Loading...
title : WAFANYAKAZI WAKALA WA UCHIMBAJI VISIMA NA UJENZI WA MABWAWA(DDCA) WAHAKIKISHIWA AJIRA ZAO ZIKO SALAMA
link : WAFANYAKAZI WAKALA WA UCHIMBAJI VISIMA NA UJENZI WA MABWAWA(DDCA) WAHAKIKISHIWA AJIRA ZAO ZIKO SALAMA
WAFANYAKAZI WAKALA WA UCHIMBAJI VISIMA NA UJENZI WA MABWAWA(DDCA) WAHAKIKISHIWA AJIRA ZAO ZIKO SALAMA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo amewataka wafanyakazi wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA)kuendelea na majukumu yao kama kawaida na wasiwe na wasiwasi na ajira zao kwani wako salama.
Profesa Mkumbo ametoa kauli hiyo katika Ofisi za DDCA jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na wafanyakazi kuhusu mabadiliko makubwa ya kiuundo ambayo yamefanyika ndani ya Wizara yao na sekta ya maji kwa ujumla.
Ametumia nafasi hiyo kuelezea uwepo wa Sheria Mpya ya Huduma za Maji ambayo imepitishwa siku za karibuni ambapo kupitia sheria hiyo imeundwa rasmi Wakala wa Maji Vijijini(RUWASA), hivyo DDCA imekufa kifo cha kawaida huku akiwahakikishia wafanyakazi kuwa ajira zao ziko salama waendelee kuchapa kazi.
Akifafanua zaidi kuhusu mabadiliko ndani ya Wizara ya Maji, Profesa Mkumbo amesema "Kuna mabadiliko makubwa sana yanaendelea katika sekta ya maji. Ni vema Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa mkafahamu nafasi yenu kutokana na mabadiliko haya.
"Kuna mabadiliko yamefanyika wizarani lakini ninyi Wakala wa visima hayajawawagusa.Kuna sheria mpya ya maji ambayo imekuja na Wakala wa Maji Vijijini ambayo hiyo sasa ndio inachukua jukumu la halmashauri katika utoaji wa huduma za maji.
"Tunakumbuka ilitolewa sera, hivyo Januari 31,2019 wabunge walipitisha sheria ya huduma za maji na mazingira ambayo kwa sasa inasubiriwa kusainiwa na Rais ili ianze kutumika. Hivyo DDCA inaondoka maana tayari kuna wakala wa maji vijijini ambayo itameza taasisi nyingine, ikiwemo hii ya kwenu ambayo inakufa kifo cha kawaida,"amesema Profesa Mkumbo.
Hata hivyo amesema hakuna ambaye ataondolewa kazini kwasababu ya kuwepo kwa mabadiliko hayo kwani wamezingatia ajira ya kila mmoja.
"Baada ya kupita sheria hii utaratibu ni kwamba iwapo kuna wakurugenzi wawili mmoja ilikuwa lazima aondoke.Lakini hapa DDCA Mkurugenzi wenu alikuwa anakaimu, hivyo hakuna wakurugenzi wawili.
"Kwa lugha rahisi Mkurugenzi wenu alikuwa ana -Act na kiswahili ni kuigiza, hivyo akiwambia acha kuigiza kuna tatizo gani?Ujio wa sheria ya Huduma za Maji kinachobadilika hapa kwenu ni jina tu.Hivyo DDCA itakuwa ndani ya RUWASA na kikubwa ambacho tunasisitiza ni kushirikiana kikamilifu ili kufikia lengo la Serikali kupitia sheria ya Maji,"amefafanua.
Kutokana na mabadiliko hayo wamesimamisha mchakato wa kupata wajumbe wa bodi, na hilo si tatizo kwani Serikali inayo mfumo na muundo mzuri wa kufanya kazi zake hata kama bodi itakuwa bado haijapatikana.
Profesa Mkumbo amewahakikishia wafanyakazi wa DDCA kuwa mabadiliko hayo yanatoa fursa nyingi zikiwemo za nafasi za ajira ambazo zitatangazwa kwa ajili ya RUWASA na watakaopewa kipaumbele ni wale walipo ndani ya Wakala hiyo.
"Kuna fursa nyingi zimefunguliwa, kuna nafasi zinatajiwa kujazwa na ni nyinyi, huu ndio wakati wenu kuzichangamkia.Mtakaoomba tutawashindanisha na kisha tutawapata wenye sifa zinazohitajika.
Amesema wafanyakazi wa DDCA ndio wababe katika uchimbaji visima na mabwawa vijijini. "Katika uchimbaji visima na mabwawa ninyi ndio washauri wakuu wa Serikali lakini bado hawajatumika vizuri na sasa ndio wakati wake".
Amewashauri DDCA kupanga malengo sahihi na mkakati wa Serikali ni kuona wakala hao wanajitegemea kwa asilimia 100 na hatimaye kuwa na Kampuni inayojiendesha kwa faida inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100.
"Tunataka kuona mnajiendesha kwa fedha zenu wenyewe, hivyo hata Mkurugenzi wa RUWASA atapewa malengo ya kuwahakikisha anawalea maana tunajua uwezo wenu katika kuchimba visima na ujenzi wa mabwawa.Akitoa Mkurugenzi mjinga wa RUWASA ataona kama vile huu Wakala ni mshindani wake wakati si kweli.Mkurugenzi wa RUWASA atakayekuja lazima ailee,"amesisitiza.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na viongozi pamoja na wafanyakazi wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa(DDCA),jijini Dar es Salaam kuhusu mabadiliko mbalimbali yanayoendelea ndani ya Wizara na sekta ya maji kwa ujumla nchini
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) wakimsililiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Process Kitila Mkumbo baada ya kukutana nao kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya Maji
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa Domina Msonge(katikati).
Wafanyakazi wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa wakifuatilia mkutano ambao mgeni rasmi ambaye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prodesa Kitila Mkumbo
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo ( aliyevaa shati nyeupe) akizungumza na viongozi pamoja na Wafanyakazi was Wakaja wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa
Hivyo makala WAFANYAKAZI WAKALA WA UCHIMBAJI VISIMA NA UJENZI WA MABWAWA(DDCA) WAHAKIKISHIWA AJIRA ZAO ZIKO SALAMA
yaani makala yote WAFANYAKAZI WAKALA WA UCHIMBAJI VISIMA NA UJENZI WA MABWAWA(DDCA) WAHAKIKISHIWA AJIRA ZAO ZIKO SALAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAFANYAKAZI WAKALA WA UCHIMBAJI VISIMA NA UJENZI WA MABWAWA(DDCA) WAHAKIKISHIWA AJIRA ZAO ZIKO SALAMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/wafanyakazi-wakala-wa-uchimbaji-visima.html
0 Response to "WAFANYAKAZI WAKALA WA UCHIMBAJI VISIMA NA UJENZI WA MABWAWA(DDCA) WAHAKIKISHIWA AJIRA ZAO ZIKO SALAMA"
Post a Comment