Loading...
title : WATU NANE WAPATA MAJERAHA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA VIGWAZA
link : WATU NANE WAPATA MAJERAHA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA VIGWAZA
WATU NANE WAPATA MAJERAHA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA VIGWAZA
NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE
WATU nane wapata majeraha baada ya gari la abiria , mali ya kampuni ya Friends ikitokea Dar es salaam kuelekea Kampala nchini Uganda kupata ajali ,eneo la Kwazoka, kata ya Vigwaza, Chalinze mkoani Pwani.
Aidha dereva wa gari hilo lenye namba za usajili, UAY 458 F aina ya Scania ,Bashiru Telu mkazi wa nchini Uganda amekimbia baada ya kutokea ajali hiyo.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, ACP Wankyo Nyigesa, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo mchana march 18,mwaka huu na kusema gari hiyo ilikuwa na abiria 42.
Alieleza, gari hiyo iliacha njia na kupinduka na kusababisha majeruhi hao ambapo chanzo cha ajali ni dereva huyo kujaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari.
Wankyo aliwataja waliopata majeraha kuwa ni Kubo Zuberi (24) aliyepata jeraha katika mkono wa kulia mkazi wa Uganda ,Rudigo Benjamin (24) na Aisha Salin (34) mkazi wa Dar es salaam ameumia kichwa.
Wengine ni Theonestina Gedioni (29) mkazi wa Tabata ,Baiga Jacquie (30) mkazi wa Uganda, Nasra Amani (12) mkazi wa Dar es salaam, Farouqs Natkunda (22)mkazi wa Uganda na Hassan Omary mkazi wa Mbezi Dar es salaam.
"Majeruhi hao walikimbizwa katika kituo cha afya Mlandizi, ambapo wanaendelea na matibabu "alifafanua Wankyo.
Kamanda huyo alitoa rai kwa madereva wa vyombo vya moto kutii sheria za usalama barabarani.
Vile vile wasafiri wanaotumia vyombo hivyo kuendelea kuwafichua madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani ili waweze kuchukuliwa hatua kwa kupiga namba za makamanda wa mkoa wa wakuu wa usalama barabarani.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, ACP Wankyo Nyigesa
Hivyo makala WATU NANE WAPATA MAJERAHA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA VIGWAZA
yaani makala yote WATU NANE WAPATA MAJERAHA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA VIGWAZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATU NANE WAPATA MAJERAHA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA VIGWAZA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/03/watu-nane-wapata-majeraha-katika-ajali.html
0 Response to "WATU NANE WAPATA MAJERAHA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA VIGWAZA"
Post a Comment