Loading...
title : VISA, MABENKI 15 WAZINDUA HUDUMA YA VISA KWENYE SIMU YA MKONONI JIJINI DAR
link : VISA, MABENKI 15 WAZINDUA HUDUMA YA VISA KWENYE SIMU YA MKONONI JIJINI DAR
VISA, MABENKI 15 WAZINDUA HUDUMA YA VISA KWENYE SIMU YA MKONONI JIJINI DAR
Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya Visa kwenye simu za mkononi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi wa huduma ya Visa kwenye simu za mkononi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais wa Kampuni ya VISA kwa Sab-Sahara Afrika Aida Diara akizungumza katika katika uzinduzi wa huduma ya Visa kwenye simu za mkononi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amesema lengo la kuzinduwa huduma hiyo ni kuhamasisha uboreshaji huduma na kupunguza makato kwa wateja, wafanyabiashara na sekta ya huduma ya fedha kwa ujumla.
Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Mauzo ya Biashara Kennedy Luhombo akitoa ufafanuzi juu ya huduma ya VISA inavyofanya kazi katika simu za mkononi katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
*BoT yasema Tanzania imepiga hatua kuongeza malipo ya kieletroniki *Yaelezwa Watanzania milioni 20 wana usajili au akaunti za fedha kwenye simu Na Said Mwishehe, Globu ya jamii. VISA na benki 15 nchini Tanzania wamezindua huduma ya kwanza ya malipo ya simu bure ambapo sasa wateja wanaofanya miamala watakuwa na uwezo wa kutuma au kupokea fedha ndani na nje ya nchi bila makato yoyote.
Akizungumza leo Machi 12, 2019 jijini Dar es Salaam, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Bernad Kibese amesema uzinduzi huo wa VISA kwenye simu ya mkononi ni hatua nzuri na Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuongeza malipo ya kieletroniki na kukuza ushirikishwaji wa fedha. "Uzinduzi wa Visa kwa njia ya simu ya mkononi unaonesha hatua muhimu katika kuongeza kasi ya uhamaji kutoka fedha taslimu kwenda mfumo wa uchumi wa kidigitali Tanzania ambao ni mzuri kwa jamii zetu,"amesema Dk. Kibese.
Kwa upande wake Rais wa Kampuni ya VISA kwa Sab-Sahara Afrika Aida Diara amesema lengo la kuzinduliwa kwa huduma hiyo ni kuhamasisha uboreshaji huduma na kupunguza makato kwa wateja, wafanyabiashara na sekta ya huduma ya fedha kwa ujumla. Amesema ili kutumia huduma hiyo , Diara amesema mteja wa benki anatakiwa kupakua programu ya simu ya benki husika, kisha atatafuta Visa kwenye programu na lipia bidhaa na huduma ama kwa kupiga picha alama ya QR au kwa kutumia USSD (Unstructed Supplimentary Service Data)katika sehemu ya biashara ulipo.
Huduma hiyo ni ya Visa na inapatikana bure na salama. "Matumizi ya malipo ya kieletroniki yanaongeza usalama na urahisi barani Afrika huku ikipunguza gharama na kuongeza uwazi katika shughuli za kifedha.Sehemu kubwa ya uchumi wa Afrika na usio rasmi, malipo hufanyika kwa kubadilishana fedha taslimu kwa zaidi ya asilimia 90.
"Inatia moyo kuona Watanzania tayari wanafuata na kukubali teknolojia ya simu ikiwa na usajili wa watu zaidi ya milioni 41 na zaidi ya asilimia 80 ya waliosajiliwa hutumia mtandao kwa kutumia simu za mkononi.Ni ukweli unaofahamika kuwa zaidi ya Watanzania milioni 20 wana usajili au akaunti za fedha kwenye simu.Hizi zote ni ishara za matumaini kwa VISA,"amesema.
Diara amesisitiza lengo la uzinduzi wa Visa kwa njia ya simu nchini Tanzania, lina msingi imara na kwamba wafanyabiashara watafurahia na kuthamini utamaduni huo mpya kabisa wa malipo ya fedha taslimu wa kulipa au kulipwa. Ameongeza kuwa uhamaji wa kutoa fedha taslimu kwenda kidigitali unapanua wigo wa juu na chini wa thamani .
Kwa mteja huduma za fedha za simu zinaleta usalama,urahisi, mazingira mazuri ya malipo kuliko fedha taslimu na inaokoa muda na gharama za safari. Kuhusu malengo yao kwa upande wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Diara amesema wameendelea kukuza mipango yao, biashara na teknolojia katika ukanda huo kwa kufungua mtandao wao kuunga mkono mahitaji ya taasisi za fedha, wauzaji , waendelezaji na washirika wa FinTech ili kujenga mazingira jumuishi ya kimazingira.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley amesema kulingana na jarida la TanzaniaInvest , eneo la biashara ya simu nchini Tanzania inashuhudia ukuaji wa haraka unaofikia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 1.6 zilizofanyika kila mwezi mwaka 2018. Amezitaja baadhi ya benki ambazo zimeshirikiana na VISA kutoa huduma hiyo ni CRDB, NMB, NBC, benki ya Azania, TIB , benki ya Posta, DCB, benki ya Mkombozi, Mufindi Community Bank Limited, Benki ya Watu wa Zanzibar , Benki ya Uchumi,Benki ya Mwalimu,Benki ya Maendeleo na Yetu Microfinance Bank.
Hivyo makala VISA, MABENKI 15 WAZINDUA HUDUMA YA VISA KWENYE SIMU YA MKONONI JIJINI DAR
yaani makala yote VISA, MABENKI 15 WAZINDUA HUDUMA YA VISA KWENYE SIMU YA MKONONI JIJINI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VISA, MABENKI 15 WAZINDUA HUDUMA YA VISA KWENYE SIMU YA MKONONI JIJINI DAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/visa-mabenki-15-wazindua-huduma-ya-visa.html
0 Response to "VISA, MABENKI 15 WAZINDUA HUDUMA YA VISA KWENYE SIMU YA MKONONI JIJINI DAR"
Post a Comment