Loading...
title : UKIWA UNAONGEA UNACHOANDIKA NA UNA MWANDIKO MBAYA SOMA HAPA
link : UKIWA UNAONGEA UNACHOANDIKA NA UNA MWANDIKO MBAYA SOMA HAPA
UKIWA UNAONGEA UNACHOANDIKA NA UNA MWANDIKO MBAYA SOMA HAPA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
BAADHI ya watu wana matatizo au hali za chini katika kuelewa lugha hasa katika maandishi na kuongea, wataalamu wengi wamefanya tafiti nyingi ya kutambua matatizo hayo likiwemo la Disigrafia.
Imeelezwa kuwa disgrafia ni tatizo linalompata mtu ambapo hushindwa kuandika na kuelewa maandishi na michoro, mtu mwenye tatizo hili hushindwa kuumba herufi na anakuwa na mwandiko mbaya. Aidha mtu mwenye disigrafia hushindwa kuwasilisha mantiki katika karatasi.
Watu wengi huwa na matatizo katika kuandika ila disigrafia ni zaidi ya hapo kwani tatizo hilo hugusa mifumo ya fahamu na hujitokeza wakati mtoto anapoanza kujifunza kuandika, mfano: katika daftari lenye mistari anaweza kuandika sentensi moja katika mistari minne huku akichanganya herufi kubwa na ndogo na zenye ukubwa tofauti tofauti.
Tatizo hili humfanya mtu kushindwa kubadili sauti za lugha kuwa herufi za maandishi, kushindwa kutambua herufi au kuandika kinyume mfano: d kuwa b au z kuwa 3.
Dalili za mtu mwenye tatizo hili ni pamoja na; kugeuza herufi, maandishi yasiyolingana ukubwa, kuchanganya herufi na namba na kuchanganya herufi kubwa na ndogo.
Pia mwenye tatizo hili anaweza kuandika maneno yasiyokamili mfano; Mama anapk, kushika vibaya viandikio kama kalamu na peni. Aidha mtu mwenye tatizo hili huandika mwili ukiwa unacheza, kuzungumza kila anachoandika na kupata ugumu wa kuunganisha mawazo.
Na inasemekana kuwa watu wenye tatizo hili huzungumza vizuri kuliko kuandika.
Hivyo makala UKIWA UNAONGEA UNACHOANDIKA NA UNA MWANDIKO MBAYA SOMA HAPA
yaani makala yote UKIWA UNAONGEA UNACHOANDIKA NA UNA MWANDIKO MBAYA SOMA HAPA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UKIWA UNAONGEA UNACHOANDIKA NA UNA MWANDIKO MBAYA SOMA HAPA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/ukiwa-unaongea-unachoandika-na-una.html
0 Response to "UKIWA UNAONGEA UNACHOANDIKA NA UNA MWANDIKO MBAYA SOMA HAPA"
Post a Comment