Loading...
title : WATAFITI WAAGIZWA KUTAFSIRI TAFITI ZAO KWA LUGHA YA KISWAHILI KUWASAIDIA WAKULIMA
link : WATAFITI WAAGIZWA KUTAFSIRI TAFITI ZAO KWA LUGHA YA KISWAHILI KUWASAIDIA WAKULIMA
WATAFITI WAAGIZWA KUTAFSIRI TAFITI ZAO KWA LUGHA YA KISWAHILI KUWASAIDIA WAKULIMA
Na Woinde Shizza,Arusha
Naibu waziri wa kilimo Mh Inocent Bashungwa amewaagiza watafiti wa kilimo kuhakikisha wanatafsiri matokeo ya tafiti kwa lugha ya kiswahili ili iweze kueleweka kwa wakulima, badala ya kutumia lugha ya kiigireza ambayo mwisho wa siku haiwanufaishi wakulima.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika uzinduzi wa teknolojia ya kilimo hifadhi ijulikanayo kwa jina la CASI iliyofanyika mjini hapa.
Alisema kuwa,tafiti nyingi ambazo zimekuwa zikifanyika zimekuwa zikiandaliwa kwa lugha ya kiingireza hali ambayo imeshindwa kuwafikia walengwa wengi ambao ni wakulima ,hivyo lazima pawepo na mabadiliko hayo ili ziwafikie walengwa kwa wakati.
Alisema kuwa,teknolojia hiyo inajikita katika kuleta mabadiliko makubwa kwa wakulima hususani katika kuongeza uzalishaji zaidi kutokana na teknolojia hiyo kustahimili ukame kwa kiwango kikubwa.
Kwa upande wake mkuu wa mradi wa SIMLESA ,Dkt John Sariah amesema kuwa,mradi huo umewafikia zaidi ya wakulima elfu hamsini ,ambao wamefikiwa moja kwa moja huku zaidi ya wakulima zaidi ya elfu kumi na tano wakiwa wamepata taarifa juu ya mradi huo.
Alisema kuwa ,mradi huo ulianza kufanya kazi mwaka 2010 ambapo walifanya tafiti katika katika wilaya mbalimbali na kugundua manufaa ya mradi huo kwani unafanya kazi katika maeneo yote hasa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi huku ukiokoa muda wa mkulima kwa asilimia 50.
Nae Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania TARI ,dokta Geoffrey Mkamilo,amesema kuwa,utafiti unaonyesho kuwa teknolojia hiyo ina manufaa makubwa kwa wakulima na tayari imeshaonyesha matunda kwa baadhi ya wakulima ambao wameshaitumia teknolojia hiyo .
Dokta Mkamilo amesema kuwa,watahakikisha teknolojia hiyo inawafikia wakulima wote ili waweze kunufaika na kuongeza uzalishaji zaidi ,ambapo watahakikisha wanaingiza utaratibu wa kuhaulisha teknolojia hiyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa utafiti kituo cha selian ambao ndio walioibua teknolojia ya kilimo hifadhi dokta Joseph Ndunguru amesema wanahitaji teknolojia hiyo iwafikie wakulima wengi ili iweze kuongeza uzalishaji wa chakula ,hata kuongeza malighafi kwenye viwanda.
Bi Rehema hasan ni mkulima kutokea mviwata morogoro ambao ni mmoja wa walionufaika na mradi huo amesema baada ya simlesa kuwapelekea mradi huo wamenufaika kwa kiwango kikubwa cha uzalishaji wa mazao kufuatia elimu waliyopatiwa.
Naibu waziri Wa Kilimo Innocent Bashugwa akizungumza na waandishi Wa habari mara baada ya kuzindua rasmi teknologia ya Kilimo hifadhi .
Katibu tawala Mkoa wa Morogoro Clifford Tandari akizungumza namna wananchi wa mkoa wake walivyoelimishwa wakati wa utafiti huo
Mwenyekiti Wa kamati ya kudumu ya Bunge Kilimo ,mifugo na maji Mohammed mkiwa akito ufafanuzi wa jambo katika katika uzinduzi huo
Mkurugenzi wa kituo cha utafiti seliani Josephy Ndunguru akizungumza na waandishi kuhusu mipango yao mbalimbali baada ya uzinduzi
Hivyo makala WATAFITI WAAGIZWA KUTAFSIRI TAFITI ZAO KWA LUGHA YA KISWAHILI KUWASAIDIA WAKULIMA
yaani makala yote WATAFITI WAAGIZWA KUTAFSIRI TAFITI ZAO KWA LUGHA YA KISWAHILI KUWASAIDIA WAKULIMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATAFITI WAAGIZWA KUTAFSIRI TAFITI ZAO KWA LUGHA YA KISWAHILI KUWASAIDIA WAKULIMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/watafiti-waagizwa-kutafsiri-tafiti-zao.html
0 Response to "WATAFITI WAAGIZWA KUTAFSIRI TAFITI ZAO KWA LUGHA YA KISWAHILI KUWASAIDIA WAKULIMA"
Post a Comment