache nyodo,Kibonde alikuwa maarufu kuliko wasanii wowote lakini ameondoka,kama fedha zinaokoa maisha tungeweza kumuokoa kutokana na jitihada.Tuache nyodo kwani duniani tunapita tu.

" Umaarufu na fedha sio chochote mbele ya kifo,Kibonde nenda tunakuaga,tunajua utakutana na mzee Kusaga ambaye alikupenda sana,utakutana na Ruge ambaye mlishirikia naye kikamilifu .Nenda Kibonde ,uliniheshimu nami nilikiluheshimu sana.

"Niombe kila mmoja wetu hapa atambue anayo fursa ya kuonesha upendo kwa kila mtu,onesha upendo kadri unavyoweza.Hapa duniani tunapita tu.Tushikane mikoni kuonesha ishara ya kusameehana na kuanza upya," amesema Kusaga.

Hata hivyo baada ya Kusaga kutoa ujumbe mzito ambapo ulisababisha watu kushindwa kuvumilia na kuwafanya wapige makofi kumppngeza ilifuata hatua ya kuweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu Ephraim Kibonde.
Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akizungumza jamo wakati wa Mazishi wa Mtangazaji wa kituo hicho cha redio,Marehemu Ephraim Kibonde

Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Media Reginald Mengi akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Joseph Kusaga wakati wa mazishi ya Ephraim Kibonde,leo makaburi ya Kinondoni jijini Dar
Rafiki na Myanyakazi mwenzake Marehemu,Gadna G Habash akiwa na majonzi makubwa kufuatia msiba wa Ephraim Kibonde ,wa pili kati ni Mtoto wa Marehemu.
Wazazi wa Marehemu wakihuzunika kuondokewa na mtoto wao mpendwa
Sanduku lenye mwili wa maerehemu Ephraim Kibonde ukiwasili katika makaburi ya Kinondoni jioni ya leo kwa maziko
Watoto wa Marehemu wakiweka udongo kwenye kaburi la Baba yao



Hivyo makala UJUMBE WA JOSEPH KUSAGA KWENYE MAZIKO YA KIBONDE WAIBUA HISIA NZITO ,WAACHA TAFAKARI KWA WAOMBOLEZAJI

yaani makala yote UJUMBE WA JOSEPH KUSAGA KWENYE MAZIKO YA KIBONDE WAIBUA HISIA NZITO ,WAACHA TAFAKARI KWA WAOMBOLEZAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UJUMBE WA JOSEPH KUSAGA KWENYE MAZIKO YA KIBONDE WAIBUA HISIA NZITO ,WAACHA TAFAKARI KWA WAOMBOLEZAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/ujumbe-wa-joseph-kusaga-kwenye-maziko.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UJUMBE WA JOSEPH KUSAGA KWENYE MAZIKO YA KIBONDE WAIBUA HISIA NZITO ,WAACHA TAFAKARI KWA WAOMBOLEZAJI"

Post a Comment

Loading...