Loading...
title : Wanawake VETA Chang’ombe watoa msaada Kambi ya Nunge
link : Wanawake VETA Chang’ombe watoa msaada Kambi ya Nunge
Wanawake VETA Chang’ombe watoa msaada Kambi ya Nunge
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
CHUO cha VETA Chang’ombe kimetoa msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni Moja katika Kambi ya Wazee Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Msaada huo umetokana na mchango wa Wanawake wa chuo hicho katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila Machi 8 ya kila mwaka.
Akizungumza na Wazee wa Kambi ya Nunge Kaimu Msajili wa Chuo cha VETA Chang’ombe Clara Kibodya amesema kuwa wanawake wamekuwa na mwitikio katika kambi ya Nunge na hivyo kuamua kutoa mchango wao kwa jamii inayoishi hapo.
Amesema kuwa Kambi hiyo inahitaji msaada, na kutaka wadau na mtu mmoja moja kuona kuna umuhimu wa kutoa msaada kwani serikali pekee yake haiwezi kutosheleza.
“Tumefika na kujionea hali ya wazee na kuamini wanauhitaji wa msaada na tumevutiwa kama wanawake ndio wasimamizi wa familia hatuwezi tukawaacha wazee hao kwani ni baba zetu na babu zetu katika mila na tamaduni za Afrika”.amesema Kibodya.
Nae Katibu Mukhtasi wa Chuo hicho Bena Maimu amesema katika kuadhimisha siku wanawake duniani Kambi ya Nunge imewagusa na kutaka kuwa na utaratibu wa kuwatembelea mara kwa mara na kujua changamoto zao ili wazee wasione jamii imewatupa.
Kwa upende wa Afisa Kilimo na Msimamizi wa Kambi ya Nunge Frank Munuo amesema kuwa msaada huo ni mkubwa sana kwani kuna watu wana uwezo lakini hawajawahi kusaidia kambi hiyo.
Amesema kambi imepokea mssada kwa mikono miwili na kuwataka VETA kuwa mabalozi wa kuwambia watu wengine katika kuwasaidia.
Akitoa shukrani mmoja wa wazee wa Kambi ya Nunge Salum Ubwabwa amesema kuwa wanawake VETA wamekuwa mstari wa mbele katika kuwajali hivyo waendelee kuwa na moyo huo huo kuwakumbuka kwani wanauhitaji wa msaada.
Kaimu Msajili wa Chuo ch VETA Chang'ombe Clara Kibodya akizungumza na Wazee wa Kambi ya Nunge wakati Wanawake Chuo hicho walivyokwenda kutoa msaada Kambi hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Kaimu Msajili wa Chuo cha VETA Chang'ombe Clara Kibodya akitoa msaada kwa Wazee wa Kambi ya Nunge katika maadhimisho ya Siku Wanawake Duniani.
Wanawake wa Chuo cha VETA Chang'ombe wakiwa katika picha ya pamoja na Wazee wa Kambi ya Nunge wakati walipotembelea na kutoa msaada katika maadhimisho ya Siku Wanawake Duniani.
Afisa Kilimo na Msimamizi wa Kambi ya Wazee ya Nunge Frank Munuo akizungumza kuhusiana na historia ya Kambi hiyo wakati Wanawake wa Chuo cha VETA Chang'ombe walivyokwenda kutoa msaada kambini hapo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Macho 8.
Bidhaa mbalimbali walizozitoa Wanawake wa Chuo cha VETA Chang'ombe katika Kambi ya Wazee Nunge.
Baadhi ya a Wazee na Wanawake wa Chuo cha VETA Chang'ombe wakiwa na Wazee wa Kambi ya Nunge wakati walipotembelea ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Hivyo makala Wanawake VETA Chang’ombe watoa msaada Kambi ya Nunge
yaani makala yote Wanawake VETA Chang’ombe watoa msaada Kambi ya Nunge Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wanawake VETA Chang’ombe watoa msaada Kambi ya Nunge mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/wanawake-veta-changombe-watoa-msaada.html
0 Response to "Wanawake VETA Chang’ombe watoa msaada Kambi ya Nunge"
Post a Comment