Loading...
title : Wanawake soko la Feri na maeneo jirani waishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
link : Wanawake soko la Feri na maeneo jirani waishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Wanawake soko la Feri na maeneo jirani waishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Na Mwandishi Maalum
Wanawake wa soko la Feri pamoja na maeneo jirani wameishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kufanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo pamoja na kutoa elimu ya magonjwa hayo.
Upimaji huo umefanywa leo na wafanyakazi wanawake wa Taasisi hiyo ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kitaifa yatafanyika kesho.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wanawake hao walisema muda mwingi wamekuwa wakiutumia katika biashara na kutunza familia zao na hivyo kukosa nafasi ya kwenda kupima afya zao.
Akiongea na mwandishi wa habari hizi Ashura Omari ambaye ni mfanyabiashara wa chakula katika soko hilo alisema wamefarijika sana kuona wataalamu wa magonjwa ya moyo wamewafuata katika soko la Feri la kuwapa huduma ya upimaji pamoja na kutoa elimu.
“Tunashukuru sana kwa kupimwa afya zetu, nimepimwa urefu, uzito, wingi wa sukari na msukumo wa damu mwilini (BP). Tunaiomba Taasisi hii na Serikali kwa ujumla waweze kutoa huduma kama hii katika maeneo mengi zaidi”, alisema Ashura.Naye Mariam Mohamed ambaye ni mkazi wa Kinondoni alisema amefika katika soko hilo la feri kupata huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake.
Mariam alisema amepata elimu ya jinsi ya kuandaa chakula bora kwa familia, kutotumia chumvi nyingi na mafuta mengi katika chakula, pia anapoandaa chakula ni ahakikishe familia ile chakula chenye mboga za majani na matunda.
“Pia nimeambiwa unywaji wa pombe uliokithiri pamoja na kutokufanya mazoezi ni vitu ambavyo vinapelekea kupata magonjwa ya moyo nitajitahidi mimi na familia yangu kufuata haya yote niliyofundishwa leo”, alisema Mariam.
Akitoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa wanawake waliohudhuria upimaji huo Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hildegard Karau alisema mtindo wa maisha unapelekea watu wengi kupata magonjwa ya moyo ikiwemo shinikizo la damu na kuwataka wanawake hao pamoja na familia zao kufanya mazoezi.
“Wanawake ni watu wa muhimu sana katika familia kama mtazingatia mafunzo mliyopewa leo na kuandaa vyakula bora katika familia zenu itawasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda familia familia zao”, alisema Hildegard.
Wakati huo huo wanaume wa soko la Feri waliiomba Taasisi hiyo wakati mwingine watakapoandaa upimaji kama huo wasiwasahau wanaume kwani nao muda mwingi wanahangaika kutafuta fedha za kutunza familia na kukosa muda wa kwenda kupima afya zao.
Mzee Husein Mbaraka alisema, “Katika soko hili kuna watu wengi wanaofanya kazi mbalimbali wakiwemo wavuvi ambao muda mwingi wanashinda Baharini , tunaiomba Taasisi hii siku nyingine waje kutupima na sisi magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na kutupa elimu.
Hivyo makala Wanawake soko la Feri na maeneo jirani waishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
yaani makala yote Wanawake soko la Feri na maeneo jirani waishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wanawake soko la Feri na maeneo jirani waishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/wanawake-soko-la-feri-na-maeneo-jirani.html
0 Response to "Wanawake soko la Feri na maeneo jirani waishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)"
Post a Comment