Loading...
title : WALIOKUWA WAFANYAKAZI BANDARI KAVU WATUPWA JELA KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA BILIONI 12.7
link : WALIOKUWA WAFANYAKAZI BANDARI KAVU WATUPWA JELA KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA BILIONI 12.7
WALIOKUWA WAFANYAKAZI BANDARI KAVU WATUPWA JELA KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA BILIONI 12.7
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MAHAKAMA Kuu divisheni ya Rushwa na uhujumu uchumi imewahakumu wafanyakazi wawili wa zamani wa bandari kavu ya Azam ICD kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya kughushi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bil.12.7 na kuachiwa kwa makosa ya kutakatisha fedha na kukwepa kodi.
Pia mahakama imemuhukumu Benson Malembo mfanyakazi wa Region Cargo Service kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kukutwa na hatia ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya sh. Bilioni 12.
Aidha Mahakama imewaamuru washtakiwa hao mara baada ya kumaliza kifungo chao kulipa fidia ya sh. Bilioni 6.35 ambayo ni nusu ya fedha waliyoisababishia taasisi hasara, bilioni 12.7.
Mbali na Malembo, washtakiwa waliotiwa hatiani na kusomewa Hukumu yao leo Machi 28.2019 na Jaji Winifrida. Korosso ni Raymond Adolf Louis ambaye ni Meneja wa oparesheni za usalama, Khalid Yusufu Louis.
Washtakiwa hao wamesomewa hukumu yao leo baada ya Machi 25.2019 (jumatatu) mahakama hiyo kuwakuta na hatia.
Katika kesi hiyo, washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 110 yakiwemo ya kula njama, utakatishaji wa fedha na kukwepa kodi.
Akisoma adhabu hiyo, Jaji Koroso amesema, katika shtaka la 2 hadi la 106 ambayo ni ya kughushi, washtakiwa Raymond na Khalid wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani katika kila shtaka huku katika shtaka la kusababisha hasara washtakiwa wote wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani.
Upande wa mashtaka uliita jumla ya mashahidi 34 mahakamani hapo kutoa ushahidi wao ambapo Jaji Korosso amesema kupitia ushahidi huo, upande wa mashtaka umethibitisha kesi dhidi ya washtakiwa hao.
Hata hivyo, mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka hayo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.
Washtakiwa walioachiwa ni, Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA, Hamis Omary, Haroun Mpande wa kitengo cha mawasiliano na kompyuta ICT TRA
Jaji Korosso amesema amepitia maelezo ya upande wa mashtaka na yale ya washtakiwa pamoja na mawakili wa utetezi ambapo wamedai washtakiwa ni wakosaji wa kwanza na kwamba wanafamilia zinazowategemea kwani wote wana wake na watoto ambao wanawategemea.
Jaji Korosso amesema, amezingatia maombi yote ya washtakiwa kuwa wanajutia makosa yao na pia mshtakiwa Raymond na Khalid wameiomba mahakama iangalie kipindi cha zaidi ya miaka mitatu walichokaa gerezani. Aidha katika utetezi wao waliiomba mahakama kuzingatia kuwa katika kipindi chote wakiwa waajiriwa wa Azam hakukuwahi kutokea upotevu wowote na mara zote walikiwa wakionyesha nidhamu na kufika mahakani bila kukosa.
Washtakiwa Raymond na Khalid wanadaiwa kutoa makontena kwenye Bandari kavu ya Azam ICD iliyopo maeneo Sokota na kujaribu kuonesha yalitolewa kihalali na TRA Dar es Salaam.
Kwa upande wa washtakiwa
Pia wanadaiwa walisababisha hasara ya Sh 12, 618,970,229 kwa kutoa makontena 329 bila ya kulipia ushuru na malipo mengine.
Watuhumiwa Raymond Adolf Louis wa kwanza kushoto mwenye shati Jeupe, Khalid Yusufu Louis wa kati kati na Benson wakiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama kuu devisheni ya rushwa na uhujumu uchumi, wakisuburi kusomewa hukumu yao baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya uhujumu uchumi kwenye makosa ya kughushi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bil. 12.7
Wshtakiwa hao wakijadiliana jambo na mawakili wao baada ya Jaji Winfrida Korosso kuwasomea hukumu yao ambapo Raymond mwenye shati jeupe na Khalid shati la bluu wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani hukumu Mulembo kushoto akihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani.
Hivyo makala WALIOKUWA WAFANYAKAZI BANDARI KAVU WATUPWA JELA KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA BILIONI 12.7
yaani makala yote WALIOKUWA WAFANYAKAZI BANDARI KAVU WATUPWA JELA KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA BILIONI 12.7 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WALIOKUWA WAFANYAKAZI BANDARI KAVU WATUPWA JELA KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA BILIONI 12.7 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/waliokuwa-wafanyakazi-bandari-kavu.html
0 Response to "WALIOKUWA WAFANYAKAZI BANDARI KAVU WATUPWA JELA KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA BILIONI 12.7"
Post a Comment